Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Nyie vjana wa cdm achen ujinga achen kijana mwenzenu agombee mbona ana uwezo?
 
Zito ni chaguo la CCM, hivyo ni bora kama tumekosa mtu wa kugombea kupitia chadema, badala ya kumpitisha Zito kabwe ni bora tuichague CCM yenyewe ambayo ndio inampigia DEBE.
Zito Kabwe ni mwanasiasa mnafiki sana na mbinafsi, na ndio maana hoja zake anataka zionekane ni za ZITO KABWE na sio za chama, sasa umaarufu wa mtu mmojammoja kwenye chama hauna tija.
 
zitto Kabwe bado anahitaji mda wa kutosha kujifunza siasa za kuongoza nchi.
 
kama ni uongo kamkamateni sasa au?
 
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.

Ningemteua DR. Wilbroad Slaa. kwa sababu
1.Amezoeleka sana huko vijijini kama mgombea wa urais Chadema ambako ndo wapiga kura wanajitokeza.
2.Busara zake kwa kiti cha urais zinafaa.
3.Amejaribu mara moja tumeona jinsi Chadema ilivyopata wafuasi wengi na # ya wabunge ilivyoongezeka.
4.Sasa hivi Zitto haaminiki tena kwa watu kama alivyokuwa zamani keshameza Ndoano.
 
mabadiliko ni muhimu yawepo ila c kwa staili hii!!
 
Waungwana tuangalie watu wa kulinganisha katika masuala ya siasa.Tusifanye ushabiki ucokuwa na mantiki.DCT SLAA nafikiri alinganishwe na LIPUMBA na JK.KABWE zito alinganishwe na KUGA MZIRAI na DOVUTWA
 

We mke wake wa kwanza mpaka ujue busara zake..,,,cz jukwaan kazi yake kuropoka na maneno meng kuliko maelezo..!josephine hawezi kuwa our first lady n he cnt b pres..!!
 
Mtoa mada ameiunderrate Tanzania, kati ya hao wawili hakuna anayefaa kuiongoza Nchi hii labda wakope CCM Mtu kama Magufuli au Sita na waanze mapema wasingoje watakao temwa 2015 vinginevyo CCM hiyoooooooooooo!
 
Je tunataka rais wa nchi hii awe na majukumu gani? Hapo ndipo tuseme kati ya hao watajwa nani atayamudu? Kukimbilia kuwalinganisha watu wakati hatujawa na mtazamo moja juu ya kile rais ataenda kuteleza si sawa.
 
Tabia zao binafsi ziwe kioo kwa jamii, chimbuko lao lisiwe na mashaka, Wawe na hofu ya Mungu, walie na waliao wafurahi na wanaofurahi mzigo na mateso ya jamii uwe ni mzigo wao, Watanzania wanapolala njaa wayahisi maumivu hayo kwa vitendo, wanapokosa huduma za msingi kwao iwanyime usingizi, Watanzana wanapoibiwa wawe kidedea kukamata wezi na kuwashughulikia bila huruma. Wapambanishwaji hao hawana sifa hizo.
 
Nisingependa zito kabwe agombee urais kw sababu
1.zito haaminiki tena siku hiz,tofaut na yule wa buzwag
2. Hajiamin,anapenda kujipendekez(hasa kwa mafisad)ana pupa na madaraka.
3.analewa sifa mf.ubunge sio saiz yng.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…