Kurekebishana: Lema badilika

We si uko nje ya nchi? Mambo ya huko nyumbani huyajui unayasikia tu!
 
Sasa wewe ulitaka lema aende america akaongee kichaga? mtu hana elimu, anajua nini kuhusu uchumi wakati yeye kapitia biashara za panya road. We hukuona ile picha alivyo chanua kwenye bonet ya gari? Itafute ndio utajua akili yake iko wapi.
 
Mimi kwa uwazi sio CCM wala Chadema mimi sina Chama. Kwa uwazi vilevile nampenda Lema ni kijana mwenzangu na ni mbunge ambaye anaweza kubadilisha Arusha na kuwa ya uwazi na kuleta maendeleo. Ukweli ni kwamba Lema ni lazima arekebishwe na mimi nimeona ni muhimu kusema ukweli badala ya kuwa mnafiki hapa.

Kazi moja wapo ya Lema ni kufanya kila namna ya kuongeza kipato kwa wana Arusha na wana Arusha kuanzia Wafanya biashara wa hotel na machinga wote wanategemea utalii. Sijawahi kumuona Lema kwenye mjadala wowote wa kukaribisha wageni, sijawahi kumuona Lema nje hata mara moja akikaribisha watu Arusha na sijawahi wahi kumuona Lema anafanya mkutano na Wafanyabiashara wote kwa ujumla bila kujali vyama.

Tunaweza kupigana madongo hapa lakini Arusha ni mji wa watalii na wafnayabishara! Arusha sio Mwanza na mbunge wa Arusha anatakiwa kufanya vitu kwa Arusha. Mimi kwa mawazo yangu Lema anaweza kufanya zaidi ya anavyofanya sasa. Lema naomba nisikilize badilika ndugu yangu au utakuja kunikumbuka.
 

Nyiye ndiyo mnaouza hii nchi..... Kaulizie kwanza kwa nini Tanzanite inauzwa zaidi na nchi za SA, Kenya kwenye soko la dunia????.

Uliza kwanza kwa nini wacha na wahindi wanauza bidhaa, bei ya jumla na reja reja ni sawa????

Jiulize kwanza kwa nini watu wanauza vitu barabarani na si kwenye masoko,,, au masoko yako wapi???

Na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya masoko yako wapi????

Je wewe huko nje unafanya nini??? au ndiyo nyie mnaiuza nchi hii kisisrisiri???
 
Tumewazoea ninyi, mnafikiri mnajua kila kitu.
Kama ni mshauri wa Lema basi jua linawachea.
Lema is no more. politically!

Mwacheni Lema apumzike kwa kuhutubia vigenge vya watu waili watu vichochoroni.
 
Bado namshauri Lema mdogo wangu vilevile! ni kwa manufaa ya Arusha
 
Sasa wewe ulitaka lema aende america akaongee kichaga? mtu hana elimu, anajua nini kuhusu uchumi wakati yeye kapitia biashara za panya road. We hukuona ile picha alivyo chanua kwenye bonet ya gari? Itafute ndio utajua akili yake iko wapi.

kama akili yako imekwisha muazime hata mmeo basi ili ukija kutoa mchango useme vitu vya maana. Ni hayo tu!
 

Huelewi mazingira ya siasa za Tanzania, hasa Arusha, ungejua context ungeweza kushauri vizuri, hata hivyo si kosa lako huishi Tanzania.
 
Jamaa anakuambia eti yeye hana chama. Mwizi mkubwa. Hata Bwana Benson Bana nayeye anasemaga hana chama wakati kujulikana chama cha mtu hakuhitaji spana wala nyundo, matendo yako ndio mpango mzima jombaaa. Halafu msidhani ninyi mlioko nje ya nchi eti mnayo akili kuliko walioko home!
 
lema akibadilika tabia Arusha itamchukia
 
Wazo zuri mijitu inayoangalia kimtazamo wa kichama hayatakuelewa.Lema kubali kupokea ushauri wa huyu jamaa
 
Swala utalii aulizwe JK ndiyo huenda huko diaspora kutalii na kutangaza utalii. Swala la makampuni ya biashara ya utalii waulizwe Kagasheki, Membe na Sita na Mkangara na mkuu wa mkoa, wilaya, wakurugenzi na meya. Swala la mahoteli waulizwe Nagu, Wassira, Kagasheki, Pinda, JK, na Kigoda, TIC, TCAAA. Kwani serikali yote ipo. Si kazi ya Lema kwa sasa.
 
Ushauri wa kijinga tu

kamanda mzima, wanamfundisha nidhamu ya uoka kamanda hahahahahaha lema ongeza moto naona mavuvuzela una wachoma alianza nape sasa naona wengi wanafata..
 
kwanini ushauri kama huu siuoni kwa shibuda, thelasini na wengine inamaana wako vizuri sana kwenye majimbo yao au unafiki umewajaa..
 
Kamundu, kulikuwa na ulazima wowote kujitambulisha unaishi nje? Imeongeza chochote kwenye uzito wa hoja yako?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…