Kurudisha pesa kwa mtoaji (Hasa katika wizara ya Maliasili) bila hivyo hutotumiwa pesa

niibada

Member
Jul 6, 2012
40
6
Naomba kuuliza nasikia kila anayetumiwa pesa za kazi (mfano za doria, kueweka uzio wa moto,kukusanya maduhuri nk) lazima arudishe fungu (kwa wale wanaoidhinisha matumizi/kupanga matumizi) ndo Meneja/mkuu wa kituo husika ataendelea kutumiwa tena mafungu naomba anayefahamu ukweli anifahamishe wanajamii forum
Pili naomba kuelezwa Retirement( Mapato na Matumizi yake kwa kuzingatia waraka wa fedha) inakuwaje utawaandika na wale uliowarudishia fungu ili awamu nyingine wakugawie tena? Au fungu la kurudisha huwa limeandikwa katika barua ya Imprest?/masurufu unayoletewa?
Na je hii ndo tabia ya wizara zote? au Maliasili pekee? Je tabia hii ni kawaida ya utendaji wa serikalini kwa wanaofanya kazi huko?
 
Uhh labda utumie lugha nyingine hata kama ni kilugha, maana hapa hata hueleweki unauliza nini ? Unatumiwa hela za kazi ? Are you talking about cash advances, allowances au imprest ? Retirement ina mapato na matumizi ? Seems like unaongelea imprest (madurufu) na kama ni hizo basi taratibu za fedha sehemu nyingi (unless uwe ni kigogo) ni kuwa huwezi kuchukua imprest ya pili kabla hujarudisha ya kwanza !

Na wewe mwenzetu upo wapi ( naona umejiunga juzi tuu) mpaka utumiwe fungu kila mara ? Au upo sehemu unakamata twiga na furo zaidi kwa ajili ya mauzo awamu ya pili ( maana hata hujui namna ya kurudisha madurufu na kwa nani ??? )
 
Masurufu sio Madurufu
 
Back
Top Bottom