Kuruka dhamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuruka dhamana

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by kande kavu, Dec 3, 2011.

 1. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waungwana naomba mawazo yenu.

  Kuna dogo langu hivi ninavyoandika liko Segerea mahabusu kwa tuhuma za Cyber Crimes(Limekwiba kwa mtandao).Kifupi nimetoka nalo mbali ikiwa ni pamoja na kulitafutia elimu lakini kwa kuwa la kuvunda ni la kuvunda halikuambulia kitu shule.Nimesumbuka sana kuliweka katika misingi ya maadili kwa namna zote lakini wapi, na badala yake dogo haaminiki kwani ni mzuri sana wa fix.Kitambo nyuma lilipata soo jingine na mie sikuwa tayari kuliwekea dhamana na hivyo dogo wangu mwingine akaliwekea na kwa kiasi siku ya kesi yake ilikuwa ni lazima kijasho kikutoke kujua yuko wapi.Nimepata elimu ya msingi kwa hela za baba wa dogo hili.Niko njia panda,niliache licheze na kesi yake toka mahabusu, au nilidhamini ilihali nikijua kuwa linaweza kukimbia na mimi nikabaki na msala na mamlaka za serikali? Ikitokea amesepa nini madhara kwa mimi mdhamini wake?
   
 2. m

  moshingi JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawapenda sana wanasheria kwa sababu wamebaki kimya muda mrefu bila kuijibu
  thread yako!! Bila shaka ni kwa sababu katika sura yake halisi ya nje haina jambo
  lolote linalohitaji ushauri wa kitaalamu kutoka kwa kwa wanasheria wetu waliomo
  humu. Big Up!!
  Hata hivyo ningependa ufafanue ni kosa gani aliloshitakiwa nalo huyo dogo, maana
  CYBER CRIMES ni dhana ya jumla, ambayo inajumuisha wizi wa mali kupitia mfumo
  wa kompyuta, uharamia wa kazi za ubunifu, usambazaji wa picha za ngono, kashfa/
  matusi/vitisho kupitia mtandao wa kompyuta, kula njama kupitia mtandao, nk.
  Aidha sasa niwaalike wanasheria wenzangu wajadili ili kila mtu humu apate mwanga
  Je, Tanzania inayosheria inayotambua uwepo wa "Cyber Crimes"?
  Mfano katika Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya sheria zetu, imeelezea sifa ya vitu
  vinavyoweza kuibika kuwa lazima iwe ni mali,yenye thamani, inayohamishika(inayoshikika"tangible"),
  ya mtu mwingine nk.
  Sasa swali je electronic money(e-money) inazo sifa za kuibika kwa mujibu wa sheria yetu?
  je inapohamishwa huwa ni mali ya nani? benki au mwenye A/C au wamiliki wa mitandao?
  Napenda nitoe hongera sana kwa Adamu Mambi ambaye muda mrefu ametoa wito itungwe sheria
  maalumu itakayoratibu matumizi na makosa ya mtandao, na pia itakayounda chombo maalumu cha
  kushughulika na uzuiaji,upelelezi na mashitaka ya makosa ya Mtandao.

  KARIBUNI WASOMI WENZANGU TULIJADILI HILI
   
 3. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu. Tuhuma za dogo hili ni kuhamisha fedha kutoka kwa akaunti ya simu pesa ya mtu mwingine, kwenda kwenye akaunti alizobumba mwenyewe, kisha kutumia pesa hizo. Hebu wazee wa sheria shusheni mautaalamu yenu.
   
 4. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nijuavyo mm Tz bado hatuna sheria za Cyber crimes... Ila huu ni wizi wa kimataifa, sheria za kimataifa zimeelezea. Hebu google International Criminal Law utapata maelezo ya kutosha.
   
Loading...