Kura za mauwaji ya albino zapotea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura za mauwaji ya albino zapotea!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msongoru, May 14, 2009.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na Claud Mshana

  MATOKEO ya kura za siri za kuwabaini wauaji wa albino, majambazi na wauza dawa za kulevya iliyopigwa Machi mwaka huu bado hayajafika kweye Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inayotakiwa kutangaza, ilifahamika jana.

  Tayari baadhi ya wanasiasa wamedai kura zile zilikuwa danganya toto ya serikali.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam, Afisa Habari Mkuu wa Wizara hiyo, Othuman Othuman alisema mpaka sasa Wizara haijapokea taarifa rasmi ya zoezi hilo.

  Zoezi la kupiga kura za maoni kuwabaini wauaji wa albino lilifanyika nchi nzima kuanzia Machi 31 mwaka huu kufuatia kukidhiri kwa vitendo vya uhalifu na mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, ambapo kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi kwa kipindi cha miaka miwili, karibu walemavu wa ngozi 43 waliuawa.

  Upigaji kura za siri ulifanyika katika kanda saba ambazo ni Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, na Shinyanga chini ya kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mikoa.

  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ilijumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa na Ruvuma wakati kanda ya kati ilikuwa na mikoa ya Dodoma na Singida na , Kanda ya Kusini ilikuwa na mikoa ya Lindi na Mtwara.

  Kanda ya Magharibi ilihusisha mikoa ya Kigoma na Tabora, wakati Kanda ya Kaskazini ilikuwa na Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara na Kanda ya Mashariki ilikuwa na mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
   
 2. H

  Hume JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Serikali ilikuwa inatuchezea shere. Haikuwa na maana yoyote zaidi ya kupoteza muda na mali za watu bila mkakati wowote wa kimsingi katika kufanya hilo.
   
Loading...