Kura za Maoni Tanga: CCM yafutilia mbali matokeo ya uchaguzi kura za maoni Handeni

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

KIMENUKA TANGA! CCM YAFUTILIA MBALI MATOKEO YA UCHAGUZI KURA ZA MAONI HANDENI,AMBAPO MTOTO WA DR KIGODA ALIKUWA MSHINDi
[h=1]
[/h]
1.jpg



Kamati Kuu ya CCM imefuta matokeo ya kura za maoni katika Jimbo la Handeni, mkoani Tanga ambako Omar Abdallah Kigoda ambaye ni mtoto wa mbunge wa zamani, marehemu Abdallah Kigoda alikuwa ameshinda.


Akizungumza jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema jana kuwa kutokana na kufutwa kwa matokeo hayo, uchaguzi wa kura maoni katika jimbo hilo unarudiwa leo.
Alifafanua kuwa wagombea 11 waliwania nafasi hiyo lakini wawili kati yao, Kigoda na Hamis Amad Mnondwa walipata kura zaidi kuwashinda wenzao.


Mkutano mkuu wa jimbo la Handeni, ulimchangua Omari Kigoda kwa kura 296 akiwashinda wenzake wawili Hamisi Mnondwa na Athumani Lukoya waliokuwa wamechujwa kutoka miongoni mwa wanachama 11 walioomba nafasi hiyo.


?Lakini matokeo yanaonyesha hakuna mshindi aliyepata kura za kuridhisha kuingia katika ushindani na vyama vingine, ndiyo maana Kamati Kuu imeamua urudiwe,? alisema bila kutaja idadi ya kura walizopata wagombea hao.


Mchakato huo wa kupata mgombea unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo, Dk Abdallah Kigoda kilichotokea Oktoba 12, mwaka huu nchini India.


Nape alisema marudio hayo ya kura za maoni yatasimamiwa na makada watatu wa CCM, Dk Maua Daftari, Dk Emmanuel Nchimbi na Abdallah Bulembo.


Nape alisema Kamati Kuu inaendelea na kikao chake cha siku moja ambacho kina ajenda ambazo hakutaka kuzitaja. Kamati Kuu imefanya uamuzi huo huku kukiwa na sintofahamu juu ya chama hicho kuanza ?utaratibu mpya? wa kuwateua watoto wa vigogo wa chama hicho wanaofariki dunia wakiwa wabunge au wagombea, kuwania nafasi iliyoachwa na wazazi wao.


Mbali na Omary, Goodluck Mtinga, mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi) Celina Kombani naye amepitishwa na chama hicho kugombea ubunge katika jimbo la Ulanga.


Utaratibu kama huo ulitumika katika Jimbo la Kalenga mwaka 2014, CCM ilipomsimamisha Godfrey Mgimwa, mtoto wa marehemu Dk William Mgimwa, kugombea ubunge katika jimbo hilo lililokuwa likishikiliwa na baba yake.


Mwaka 2012, CCM pia ilimteua Sioyi Sumari kugombea ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki kuziba nafasi iliyoachwa na baba yake, marehemu Jeremiah Sumari.

source Jamii Yetu Bongo
 
Suala ni sifa. Kama awana basi una rai yenye mashiko. Vinginevyo nawe pia utaulizwa, je pale ambapo mzazi alifariki na mtoto wake hakusimama toka tupate uhuru ina maana kuna mbinu za kuwazuia hao wana wasishiriki ktka Siasa?
 
Back
Top Bottom