Kurejea Lowassa CCM, siasa za Tanzania na uchaguzi mkuu wa 2020

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
KUREJEA LOWASA CCM, SIASA ZA TANZANIA NA UCHAGUZI MKUU WA 2020
Ukiweka ushabiki pembeni hutasita kuona uzito wa uhamaji Lowasa kuanzia 2015. Hakika CDM ilipata kura milioni 6 kutokana na mvuto WA Lowasa 2015. Hakika Lowasa aliitikisa CCM 2015 japo CCM ilijitahidi kuonyesha hakuwatikisa. Ukweli huu utabaki kuwa kumbukumbu ya kihistoria katika siasa za nchi yetu. Ilikuwa mara ya kwanza CCM kukabiliwa Kwa kiwango kile katika uchaguzi. Makovu yaliyotokana na kuhama kwake bado yangalipo. Usaliti unaoendelea ndani ya CCM asili yake kubwa ni mhamo ule. CCM itapaswa kutafakari kwa kina namna ya kudhibiti makada wenye nguvu kuhama haswa kipindi cha kampeni za uchaguzi. Kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa. Na ikiwa kweli Lowasa 'karudi nyumbani" kwa moyo mkunjufu basi anapaswa kuomba chama radhi kwa kukisababishia makovu. Na ashiriki kutibu makovu yaliyobaki hapa na pale. Mfano Lowasa anatakiwa avunje kambi yake rasmi maana bado ipo. Hapo ndipo "mtoto mpotevu" atakuwa amerudi nyumbani kwao! Lakini pia itamsaidia yeye na CCM kama atatangaza rasmi kuachana na dhamira ya kwenda Ikulu. Awe Mzee mstaafu wa chama chake. Atarejesha sehemu kubwa ya heshima aliyoipoteza.
Lakini hakuna walioumia kwa kuhamahama Kwa Lowasa kama CHADEMA. Wanaweza kujibaraguza na kumdhihaki. Na hapo ndio yanapoanzia maumivu ya CHADEMA. Kumbeza LOWASA Kwa sasa kutawachafua mno kwa makundi muhimu. Kundi la Kwanza ni la wanachama ambao tangu Alfa walipinga ujio wa Lowasa wakapuuzwa. Mbowe aliwaita "watu wasiopima mambo kwa kina"! Leo wao ndio wamedhihirisha walipima mambo kwa kina. Ile Imani "kamanda Mbowe" hakosei inatoweka. Kundi hili litataka kuonyesha lilikuwa sahihi.
Kundi la pili ni wafadhili na mataifa ya nje. Watajiuliza ikiwa kiongozi waliyempokea Kwa mbwembwe na kumtambulisha "waziri mkuu mstaafu" yamemshinda lazima kuna udhaifu. Mara kadhaa Lissu amesikika nje akisifia "mawaziri wakuu wastaafu" kuondoka CCM! Kimataifa athari ya kuondoka Lowasa kwao ni kubwa mno. Sema inahitaji akili ya ziada kuliona hili. Hili ni swali watakalokumbana nalo Kwa mabalozi na vyombo vya habari vya nje. Hawawezi kudai kanunuliwa maana wimbo huo hautaendana na sherehe!
Hasara nyingine ambayo CHADEMA itajutia ni kumpa Lowasa ujumbe wa Kamati Kuu. Kamati Kuu ya Chama chochote ndiyo yenye kuidhinisha mikakakati (halali na haramu) na kupokea taarifa za utekelezaji. Ni taasisi inayotunza siri nzito za Chama husika. Inajadili matumizi ya fedha na Mali za Chama Kwa hiyo inajua nani mbadhirifu. Siri zote hizo SASA ziko mikononi mwa Lowasa. Bila Shaka kaenda nazo CCM. CHADEMA hawawezi kujitetea kuwa hajui! Kama Kamati Kuu haijadili haya basi ina maana Kamati Kuu ya CHADEMA ni kanyaboya? Hakika lazima CHADEMA iingie hofu. Hauwezekaniki Lowasa asijue nani haswa alimshambulia Lissu! Lazima Lowasa anajua ni kwa nini dereva alitoroshwa! Lazima Lowasa anajua ukweli kuhusu Ben Saanane! Haiwezekani Lowasa asijue nini haswa kiliwafika Chacha Wangwe na wengine waliopoteza maisha katika MAZINGIRA ya utata. Lazima Lowasa anajua waliolipua Bomu Arusha. Lowasa anajua nani waliendesha mauaji Rufiji. Hofu imetanda ndani ya CHADEMA ila wanachama hawajui.
Hasara inayowasubiri CHADEMA ni 2020. Zile kura milioni 6 zitarudi zilikotoka. Ni huyu Lowasa watu walimuita raisi wa mioyoni. Ni huyu Lowasa watu walipiga deki lami asipate mafua. Ni huyu Lowasa watu waliapa ALIPO NA WAO WAPO! Hawa hawakupigia Kura CHADEMA. Walimpigia Lowasa!
Mtihani wa mwisho Kwa CHADEMA ni huu: Lowasa alienda CHADEMA na waliokuwa "TEAM LOWASA" alipokuwa CCM. Hawa bado wapo CHADEMA tena wengine wako matawi ya juu. Je CHADEMA itawafukuza? Itawatoa matawi ya juu? Hakutatokea mpasuko kati ya "wakuja" na "wazawa"? CHADEMA inathubutu kwa mfano kumtenga Sumaye na Mahanga? Hapohapo inaweza kuwaamini kuliko walivyomuaminia Lowasa? Leo hii Baraza na Kamati Kuu CHADEMA zikikutana zitathubutu kuongea mambo nyeti wakati Sumaye na Mahanga wamo kikaoni? Au watawatoa nje?
Huu ndio uzito wa hamahama ya Lowasa. Unaweza ukachukia au ukafurahi ukipendezewa!
Ushauri wangu Kwa Lowasa: usijibizane na wao. Waache wahangaike na msiba wa kujitakia.
 
Itakuwa ni uchaguzi wakwanza wa aina yake, mosi: vikundi vya wanaccm watashindana kwa pesa, pili: manunuzi ya kufuru dhidi ya upinzani utafanyika kuliko uliopita. Mwisho: Matokeo ya mshindi ndani ya CCM hayatategemea kura, vivyo hivyo na yakitaifa pia.
THE RETURN OF A SAILOR.
 
Back
Top Bottom