Makyomwango
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 322
- 80
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.
ningekuwa sijui ndo mnawaita mods ningempiga ban muanzisha uzi...mbona watu hamna adabu siku hizi?zitto anashindanishwa na lusinde..slaa na obama
kura yangu ni kwa zitto kabwe.kumpa kura slaa labda awe kalani wa mahakama maana siwezi chagua mtu anayefanya kazi kwa kusikiliza majungu na kwa sasa anaendesha chama kwa nguvu ya mchumba wake josephine mshumbuzi.kumchagua slaa ni sawa na kuipa laana nchi yangu maana huyu mzee kila kitu kachelewa mpaka mapenzi kayajulia uzeeni
dr.slaa ni mwadilifu, hatumiwi na watu wa ccm kama anavyofanya zito kabwe,leo bungeni karopoka kuwa mwandiko wa tundu lisu na mbaya sana.huyu hawezi kutunza siri hafai kuwa kiongozi wa taifa,bado ananuka maziwa.
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.
Hii nidharau kubwa.Huwezi kupambanisha Barcelona FC na Lipuli ya Iringa.
we endelea na propaganda zenu mumeishiwa na 2015 hiyoooo! Chadema ina majembe tupu ndo maana umeanza na hao wawili.tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya zitto zuberi kabwe ama wilbroad peter slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na kwa nini? Toa sababu kuu nne tu.
Haraka yote hii ni ya nini? Bado tuna miaka miwili mbele yetu ili kufika wakati muafaka wa kuzungumzia wagombea uongozi katika nafasi mbalimbali.
Hii kura ya maoni hapa haitusaidii chochote, sana sana itapalilia makundi ndani ya chama ambayo yanaweza kukivuruga chama na kuondosha mshikamano miongoni mwa wanachadema.
Kama ninavyoshauri kila mara, wanachadema tuachane na hizi sarakasi za uraisi kwa sasa. Tujielekeze katika kujenga na kuimarisha chama ngazi za chini-misingi, matawi na kata kwakuwa huko bado hakuko stable.
Rai yangu kwa wanachadema na wanaoiunga mkono chadema hapa JF naomba tuachane na mijadala isiyo na tija kwa maendeleo ya kisiasa na kidemokrasia. Tusipoteze muda kujadili mambo ya uraisi kwa sasa hakuna tija yoyote kwa mustakabali wa nchi yetu.