Kura za Majimbo zinachafua demokrasia Marekani

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,306
6,514
Taifa kubwa lenye kujipambanua kama baba wa demokrasia duniani, lenye idadi ya watu zaidi ya 324 milioni kwa makadirio ya sasa au 309 milioni kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2010, linawezaje kuchaguliwa Rais na watu 538 tu?

Tena katika hao watu 538, mtu anahitaji kupigiwa kura na watu 270 tu ili aweze kutangazwa kuwa Rais wa Marekani. Nchi kubwa inayoshika nafasi ya tatu kwa idadi ya watu duniani, nyuma ya China na India, eti Rais wake anapatikana kwa kupigiwa kura na watu 270 tu.

Watu 538? Ndiyo, hao ni wajumbe wa Kura za Majimbo (Electoral College) ambao ndiyo tabaka lenye mamlaka ya kikatiba kupiga kura za moja kwa moja kuchagua Rais wa Marekani. Watu hao 538 huitwa pia wachaguaji (electors), maana kura zao ni turufu.

Mamilioni ya wananchi wa Marekani hupiga kura kuonesha tu mgombea anayependwa na watu. Fursa yao pia huwa ni kuchagua mjumbe wa Electoral College. Hapa ndipo demokrasia ya Marekani inapoingia utata.

Katika hili, uchaguzi wa urais Marekani una utani mwingi. Mamilioni ya wananchi wanapiga kura zisizo na thamani. Watu 538 ndiyo wenye thamani. Watu 270 ndiyo wanaweza kumfanya mtu awe Rais wa Marekani kwa miaka minne.

Mfumo huo wa wachache kufanya uamuzi kwa ajili ya taifa zima, umesababisha aibu ya pili ndani ya kipindi cha miaka 16. Uchaguzi wa Novemba 8, mwaka huu, idadi kubwa ya wananchi imeonekana kumhitaji mgombea ambaye amenyimwa kura na wajumbe wengi wa Electoral College.

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democrats, Hillary Clinton, ndiye ambaye amepata kura nyingi za wananchi lakini Rais Mteule, Donald Trump wa Republican, anasubiri kuapishwa Januari 20, mwakani kwa sababu ya uamuzi wa watu 306 wa kundi la Electoral College waliomchagua.

Hillary anabaki kuwa Rais wa mioyo ya Wamarekani, kwa akufuatisha msemo maarufu Tanzania, lakini hatakwenda Ikulu ya nchi hiyo, White House, wala hatakalia kiti kwenye ofisi ya Rais wa Marekani, The Oval Office. Atatambulika kuwa mwanamke mwenye nguvu zaidi kuwahi kugombea urais wa taifa hilo.

Kilichomwanagusha ni kuchaguliwa na wajumbe 232 tu wa kura za majimbo. Akipungukiwa wajumbe 28 tu ili ashinde urais. Mamilioni ya Wamarekani waliopaza sauti kupitia Hillary, sauti zao zinanyamazishwa kwa ukosefu wa kura 28 kati ya 538.

Hesabu zinaiaibisha Marekani

Kura za wananchi wa Marekani mwaka 2016, zaidi ya 60.5 milioni, sawa na asilimia 47.6 zimemchagua Hillary, wakati Trump amepigiwa kura na wananchi 60 milioni, sawa na asilimia 47.6.

Hii maana yake ni kuwa kama Marekani ingekuwa inafuata sheria za Tanzania, mgombea urais kushinda kiti kwa kupata kura nyingi hata kama ni pungufu ya asilimia 50, Hillary ndiye angekuwa Rais Mteule wa nchi hiyo kwa sasa.

Marekani, watu 231 milioni wanaweza kupiga kura. Mwaka huu, watu 128 milioni walipiga kura. Mamilioni hao, kura zao ni bure kwa sababu ya wajumbe 538. Kwa idadi ya kura za wananchi, Hillary alimshinda Trump kwa kura 439,902. Hata hivyo mamia elfu hayo hayana thamani.

Ilitokea mwaka 2000, aliyekuwa mgombea urais kupitia Democrats, Al Gore alimshinda Rais wa 43 wa nchi hiyo, George Bush kwa kura za wananchi lakini Bush akaibuka mshindi kupitia Kura za Majimbo.

Uwiano wa Al Gore na Bush hautofautiani na wa Hillary na Trump. Wakati huo Al Gore alipata kura za wananchi 51 milioni, sawa na asilimia 48.4, wakati Bush alichaguliwa kwa kura 50.5 milioni, ikiwa ni asilimia 47.9. Al Gore alimshinda Bush kwa kura 543,895.

Hata hivyo, wajumbe 538 waliukorofisha umma wa Wamarekani, pale 271 walipomchagua Bush, huku 266 wakimpigia Al Gore. Maana yake ni kuwa sauti za Wamarekani 543,895 ambao walizidi wale wa Bush, zilinyamazishwa na ukosefu wa kura nne tu za Electoral College.

Mfanano wa Trump na Bush ni kuwa walishindwa kwenye kura za umma lakini wakafanikiwa kupenya kupitia Kura za Majimbo. Trump na Bush wote waliungwa mkono katika majimbo 30. Trump na Bush wote ni wafanyabiashara na wanatokeo koo zenye nguvu kiuchumi Marekani.

Tofauti ni moja tu, angalau Bush alishinda akiwa tayari ameshapata uzoefu wa uongozi wa kisiasa na utumishi wa umma. Alishinda urais wa Marekani akitoka kuwa Gavana wa 46 wa Texas. Trump yeye hajawahi kuwa kiongozi wa kisiasa wala mtumishi wa umma.

Mfanano wa Al Gore na Hillary ni kuwa wote ni watu wa karibu na Rais wa 42 wa nchi hiyo, Bill Clinton. Al Gore alikuwa Makamu wa Rais wa Marekani chini ya Clinton, wakati Hillary ni mke wa Clinton. Wote wamepigiwa kura katika majimbo 20.

Al Gore na Hillary wote wameangushwa na watu ambao wanawazidi uzoefu wa uongozi. Al Gore alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa mihula miwili kisha Makamu wa Rais kwa mihula miwili, wakati Bush alikuwa Gavana wa Texas kwa miaka mitano tu.

Hillary alikuwa seneta wa New York kwa mihula miwili, kisha Waziri wa Mambo ya Nje kwa muhula mmoja. Jumlisha na utumishi wake Ikulu kwa miaka nane kama mke wa Rais Clinton, lakini ameangushwa na mtu ambaye hajawahi kuonekana popote katika siasa za Marekani.

Ni aibu ya Karne ya 21

Makosa ya Hillary na Al Gore kushindwa licha ya kupata kura nyingi za wananchi, yanatosha kuipa Marekani aibu ya Karne ya 21. Ikiwa ni muongo wa pili wa karne hiyo tayari makosa yameshafanyika mara mbili, itakuwaje miongo nane iliyosalia?

Karne ya 20 hakuna uchaguzi hata mmoja uliingia kwenye mizengwe. Watu hawakukosoa utaratibu wa Kura za Majimbo kwa sababu wajumbe walichagua na kutoa matokeo yenye kufanana na kura za wananchi.

Karne ya 19 Marekani iliingia kwenye aibu hiyo mara tatu. Mwaka 1824, 1876 na 1888, marais walioshinda Kura za Wajumbe waliingia madarakani huku wakiwa wameshindwa katika kura za wananchi.

Andrew Jackson alimshinda John Quincy Adams katika kura za wananchi lakini Adams alishinda urais mwaka 1824, huo ukawa mshangao wa kwanza katika historia ya Marekani. Mwaka 1876, Rutherford Hayes alishindwa katika kura za wananchi na Samuel Tilden lakini akawa Rais. Mwaka 1888, Benjamin Harrison alishinda akiwa amezidiwa kura za wananchi na Grover Cleveland.

Ukifuatilia, wenye kubebwa na Kura za Majimbo mara zote ni wagombea wa Republican. Kasoro mwaka 1824 katika uchaguzi wa chama kimoja cha Democratic-Republican. Baada ya vyama hivyo kugawanyika na kupatikana Republican na Democrats, mara zote wanaobebwa ni Republican.

Mvurugano unakuja

Maandamano ya sasa kupinga ushindi wa Trump ni alama tu kuwa mtindo wa kumchagua Rais kupitia kura za watu wachache umepitwa na wakati. Huko mbele ya safari kuna mvurugano mkubwa unaweza kutokea.

Mapendekezo ya uwepo wa Kura za Majimbo ni ya Katiba ya mwaka 1787. Pengine mazingira ya watu wachache wanaoaminiwa kwa ajili ya kutunza uzalendo kwa nchi yao kipindi hicho yalikuwa na uaminifu kuliko sasa. Ndiyo maana ndani ya miaka 16 makosa yamekuwa mara mbili.

Matakwa ya Kura za Wajumbe yalikuwa na maana ya udhibiti, kwamba anaweza kutokea mgombea akawa anapendwa sana na wananchi lakini sera zake au nyendo zake zikawa hatari kwa maslahi ya nchi, kwa hiyo wajumbe wa Electoral College wanaweza kumdhibiti.

Hata hivyo, siyo kwa dunia ya sasa. Mtu anaweza kuutaka urais kisha akawekeza nguvu kubwa kwa wajumbe wa Electoral College. Wajumbe hao pia ni binadamu. Viongozi wengi Marekani wamekuwa wakikutwa na hatia za rushwa, hao wajumbe nao ni binadamu na wanaweza kushawishiwa.

Anayetaka urais akiwa tajiri kama alivyo Trump au Bush, anaweza kufadhili hata watu wanaowania ujumbe wa Electoral College ili wamfae mbele ya safari. Watu 538 ni wachache na wananunulika. Ndiyo maana wananchi wanamchagua huyu, wao wanampigia kura mwingine.

Sisemi kuwa rushwa ilitumika Marekani lakini natoa picha ya jinsi ambavyo hatari ya matumizi ya fedha kupora haki ya walio wengi ni kubwa mno kupitia Kura za Majimbo.

CHANZO: Maandishi Genius
 
Viongozi wengi Africa hamkupenda Trump ashinde kwani atadhibiti business as usual
 
Kwani Trump hawez kuongoza? Wewe hujui sera za Trump zilisababisha baadhi ya makundi hasa ya wahamiaji na Waislam kutengeneza movement ya kuharibu ushindi wake, hivyo wazawa wa Marekani walizidiwa kete na makundi hayo? Walichofanya Collage ni kufanya kile kilicho kwenye mioyo ya Wamarekani wazawa. Sion tatizo kwa wenzetu wako well organized watasonga tu
 
sijui ni kwa nini unalaumu USA kwa ufupi hamna nchi yoyote duniani wananchi wanachagua rais.Rais anachaguliwa mfumo-utawala uliopo hayo mambo sijui ya kura nikiini macho na ukiona upinzani ndio umeshika dola basi jua kuna internal conflicts ndani ya utawala unaosababisha mgawanyo-ambao hupelekea upinzani kushinda.
pili yule Mwanamke hawezi akatawala U.S.A mpaka dunia inaisha
 
Wewe unatakiwa uelewe kwamba ili upate Electors wengi lazima ushinde majimbo mengi.Kwa taarifa yako Trump anakubaliwa na majimbo mengi kuliko Clinton.
 
Taifa kubwa lenye kujipambanua kama baba wa demokrasia duniani, lenye idadi ya watu zaidi ya 324 milioni kwa makadirio ya sasa au 309 milioni kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2010, linawezaje kuchaguliwa Rais na watu 538 tu?

Tena katika hao watu 538, mtu anahitaji kupigiwa kura na watu 270 tu ili aweze kutangazwa kuwa Rais wa Marekani. Nchi kubwa inayoshika nafasi ya tatu kwa idadi ya watu duniani, nyuma ya China na India, eti Rais wake anapatikana kwa kupigiwa kura na watu 270 tu.

Watu 538? Ndiyo, hao ni wajumbe wa Kura za Majimbo (Electoral College) ambao ndiyo tabaka lenye mamlaka ya kikatiba kupiga kura za moja kwa moja kuchagua Rais wa Marekani. Watu hao 538 huitwa pia wachaguaji (electors), maana kura zao ni turufu.

Mamilioni ya wananchi wa Marekani hupiga kura kuonesha tu mgombea anayependwa na watu. Fursa yao pia huwa ni kuchagua mjumbe wa Electoral College. Hapa ndipo demokrasia ya Marekani inapoingia utata.

Katika hili, uchaguzi wa urais Marekani una utani mwingi. Mamilioni ya wananchi wanapiga kura zisizo na thamani. Watu 538 ndiyo wenye thamani. Watu 270 ndiyo wanaweza kumfanya mtu awe Rais wa Marekani kwa miaka minne.

Mfumo huo wa wachache kufanya uamuzi kwa ajili ya taifa zima, umesababisha aibu ya pili ndani ya kipindi cha miaka 16. Uchaguzi wa Novemba 8, mwaka huu, idadi kubwa ya wananchi imeonekana kumhitaji mgombea ambaye amenyimwa kura na wajumbe wengi wa Electoral College.

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democrats, Hillary Clinton, ndiye ambaye amepata kura nyingi za wananchi lakini Rais Mteule, Donald Trump wa Republican, anasubiri kuapishwa Januari 20, mwakani kwa sababu ya uamuzi wa watu 306 wa kundi la Electoral College waliomchagua.

Hillary anabaki kuwa Rais wa mioyo ya Wamarekani, kwa akufuatisha msemo maarufu Tanzania, lakini hatakwenda Ikulu ya nchi hiyo, White House, wala hatakalia kiti kwenye ofisi ya Rais wa Marekani, The Oval Office. Atatambulika kuwa mwanamke mwenye nguvu zaidi kuwahi kugombea urais wa taifa hilo.

Kilichomwanagusha ni kuchaguliwa na wajumbe 232 tu wa kura za majimbo. Akipungukiwa wajumbe 28 tu ili ashinde urais. Mamilioni ya Wamarekani waliopaza sauti kupitia Hillary, sauti zao zinanyamazishwa kwa ukosefu wa kura 28 kati ya 538.

Hesabu zinaiaibisha Marekani

Kura za wananchi wa Marekani mwaka 2016, zaidi ya 60.5 milioni, sawa na asilimia 47.6 zimemchagua Hillary, wakati Trump amepigiwa kura na wananchi 60 milioni, sawa na asilimia 47.6.

Hii maana yake ni kuwa kama Marekani ingekuwa inafuata sheria za Tanzania, mgombea urais kushinda kiti kwa kupata kura nyingi hata kama ni pungufu ya asilimia 50, Hillary ndiye angekuwa Rais Mteule wa nchi hiyo kwa sasa.

Marekani, watu 231 milioni wanaweza kupiga kura. Mwaka huu, watu 128 milioni walipiga kura. Mamilioni hao, kura zao ni bure kwa sababu ya wajumbe 538. Kwa idadi ya kura za wananchi, Hillary alimshinda Trump kwa kura 439,902. Hata hivyo mamia elfu hayo hayana thamani.

Ilitokea mwaka 2000, aliyekuwa mgombea urais kupitia Democrats, Al Gore alimshinda Rais wa 43 wa nchi hiyo, George Bush kwa kura za wananchi lakini Bush akaibuka mshindi kupitia Kura za Majimbo.

Uwiano wa Al Gore na Bush hautofautiani na wa Hillary na Trump. Wakati huo Al Gore alipata kura za wananchi 51 milioni, sawa na asilimia 48.4, wakati Bush alichaguliwa kwa kura 50.5 milioni, ikiwa ni asilimia 47.9. Al Gore alimshinda Bush kwa kura 543,895.

Hata hivyo, wajumbe 538 waliukorofisha umma wa Wamarekani, pale 271 walipomchagua Bush, huku 266 wakimpigia Al Gore. Maana yake ni kuwa sauti za Wamarekani 543,895 ambao walizidi wale wa Bush, zilinyamazishwa na ukosefu wa kura nne tu za Electoral College.

Mfanano wa Trump na Bush ni kuwa walishindwa kwenye kura za umma lakini wakafanikiwa kupenya kupitia Kura za Majimbo. Trump na Bush wote waliungwa mkono katika majimbo 30. Trump na Bush wote ni wafanyabiashara na wanatokeo koo zenye nguvu kiuchumi Marekani.

Tofauti ni moja tu, angalau Bush alishinda akiwa tayari ameshapata uzoefu wa uongozi wa kisiasa na utumishi wa umma. Alishinda urais wa Marekani akitoka kuwa Gavana wa 46 wa Texas. Trump yeye hajawahi kuwa kiongozi wa kisiasa wala mtumishi wa umma.

Mfanano wa Al Gore na Hillary ni kuwa wote ni watu wa karibu na Rais wa 42 wa nchi hiyo, Bill Clinton. Al Gore alikuwa Makamu wa Rais wa Marekani chini ya Clinton, wakati Hillary ni mke wa Clinton. Wote wamepigiwa kura katika majimbo 20.

Al Gore na Hillary wote wameangushwa na watu ambao wanawazidi uzoefu wa uongozi. Al Gore alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa mihula miwili kisha Makamu wa Rais kwa mihula miwili, wakati Bush alikuwa Gavana wa Texas kwa miaka mitano tu.

Hillary alikuwa seneta wa New York kwa mihula miwili, kisha Waziri wa Mambo ya Nje kwa muhula mmoja. Jumlisha na utumishi wake Ikulu kwa miaka nane kama mke wa Rais Clinton, lakini ameangushwa na mtu ambaye hajawahi kuonekana popote katika siasa za Marekani.

Ni aibu ya Karne ya 21

Makosa ya Hillary na Al Gore kushindwa licha ya kupata kura nyingi za wananchi, yanatosha kuipa Marekani aibu ya Karne ya 21. Ikiwa ni muongo wa pili wa karne hiyo tayari makosa yameshafanyika mara mbili, itakuwaje miongo nane iliyosalia?

Karne ya 20 hakuna uchaguzi hata mmoja uliingia kwenye mizengwe. Watu hawakukosoa utaratibu wa Kura za Majimbo kwa sababu wajumbe walichagua na kutoa matokeo yenye kufanana na kura za wananchi.

Karne ya 19 Marekani iliingia kwenye aibu hiyo mara tatu. Mwaka 1824, 1876 na 1888, marais walioshinda Kura za Wajumbe waliingia madarakani huku wakiwa wameshindwa katika kura za wananchi.

Andrew Jackson alimshinda John Quincy Adams katika kura za wananchi lakini Adams alishinda urais mwaka 1824, huo ukawa mshangao wa kwanza katika historia ya Marekani. Mwaka 1876, Rutherford Hayes alishindwa katika kura za wananchi na Samuel Tilden lakini akawa Rais. Mwaka 1888, Benjamin Harrison alishinda akiwa amezidiwa kura za wananchi na Grover Cleveland.

Ukifuatilia, wenye kubebwa na Kura za Majimbo mara zote ni wagombea wa Republican. Kasoro mwaka 1824 katika uchaguzi wa chama kimoja cha Democratic-Republican. Baada ya vyama hivyo kugawanyika na kupatikana Republican na Democrats, mara zote wanaobebwa ni Republican.

Mvurugano unakuja

Maandamano ya sasa kupinga ushindi wa Trump ni alama tu kuwa mtindo wa kumchagua Rais kupitia kura za watu wachache umepitwa na wakati. Huko mbele ya safari kuna mvurugano mkubwa unaweza kutokea.

Mapendekezo ya uwepo wa Kura za Majimbo ni ya Katiba ya mwaka 1787. Pengine mazingira ya watu wachache wanaoaminiwa kwa ajili ya kutunza uzalendo kwa nchi yao kipindi hicho yalikuwa na uaminifu kuliko sasa. Ndiyo maana ndani ya miaka 16 makosa yamekuwa mara mbili.

Matakwa ya Kura za Wajumbe yalikuwa na maana ya udhibiti, kwamba anaweza kutokea mgombea akawa anapendwa sana na wananchi lakini sera zake au nyendo zake zikawa hatari kwa maslahi ya nchi, kwa hiyo wajumbe wa Electoral College wanaweza kumdhibiti.

Hata hivyo, siyo kwa dunia ya sasa. Mtu anaweza kuutaka urais kisha akawekeza nguvu kubwa kwa wajumbe wa Electoral College. Wajumbe hao pia ni binadamu. Viongozi wengi Marekani wamekuwa wakikutwa na hatia za rushwa, hao wajumbe nao ni binadamu na wanaweza kushawishiwa.

Anayetaka urais akiwa tajiri kama alivyo Trump au Bush, anaweza kufadhili hata watu wanaowania ujumbe wa Electoral College ili wamfae mbele ya safari. Watu 538 ni wachache na wananunulika. Ndiyo maana wananchi wanamchagua huyu, wao wanampigia kura mwingine.

Sisemi kuwa rushwa ilitumika Marekani lakini natoa picha ya jinsi ambavyo hatari ya matumizi ya fedha kupora haki ya walio wengi ni kubwa mno kupitia Kura za Majimbo.

CHANZO: Maandishi Genius

kama mlitaka hillary ashinde kura nyingi za wajumbe, mngemuambia ashinde majimbo mengi zaidi. over
 
Back
Top Bottom