Kurasa Darasa TBC Maureen Nanago na Mohamed Said

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,916
30,259
KIPINDI ''KURASA DARASA'' TBC MAUREEN MINANAGO NA MOHAMED SAID WANAKICHAMBUA KITABU CHA JUDITH LISTOWEL, ''THE MAKING OF TANGANYIKA,'' (1965)

Kitabu hiki cha Lady Judith Listowel kwa mara ya kwanza nimekisikia kwa Ally Sykes katika miaka ya 1980 kisha nikamuuliza Juma Mwapachu.

Juma Mwapachu akanifahamisha kuwa anakifahamu na baba yake Hamza Kibwana Mwapachu akikipenda sana.

Juma Mwapachu akaniambia kuwa kitabu hiki sifa yake kubwa ni kuwa kimeeleza historia ya Tanganyika na harakati za kudai uhuru kutoka kauli za wenyewe walioupigania uhuru.

Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kulikuwa na nakala moja tu na kwa wakati ule kitabu hiki kilikuwa ''out of print,'' yaani hakipatikani.

Hii ndiyo nakala niliyosoma mimi na kwa hakika kitabu kilinisisimua pakubwa.

Leo TBC waliponitembelea nyumbani ili tujadili kitabu kimoja ambacho watazamaji watanufaika na maudhui yake nilichagua kutoka Maktaba, ''The Making of Tanganyika.''

Mwandishi Judith Listowel alikuwa mke wa Gavana Listowel wa Ghana.

Peter Colmore rafiki na mshirika mkubwa wa Ally Sykes katika biashara toka mwaka wa 1945 aliniambia tukiwa katika maongezi nyumbani kwake Muthaiga, Nairobi kuwa yeye ndiye aliyemuunganisha Judith Listowel kwa Ally Sykes kwa ajili ya utafiti wa kitabu chake.

Ally Sykes alimpokea Judith Listowel Dar es Salaam akitokea Uingereza akamfikisha kote na kumkutanisha na wazalendo wengi waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa mahojiano.

Hii ilikuwa mwaka wa 1963.

Kitu cha kusikitisha sana katika utafiti wa Judith Listowel ni kuwa Abdul Sykes hakutaka kuzungumza kuhusu mchango wake katika kuunda TANU kwa hiyo alikuwa akimkwepa.

Lakini Judith alipofanikiwa kumtia mkononi Abdul nyumbani kwake Magomeni Mikumi hakuambulia lolote la maana na Listowel alitambua kuwa Abdul Sykes hataki kusema anayoyajua kuhusu historia ya uhuru.

Nilipokuwa napitia barua za Listowel katika Nyaraka za Sykes nilisoma haya masikitiko katika barua yake moja aliyomwandikia Ally Sykes wakati huo keshamaliza utafiti na karejea London.

Barua ya kwanza kutoka kwa Listowel kwa Ally Sykes kutoka London ni ya mwaka wa 1962 na ya mwisho alimwandikia mwaka wa 1965.

Tumezungumza mengi katika kitabu cha Listowel kuanzia Vita Vya Abushiri na Mkwawa dhidi ya Wajerumani (mwishoni 1880s), Vita Vya Maji Maji (1905 - 1907), Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918) na VitanVya Pili Vya Dunia.

Tumewazungumza askari wawili kutoka Tanganyika waliopigana Vita Vya Kwanza, Kleist Abdallah Sykes na Schneider Abdillah Plantan pamoja na Kamanda wao General Von Lettow Vorbeck.

Tumemzungumza Gavana Donald Cameron aliyesaidia kuasisiwa kwa African Association (1929).

Tumewazungumza ''Makerere Intellectuals,'' hii ni sura ya kuvutia sana katika kitabu kwa kuwa ndani ya sura hii ndipo Listowel alipowaeleza vijana wanasiasa wa TAA waliokuja kuwasha moto wa ukombozi: Hamza Mwapachu, Julius Nyerere, Andrew Tindegebage na Madaktari Watano - Joseph Mutahangarwa, Luciano Tsere, Vedasto Kyaruzi, Wilbard Mwanjisi na Michael Lugazia.

Hawa walijipa jina, ''Action Group.''
Naamini watazamaji watakipenda kipindi hiki.

Kipindi hiki kitarushwa na TBC na wameahidi kutengeneza ''jingle,'' kukitangaza kipindi kabla hawajakirusha.

Picha ya kitabu toleo la pili, Mwandishi na Maureen Nanago wa TBC, Peter Colmore na Ally Sykes, Paris (1963) na Peter Colmore na Mwandishi, Nairobi (1995).

20190722_071154~3.jpg
Screenshot_20210105-180030.jpg
20210105_114729.jpg
Screenshot_20210105-180230.jpg
 
Back
Top Bottom