Kura zetu kwa Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura zetu kwa Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jibaba Bonge, Sep 30, 2010.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tumempata mwanana, mpambanaji hodari
  Mzalendo pia mwana , mafisadi kukabiri
  Utani kwake hakuna, kweli yeye dakitari
  Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa

  Tumpe kura kwa wingi, uchumi kuukomboa
  Tumpeni nyingi kingi, nchi kuisimamia,
  Avuke vyote vigingi, mtandao kuubomoa
  Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa

  Siku ile ikifika , kura tumpe Slaa
  Yeye ndiye msifika , mafisadi kwao balaa
  Wezi watetemeka, walisikiapo ‘Slaa'
  Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa

  Anahaha makamba , kama anakata kamba
  Mafuriko yamkumba, anenayo yote pumba
  Chama chake kinayumba, sasa kutumia ndumba
  Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa

  Pipozi pawa ni sasa, kona zote yasikika
  Ukombozi ndiyo sasa, ccm kuizika
  Nchi yetu kutakasa, wakati ndo umefika
  Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa
   
 2. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hii Imetulia Jibaba. Nashauri wale wenye kuweza wazidi kuusambaza huu ushauri ni ujumbe mkubwa kwa watz wapenda mabadiliko.
   
 3. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  duly noted
   
 4. h

  hagonga Senior Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF, hii nimeipenda sana, have circulated already.
   
 5. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tuko pamoja
   
 6. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  nice of you endeleza mapambano
   
 7. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  si tumtafute andanenga (RTD) akaimbe kabla ya mikutano ya slaaaa
   
Loading...