kessy kyomo
Member
- Feb 1, 2011
- 72
- 11
[h=3]Kuropoka kumetuathiri CCM-Guninita[/h]
Na Anneth Kagenda
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, kimesema wamepata madhara makubwa kutokana na baadhi yao kuropoka na kutoa siri za chama hicho
hadharani kuliko vyama vya upinzani.
Kimesema vyama vya upinzani vimekuwa na siri, na havipendi kusema mambo yao hadharani kama wanavyofanya wana CCM.
Hayo yalisemwa juzi na na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. John Guninita, wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Tawi la Mwembe Simba katika Kata ya Charambe na Mianzini Manispaa ya Temeke.
Alisema umefika wakati wanachama wa CCM kufuata katiba ya chama chao ikiwa ni pamoja na kuelekezana ndani ya vikao badala ya kuzungumza masuala ya ndani barabarani, jambo linaloweza kusababisha kubomoka kwa chama hicho.
"Sisi ndio tuna matatizo ambayo yanaweza kusababisha kubomoka kwa chama chetu, ni nani amewasikia wapinzani wakiropoka barabarani?
Lakini sisi tunashindwa kuelezana kwenye vikao badala yake tunaropoka! Acheni kufanya hivyo tumieni vikao kuelezana kila mtu alipokosea," alisema Bw. Guninita.
Aliwataka wanachama hao kuacha tabia ya rushwa na kusema kuwa hivi sasa wamejipanga vyema kuhakikisha wanakosoa tabia hiyo ndani ya CCM.
Alisema chama hicho hakitasubiri mtu akamatwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) badala yake atakayeonekana anafanya hivyo atachukuliwa hatua kali.
"Rushwa iko mara mbili, kwenye serikali pamoja na kwenye chama, lakini hasa ni serikali na Taasisi zake kuanzia kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa hadi juu.
Miradi inakuja ya mfano ya sh. milioni tano, lakini mtu anaandika milioni 15/-, mambo haya hatutayavumilia hata kidogo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa, tuna katiba inayotuongoza," alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka kesho wa chama hicho kila mtu atachaguliwa kwa sifa yake na si kwa kutoa rushwa na kusisitiza kuwa kigezo kikubwa kitakuwa ni uwezo wa mtu na uaminifu.
Source:Majira