Kura Ya Maoni Na Hatima Ya Muungano

Kura Ya Maoni Na Hatima Ya Muungano

mkuu Mchambuzi, hats off kwa bandiko lako kama kawa.

ila mimi mwenzenu nasikitika sana kuona Watanzania wanaongelea referendum ambayo as far as am concerned haitakiwi hata kuwepo. kiukweli, referendum ikifanyika huku wapinzani na wanaharakati wakitizama tu, mi naona bora tu hata Gen Davis Mwamnyange na vijana wake wachukue nchi!

seriously.....
 
Mkuu Mchambuzi asante kwa bandiko zuri na lenye mchango mkubwa sana kwa kipindi hiki tunapoelekea kura ya maoni ya katiba hii yenye mazinagombwe na sintofaham nyingi kiasi cha kutuchanganya wananchi hasa tusio na ushabiki wa kivyama.

Ninamaombi mawili makuu kwaajili ya huu uzi

1. Mods wa JF, tunaomba huu uzi uwe juu kabisa (stick - kama sijakosea) nawaomba sana mods plz plz, huu uzi utatupatia elimu sana na michango mizuri itakayoepusha taifa letu na upotoshaji wa aina yoyote, tunahitaji kuelimishwa n kuvitumi vipaji vya great thinkers kujenga taifa letu

2. Wale wote wenye ushabiki wa hovyo wa kivyama, lugha za matusi, kejeli, dharau na mihemko isiyo na maana uzi huu nafikiri hauwahusu na wala sio mahali pake, mbaki kusoma michango ya maana. Hapa pia nawaomba tuwe makini kudhibiti nidhamu, maana kuna baadhi ya member wao kazi zao kuaharibu mijadala kwa kuingiza vitu vya hovyo, tulipe jukwaa hadhi yake.
 
Mchambuzi kama nilivyosema hapo hapo awali, mchakato mzima huu unaonekana ni wenye sintofaham nyingi na kuna vitu vingi sana vinavyoendelea nyuma ya carpet kama alivyojadili kwa kina Nguruvi3 kwenye nyuzi zake za duru za siasa kule great theankers,

tatizo kubwa ninaloliona ni watu wengi kuingiza ushabiki wa kivyama na kudhania katiba ikipita basi CCM ndio imeshinda au ndio inakua imewakomoa kundi fulani, wanasahau katiba ni document itakayoishi muda mrefu sana na ambayo makosa yake yatawagharimu kuanzia wao wenyewe mpaka vitukuu n wajukuu wao, hapo hapatakua na sijui CCM, UKAWA wala kundi lolote wote tutaumizwa au kunufaishwa na uamuzi wetu.

Kura ya maoni kwa maana nyingine ni determinant ya maisha yetu kwa kipindi kirefu sana cha maisha yetu n vizazi vyetu,so lazima tuinagalie kwa umakini maana uamuzi wowote mmbovu hakika tutaujutia, watanzania tatizo letu tumezoea kulishwa mawazo na watu wengine wenye maslahi binasfi bila kuangalia athari zake huko mbeleni. Na tunawaamini sana hao ambao mara zote ni walaghai na wadanganyifu, najiuliza why tunasahau.?

So upungufu na uimara wa hii isu ya katiba lazima ujadiliwe kwa kina sana sio kama baadhi ya watu wanaotaka "kufunika kombe mwanaharamu apite", au watu wanosema katiba ni nzuri siku tatu baada ya kukamilika uandishi wake ( najiuliza wameisoma saa ngapi na kuichambua ndani ya muda mfupi hivyo???, ohoooo ni magenious kuliko wa havard hawa, doc ya katiba wameichambua vipi ndani ya muda mfupi hivyo?,
sisi tujiongeze ili tufanye uamuzi sahihi na wenye manufaa kwa taifa letu na vizazi vyetu vijavyo
 
Bwana Mchambuzi umefanya uchambuzi mzuri sana. Lakini kumbuka kwamba jinsi ambavyo CCM wamejitoa fahamu ama niseme hawana soni tena, hata WANANCHI waelimishwe na waelewe kiasi gani ubovu wa katiba inayopendekezwa (kwa usahihi kabisa ILANI YA UCHAGUZI YA CCM) na wote wapige HAPANA katika kura ya maoni, bado CCM watakutangazia kuwa katiba inayopendekezwa imepata NDIYO asilimia 90 pande zote za muungano! kwa lugha wanayopenda sana "USHINDI WA KISHINDO! Tutafanya nini? Si tutabakia tunachambua kama unavyoona tunachambua uchakachuaji wa kuanzia kupitishwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba (iliyompa madaraka Rais kuwa ndiye ameshikilia mpini) hadi katiba inayopendekezwa!!! Hawa jamaa ni kama simba alijeruhiwa - wanajua mabadiliko yo yote yale ya kimfumo yatawapeleka kuzimu.

Mimi matumaini yangu yalikuwa kwa wajumbe wa CCM katika BMK kutoka Zanzibar kwamba ndiyo ilikuwa tumaini la mwisho la kutukomboa pande zote mbili - Tanganyika na Zanzibar katika kura ya kupitisha rasimu ya Jakaya, Sitta, na Chenge. Wangepatikana robo tu kuikataa hata uchakachuaji wa kura mbili usingewezekana. Sasa tukubali tu kuwa CCM ni washindi. Tufikirie mbinu nyingine ya kufufua katiba ya wananchi lakini sio kwa njia ya KURA YA MAONI inayosimamiwa na vyombo vya dola vya CCM. Ninawashangaa hata UKAWA kwamba watazunguka nchi nzima kuwaelimisha wananchi wapige kura ya HAPANA. Hiyo nguvu na hizo resources wangezielekeza hata sijui wapi (maana sina jibu)!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mchambuzi kama nilivyosema hapo hapo awali, mchakato mzima huu unaonekana ni wenye sintofaham nyingi na kuna vitu vingi sana vinavyoendelea nyuma ya carpet kama alivyojadili kwa kina Nguruvi3 kwenye nyuzi zake za duru za siasa kule great theankers,

tatizo kubwa ninaloliona ni watu wengi kuingiza ushabiki wa kivyama na kudhania katiba ikipita basi CCM ndio imeshinda au ndio inakua imewakomoa kundi fulani, wanasahau katiba ni document itakayoishi muda mrefu sana na ambayo makosa yake yatawagharimu kuanzia wao wenyewe mpaka vitukuu n wajukuu wao, hapo hapatakua na sijui CCM, UKAWA wala kundi lolote wote tutaumizwa au kunufaishwa na uamuzi wetu.

Kura ya maoni kwa maana nyingine ni determinant ya maisha yetu kwa kipindi kirefu sana cha maisha yetu n vizazi vyetu,so lazima tuinagalie kwa umakini maana uamuzi wowote mmbovu hakika tutaujutia, watanzania tatizo letu tumezoea kulishwa mawazo na watu wengine wenye maslahi binasfi bila kuangalia athari zake huko mbeleni. Na tunawaamini sana hao ambao mara zote ni walaghai na wadanganyifu, najiuliza why tunasahau.?

So upungufu na uimara wa hii isu ya katiba lazima ujadiliwe kwa kina sana sio kama baadhi ya watu wanaotaka "kufunika kombe mwanaharamu apite", au watu wanosema katiba ni nzuri siku tatu baada ya kukamilika uandishi wake ( najiuliza wameisoma saa ngapi na kuichambua ndani ya muda mfupi hivyo???, ohoooo ni magenious kuliko wa havard hawa, doc ya katiba wameichambua vipi ndani ya muda mfupi hivyo?,
sisi tujiongeze ili tufanye uamuzi sahihi na wenye manufaa kwa taifa letu na vizazi vyetu vijavyo
Mchambuzi kama nilivyosema hapo hapo awali, mchakato mzima huu unaonekana ni wenye sintofaham nyingi na kuna vitu vingi sana vinavyoendelea nyuma ya carpet kama alivyojadili kwa kina Nguruvi3 kwenye nyuzi zake za duru za siasa kule great theankers,

tatizo kubwa ninaloliona ni watu wengi kuingiza ushabiki wa kivyama na kudhania katiba ikipita basi CCM ndio imeshinda au ndio inakua imewakomoa kundi fulani, wanasahau katiba ni document itakayoishi muda mrefu sana na ambayo makosa yake yatawagharimu kuanzia wao wenyewe mpaka vitukuu n wajukuu wao, hapo hapatakua na sijui CCM, UKAWA wala kundi lolote wote tutaumizwa au kunufaishwa na uamuzi wetu.

Kura ya maoni kwa maana nyingine ni determinant ya maisha yetu kwa kipindi kirefu sana cha maisha yetu n vizazi vyetu,so lazima tuinagalie kwa umakini maana uamuzi wowote mmbovu hakika tutaujutia, watanzania tatizo letu tumezoea kulishwa mawazo na watu wengine wenye maslahi binasfi bila kuangalia athari zake huko mbeleni. Na tunawaamini sana hao ambao mara zote ni walaghai na wadanganyifu, najiuliza why tunasahau.?

So upungufu na uimara wa hii isu ya katiba lazima ujadiliwe kwa kina sana sio kama baadhi ya watu wanaotaka "kufunika kombe mwanaharamu apite", au watu wanosema katiba ni nzuri siku tatu baada ya kukamilika uandishi wake ( najiuliza wameisoma saa ngapi na kuichambua ndani ya muda mfupi hivyo???, ohoooo ni magenious kuliko wa havard hawa, doc ya katiba wameichambua vipi ndani ya muda mfupi hivyo?,
sisi tujiongeze ili tufanye uamuzi sahihi na wenye manufaa kwa taifa letu na vizazi vyetu vijavyo
Ndio maana ninapomsikia Rais anaongelea katiba kimzaha inanisikitisha sana.
Rais anafanya michezo ya ulaghai katika suala zito kama hili inatisha.

Kwa mfano, katika hotuba yake Dodoma wakati anakabidhiwa na Chenge rasimu, Rais amesema, suala la ardhi limepatiwa ufumbuzi. Akasema katiba isiyozungumzia ardhi ina matatizo. Hapa anamuongelea Warioba na tume yake.

Asichokijua Rais wetu ni kuwa tume ya Warioba imealiangalia suala la katiba kwa undani na mapana yake.
Tume iliamua kuwa kila nchi ibaki na ardhi kama suala lake na ipange matumizi yake.

Kwa mfano, Rais Kikwete anasema, gesi na mafuta yameondolewa katika mambo ya muungano.
Halafu suala la ardhi ni la muungano.

Swali linakuja, hivi mafuta na gesi yanayopatikana ardhini unawezaje kuyatenga na matumizi ya ardhi?
Nina maana utalindiaje ardhi ikiwa znz imepata mwekezaji wa mafuta na gesi wakati JMT ndio mmiliki wa ardhi.

Pamoja na hayo, znz walikataa ardhi lisiwe suala la muungano.
Wanasheria zao zilizotungwa mahususi kumdhibiti Mtanganyika.

Wakati huo huo wao wana uhuru wa kuja na kufanya watakacho bila kuhojiwa kwasababu ardhi ya Tanganyika ni ya muungano. Kuna matatizo mengi yatakayojitokeza katika suala hili.

Mfano,
Kwavile kuna sintofahamu, matumizi ya ardhi ya znz yatakuwa ya'' muungano''.
Wakati huo huo znz inasheria zake zinazohusu mambo ya ardhi. Sheria mbili zinawezaje kuoanishwa kwa katiba mbili tofauti. Na je, znz wapo tayari kufuta katiba ya 2010 ili kuleta uwiano na rasimu iliyoandikwa na Chenge/Sitta mafichoni?

Kutafika wakati wznz watakuwa na wakati mgumu sana Tanganyika.
Suala la ardhi halina majibu ya kueleweka na hivyo wznz wataonekana kama wavamizi.
Inaweza kutotokea leo lakini vizazi vijavyo vitahoji kwavile hakuna maelezo ya kuridhisha kwanini imekuwa hivyo.

Kitakachofuata ni yale ya Humvzi wa Zimbabwe kuvamia mashamba ya masetla wa kizungu.
Hapa kwetu itakuwa uvamizi dhidi ya rasilimali za wnz waishio Tanganyika.

Hali itakuwa tofauti na wawekezaji wa nje kwasababu wao wana mkataba, kwa mfano, miaka 99.
Wanalindwa na sheria tofauti na ambavyo wznz watakuwa wanalindwa na ''logic'' zisizo wazi.

Hivyo Rais amelingalia suala la ardhi katika kiwango cha mtu mmoja mmoja na si tatizo la mataifa mawili, Tanganyika na Zanzibar. Hapa waliopo katika wakati mbaya ni wznz kwani muda utakapotimia watajikuta wenyewe.
Walinzi wao ambao leo wanawaambia mambo shwari ukweli ni kuwategea bomu.

Katika suala hilo hilo, haijaelezwa ushiriki wa znz katika jumuiya kama EAC na SADC.

Endapo znz watakwenda kama nchi, hilo litaweka masilahi ya Tanganyika katika utata.
Kwa mfano, kama znz itakuwa mshiriki wa EAC basi maamuzi yanayohusu ardhi yatakuwa ya znz.
Lakini suala la ardhi ni la muungano. Hapa unawezaje kuwa na sera moja ya ardhi ukiwa na ushiriki tofauti?

Washirika wengine nao watahoji, kama znz inaweza kupata uhuru wa ardhi ya Tanganyika kwanini Kenya, Uganda, Rwanda n.k. wasipewe fursa ile ile.

Utetezi kuwa katiba ya JMT inawalinda wznz hauna mashiko, znz inasheria zake na ushiriki kama nchi tofauti?
Wakati huo itakuwa kama Burundi au Kenya kwa hadhi mbele ya EAC

Kwa mtazamo huo, rais anaongelea mambo magumu kwa njia rahisi sana na hilo ni tatizo kubwa mbele ya Safari.

Tofauti na tume ya Warioba iliyoliangalia suala hilo kwa upana wake, Kikwete na Chenge wameliangalia kwa kutafuta dawa ya kupunguza maumivu na si kutibu ugomjwa husika.

Masuala kama haya yanawagusa wananchi kila mmoja alipo, kwabahati mbaya halionekani kama tatizo bali nderemo na vifijo tu vya kwaya za Komba, mbili zinatosha, tatu gharama n.k. bila justification au utambuzi na uchanganuzi makini.
Mtanganyika hii funika kombe ya Kikwete italeta tabu kweli kweli. Hatujifunzi kutokana na yaliyopita.
Kwa mfano, suala la S3 lilimuondoa Jumbe madarakani. Likarudi wakati wa G55 na tume za Nyalali, Kisanga n.k. kama alivyojadili Mchambuzi kwa kina. Bado tunaendelea kufunika kombe kwa kauli ya muda bado.

Muda wa tunda kuliwa ni wakati limeiva baada ya hapo linageuka kuwa uozo. JK anashauri watu wasbiri uozo.
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA NNE
Swali la msingi linalofuata ni je:
· Iwapo huu ndio umekuwa msimamo wa serikali kwa kipindi kirefu, ni kitu gani kilibadilisha msimamo huu mwaka 2011, mwaka mmoja tu baada ya uchaguzi ambapo suala la katiba mpya halikuwa sehemu ya ilani ya uchaguzi?

Kwa mtazamo, upo uwezekano tena mkubwa kilichosukuma serikali ya CCM kuanzisha mchakato wa katiba mpya ni mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yaliTOtambua Zanzibar kama nchi.
Kitendo cha Zanzibar kujitambua "nchi" kwa mujibu wa katiba yake (2010) kingepelekea umma (hasa wa Tanganyika) kuhoji juu ya ‘sovereignity status' ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar (2010).
Kwa maana, CCM mchakato wa katiba ulitokana na matukio ya Zanzibar, na sio mahitaji ya wananchi, hasa watanganyika kama wananchi wengi wa Tanganyika wanavyoendelea kuaminishwa kwenye kampeni zilizoanza za kuhamasisha upigaji wa kura ya ndio kwa rasimu iliyopendekezwa katika kura ya maoni. Iwapo hatupo sahihi katika hili, basi wacha historia ije kutuhukumu.

CCM wamekabidhiana rasimu wakitambua haina uungwaji mkono. Ndio maana wanaacha kunadi kwa wananchi moyo wa rasimu (muundo wa shirikisho la serikali tatu), na badala yake wananadi viungo kama vile vidole, magoti, makalio, n.k, viungo ambavyo bila ya moyo, ni viungo ambavyo havina kazi. wanaotambua kwamba walipobaki wenyewe hakukuwa na cha maana zaidi ya uhuni wa kura ambao hauhitaji akili kubaini. Katiba yao haikubaliki kwa wananchi na ni suala la muda tu kukataliwa hata kama watalazimisha iwe kama wanavyotaka.

Mkakati wa CCM ni kuwasahaulisha wananchi na kuwaaminisha mchakato umekamilika. Wanaaminisha wananchi ili wasahau uhuni uliofanyika kuanzia mwanzo hadi mwisho .
Jitihada za CCM ni kuona wananchi wanajadili rasimu yao ya mafichoni kwa lengo la kuwasahaulisha kwamba mtiririko wake umejaa dhambi, uchafu na najisi kwa demokrasia.

Kama tulivyokwisha jadili, Rasimu ya CCM imeonekana kujibu hoja za wazanzibari badala ya matakwa ya watanzania kikatiba. Na katika kuficha ukweli, CCM wametumia mwanya wa kusema zipo haki za akina mama, watoto, wafugaji, vijana, wasanii n.k kama mkakati wa kutumia makundi haya kupitisha katiba haramu inayopendekezwa. Huku ni kuendelea kuwalaghai wananchi ili kuficha makosa, dhambi na uhuni uliotendeka dhidi ya taifa. Isitoshe, ni kusema kwamba kwa miaka 50, CCM haikujali haki za wananchi, lakini sasa imeona haja ya kuanza kujali haki hizo:
Je hivyo ndivyo CCM inataka kuambia wananchi?

Lengo kubwa la CCM ni kuondoa umma katika mjadala halisi, mjadala muhimu kwa maisha yao ya sasa na baadae,badala yake kuwatupia viungo vya katiba ili waridhike. CCM wanafahamu katiba yao imekosa ‘moyo' na ndio sababu hawakujadili muundo wa muungano katika vifungu husika.

Ni aidha:

  1. Walikwepa ukweli kuhusu muungano.
  2. Hawakuwa na majibu ya kero za muungano.
  3. Walikwepa ili waendelee na ulaghai wa miaka 50 iliyopita, na waendeleze ulaghai kwa miaka mingine ijayo.
Mkuu Mchambuzi, kwanini Serikali ya CCM iliamini muundo wanaoupenekeza ni kutokana na kukosa umakini ndani ya chama na viongozi.Siku za nyuma CCM ilisoma nyakati na kujadili kwa kuangalia ukweli. Ndio msingi wa whitepaper na matokeo tofauti.
Wakati ulitimia na CCM walijua vyama vingi haviepukiki.

Rais Kikwete alidhani angeweza kutawala kwa kuwaridhisha wznz. Akakubali mabadiliko ya katiba ya znz 2010 iliyokinzana na JMT. Wazanzibar walioshiriki uhuni huo wa 2010 kwa maana ya znz huru, ndio hao hao wamerudikuungana na Chenge rasimu ya mafichoni(Nahodha, Kificho, Aboud, Asha, Seif khatibu n.k.)

Tatizo la JK kukubali 2010 znz, lilizaa maswali ndani ya JMT.
Kwavile wapinzani walishikia bango katiba mpya, kwa malengo tofauti kabisa wasi wasi ulimkumba Kikwete, agebda inaweza kuunganishwa na katiba ya znz 2010.

Hivyo kuanzisha mchakato ili kuwa njia ya kuteka hoja ya wapinzani na kudhibiti muungano kama ilivyotokea mswada wa kwanza ie. kujadili muungano ilikuwa haramu, na ilivyofanyika sasa.

Katiba ya znz 2010 ndio iliwapa nguvu ya kuchochea Utanganyika. Hiyo ilikuwa point of no return kwa Kikwete.
Hisia na uchungu wa Tanganyika ulikuwepo miaka mingi, kumbuka G55 na tume nyingine. Lakini haja ya mabadiliko ilikuwepo ,Tanganyika ni suala linalozizima wala si suala jipya.

CCM wanatambua wanachokifanya ni haramu. Kazi kubwa ni kuaminisha umma kila kitu ni maua mazuri,twende mbele.
Hoja inayosemwa ni kura ya maoni. Katiba yao ya mafichoni ya Chenge na tume ya kukusanya maoni ya Sitta hazijajibu agenda kubwa za taifa kabla ya mchakato.

  1. Je, mfumo wa utawala wa nchi kwa miaka 50 unahitaji mabadiliko kulingana na mabadiliko ya kijamii? Hapa ikiwemo hoja ya mfumo wa kisiasa wa vyama vingi, kubadilika kwa thamani za kitaifa kama kufa kwa ujamaa n.k.
  2. Je, matatizo yaliyopo ya muundo wa muungano yamepatiwa ufumbuzi?
  3. Nini dira na mwelekeo wa taifa wa siku zijazo

Hoja hizi hazijibiki bila kugusa masilahi ya CCM. Ndio maana wamezikwepa wakisema. Kilichofanyika ni kujadili hoja za wazanzibar kwa kuandika katiba si ya Wananchi wa Tanzania bali kujibu hoja za wznz.

Kwaile maswali 3 hapo juu haya kuwa na majibu,CCM wameshindwa kujibu hoja za Wazanzibar. Kwa mfano, wznz wakisema mambo ya muungano yapunguzwe, CCM imeyaongeza. Mkataba wa muungano ulikuwa na mambo 11, tume ya Warioba 7 na Rasimu ya Chenge/Sitta ya mafichoni ina 16. Bado hoja za wznz hazijajibika pamoja na jitihada zao.

Pili,hoja za wznz ni kuwa huru kiuchumi na kiutawala. Kuwashirikisha katika JMT ni kuwaondolea yale wanayoyadai kwasababu watawajibika kwa JMT zaidi kuliko SMZ.

Mwaka 1984 Jumbe aliondolewa madarakani kwasababu ya kuwa makamu wa Rais. Kilichomuondoa si hoja ya Tanganyika, ni hoja ya Umakamu wa JMT akiwa na agenda ya waznz ba nakamu wa Rais(collective responsibility).
Hilo likatumika kama rungu.

Kwasasa rais wa znz anachaguliwa na wznz kwa kupendekezwa na CCM. Udhibiti wake ni mgumu kidogo ukilinganisha na wakati atakapokuwa makamu wa Rais JMT. Swali je, hiyo ndiyo znz huru wanayoitaka?

Kuhusu suala la kuaminisha watu kura ya maoni, hizo ni jitihada za kuwasahulisha wananchi dhambi kuu iliyotendwa kuanzia mchakato hadi mwisho.

Dhambi ya kutokuwa na maridhiano, upuuzi wa kuiba kura na kubadili sheria si kwa manufaa ya taifa bali Chnege/Sitta
Hya ni mambo Watanzania wanatakiwa kuyaangalia na kusahau kura ya maoni.

Kura ya maoni ni kuhalalisha uovu uliotendwa, kwamba unakubali dhambi iliyotendwa kwa kutupiwa kitanzi.
Lakini muhimu zaidi ni kwa Watanganyika kujiuliza;

Haja na kiu ya kutaka katiba mpya, Je, imekidhi matamanio yao?
Tumeona katiba ya Chenge/Sitta ilivyodharau hoja zao kwa kina na ukamilifu.
Je, waendelee tu au ni wakati wa kusema enough is enough!
 
Katika hali halisi na ukweli usiopingika ni kuwa katiba pendekezi aliyokabidhiwa Jakaya Kikwete na Dr Shein, pale uwanja wa Jamhuri Dodoma, ile ni katiba ya watawala wa CCM.

Kiuhalisia pia ni kuwa hata wanachama na mashabiki wa kawaida wa CCM, ile katiba ya Sitta/Chenge, wao pia haiwafai hata kidogo.

Katiba pekee ya wananchi wa nchi hii ni ile Rasimu ya pili ya Tume ya Warioba, ambayo ndiyo iliyobeba maoni ya wananchi.

Kwa maana hiyo katiba hii ya akina Sitta/ Chenge na wapambe wao kwenye bunge maalum la katiba, haipaswi tu kupigiwa kura za HAPANA na wanachama wanaounda ukawa, bali hata kwa wanaccm wa kawaida, wanaoitakia mema nchi yetu.

Waraka huu muhimu wa Mchambuzi, ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu.
 
Na ndiyo maana JK alipokuwa anaipokea katiba hiyo pendekezi, alifichua siri kwa kueleza kuwa wakati anatoa wazo hilo la uundwaji wa katiba mpya kwenye vikao vya juu vya chama chake, wahafidhina wa chama chake walimweka 'kitimoto' na kumuuliza hilo wazo la uundwaji wa katiba mpya, ameliibua toka wapi?

Kwa kuwa maccm wenziwe walimweleza bayana kuwa 'idea' ya uundwaji wa wa katiba mpya siyo ya CCM.

Kwa hiyo haishangazi hata kidogo kwa akina Sitta/ Chenge kumjabidhi JK pale uwanja wa Jamhuri Dodoma, kumpa 'waraka' wa CCM badala ya katiba ya nchi!
 
Kwahakika huu ni baadhi ya uzi wa maana niliowahi kuuona hapa jf. Ni nadra sana kuuona wanasiasa na vibaraka wao kutia neno hapa maana uwezo wao uko chini. Nirudi kwenye mada, uzoefu wangu kwenye nchi nyingi za kiafrika katiba huwa inatekelezwa kwa utashi wa viongozi walio madaraka na wala sio katiba inasema nini. Nadhani mtakubaliana na mimi kwamba katiba yetu ya mwaka 77 imewekwa viraka vingi mpaka hivi leo kukidhi utashi wa watawala. Labda nitoe mfano rahisi kabisa, angalia kanuni za BMK zilivyobadilishwa kila mara hadi akidi ya utata kupatikana. Sasa tabia ile ya wazi tuliyoiona ndio itakavyokuwa kwa mtawala yoyote atakayeingia madarakani atafanya atakavyo kukidhi mahitaji yake na ya wakati huo. Hivi mmesahau huu msemo maarufu hii katiba/rasimu sio msahafu/biblia? Watawala wa kiafrika hawana tabia ya kuheshimu katiba. Kwahiyo msishangae watawala wanaacha matakwa ya wananchi wanaweka yao na jeshi linatumika kama kinga ya uovu huo. Sisi waafrika bado sana kwenye kuheshimu sheria tunazojiwekea. Usishangae wasomi na wasiosoma huku africa kufanana kwa tabia, uwezo wa kufikiri na kutenda.
 
Wafanye watakavo fanya lakini msimamo wa wazanzibari unajulikana. Mutaiba mpaka lini?. Machafuko yakitokea hatutaumia wazanzibari peke yetu. Hata bara na wao wamo. Ikiwa CCM hawajatia akili, wajue kilichobakia ni kitu kidogo tu, taifa hili litaripuka.
 
Hivi itakuwaje, kwa mfano, Tanzania Bara wakipiga kura ya Ndiyo na Zanzibar kura ya Hapana?

Nauliza tuu in theory maana sidhani kama hili linaweza kutokea in practice anyway.

Huwa nawashangaa sana wale wanaodai kuwa wanaisubiri katiba inayopendekezwa kitaani wapigie kura ya Hapana.

Hata kama wengi wakipiga kura ya Hapana lazima kura za Ndiyo zitoshelezwe kwa namna yoyote ile.

Huo ndiyo ukweli wenyewe ambao wengi hawataki kuuamini. Lazima watu wakubali kuvuna walichopanda.

Mh... huu ndio ukweli mtupu tena bila chenga! Watanzania HAWAITAKUBALI hii katiba lakini kura za NDIO ZITASHINDA! Hapo ndipo panapotakiwa kushuhulikiwa kwa sasa!
 
Mkuu Mchambuzi, kwanini Serikali ya CCM iliamini muundo wanaoupenekeza ni kutokana na kukosa umakini ndani ya chama na viongozi.Siku za nyuma CCM ilisoma nyakati na kujadili kwa kuangalia ukweli. Ndio msingi wa whitepaper na matokeo tofauti.
Wakati ulitimia na CCM walijua vyama vingi haviepukiki.

Rais Kikwete alidhani angeweza kutawala kwa kuwaridhisha wznz. Akakubali mabadiliko ya katiba ya znz 2010 iliyokinzana na JMT. Wazanzibar walioshiriki uhuni huo wa 2010 kwa maana ya znz huru, ndio hao hao wamerudikuungana na Chenge rasimu ya mafichoni(Nahodha, Kificho, Aboud, Asha, Seif khatibu n.k.)

Tatizo la JK kukubali 2010 znz, lilizaa maswali ndani ya JMT.
Kwavile wapinzani walishikia bango katiba mpya, kwa malengo tofauti kabisa wasi wasi ulimkumba Kikwete, agebda inaweza kuunganishwa na katiba ya znz 2010.

Hivyo kuanzisha mchakato ili kuwa njia ya kuteka hoja ya wapinzani na kudhibiti muungano kama ilivyotokea mswada wa kwanza ie. kujadili muungano ilikuwa haramu, na ilivyofanyika sasa.

Katiba ya znz 2010 ndio iliwapa nguvu ya kuchochea Utanganyika. Hiyo ilikuwa point of no return kwa Kikwete.
Hisia na uchungu wa Tanganyika ulikuwepo miaka mingi, kumbuka G55 na tume nyingine. Lakini haja ya mabadiliko ilikuwepo ,Tanganyika ni suala linalozizima wala si suala jipya.

That bold text refer to your ignorance of strategic thinking of patriotic Zanzibaris, ironically you have noted the impact Zanzibaris have on the return of Tanganyika. Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi.

Nadhani ingekuwa bora zaidi ungeongeza kiduchu bandiko na kuandika "Kura ya Maoni na hatima ya Tanganyika"

Muungano na Tanganyika ni kipi bora kwenu muungano unaweza kuwepo na Tanganyika ikapotea kama ilivyo sasa.

Katiba inaelekea kupatika na hakuna dalili zozote za Tanganyika kupatikani.
 
Ritz,

Naona mantiki ya hoja yako, lakini nilichagua kujadili hatima ya muungano badala ya hatima ya Tanganyika kwa sababu hoja ya msingi ni muundo wa muungano, kwa kufananisha muundo ndani ya rasimu ya tume na ule ndani ya rasimu ya Chenge. Ni baada ya kujadili uwepo wake (muungano) na muundo wake Ndio suala la washirika wa muungano linapojitokeza. Kwa maana nyingine Rahisi zaidi - Kama nia yetu ni kuelimisha umma juu ya kwanini wana haja ya kuikataa rasimu ya Chenge ni kwa kujadili kwanza suala juu ya uwepo wa muungano na muundo wa muungano ili kubaini iwapo masuala haya mawili yana ridhaa ya wananchi wa pande zote Mbili za muungano. Tofauti na kufanya hivyo, tutajikuta tukijadili kitu ambacho hakina maana sana kwa wananchi Wakati wa maandalizi ya kwenda kwenye kura ya maoni.

Kwa Mujibu wa rasimu ya Chenge (ukurasa wa ‘108’), kura ya maoni inakadiliwa Kama ifuatavyo:

---
Mambo ambayo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa mkono kwa zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa ma wananchi wa Tanzania Bara, na zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa na wananchi wa Tanzania Zanzibar katika kura ya maoni”:

•Muundo wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
•Kuwepo kwa Jamhuri ya muungano.
•Kubadilisha masharti ya ibara ya 129(1) (c) ya katiba hii.

----

Kwa maana hii, Chenge na wenzake tayari wameshawaamulia wananchi:

1. Uwepo wa muungano kwa lazima na sio kwa ridhaa ya wananchi.
2. Pili, wameshaamua Aina au Mfumo wa muungano ambao wao Kama watawala wanaona Ndio utakaowafaa wananchi.

Haya yakisha kaa vyema vichwani mwa wananchi, inakuwa Rahisi kwa wao - wananchi kuelewa kwa urahisi kwanini kupigia kura ya ndiyo rasimu ya Chenge maana yake ni wananchi kwa Mara ya kwanza tangia uhuru na muungano, kuhalalisha kwa Mujibu wa Sheria, uchakachuaji wa masuala yafuatayo juu ya Tanganyika:

1. Historia ya Tanganyika ndani ya muungano.
2. Hadhi ya Tanganyika ndani ya muungano.
3. Utambulisho wa Tanganyika ndani ya muungano.
4. Mamlaka ya Tanganyika ndani ya muungano.

Wananchi wakipiga kura ya ndiyo kuhalalisha haya, kazi ya CCM kuchakachua Muungano na Tanganyika itakuwa imehalalishwa kwa Mujibu wa Sheria, tofauti na sasa ambapo CCM bado Ina Wakati Mgumu wa Kujibu maswali mbalimbali juu ya uchakachuaji uliofanyika.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
RASIMU YA CHENGE ITABOMOA NCHI.

Samuel Sitta, Chenge, asha migiro na wenzao wametupilia Mbali rasimu ya tume ya jaji warioba ambayo iliweka misingi ya kutatua kero za muungano kwa pande zote Mbili za muungano, hasa kuzinduliwa kwa Tanganyika na mshirika Huyu kupewa hadhi na utambulisho wa kikatiba.

Rasimu ya mafichoni ya akina Sitta, Chenge, migiro na wenzao imeshindwa kutengua kitendawili cha Zanzibar kuwa ni nchi au ni sehemu ya jamhuri ya muungano. Dr shein Anasema Zanzibar ni sehemu ya muungano huku Katika aliyoapa kuilinda Ikisema Kwamba Zanzibar ni nchi. Shein anayasema haya akiwa kwenye ziara nje ya nchi ya Zanzibar, yani Tanganyika, lakini akirudi nchini kwake Zanzibar, Anasema Kwamba Zanzibar ni nchi.

Rasimu ya Chenge imeongeza mgogoro wa kikatiba Kati ya Zanzibar, Tanganyika na jamhuri ya muungano wa Tanzania; kwa mfano, rais wa Zanzibar kwa Mujibu wa katiba ya Chenge anafanywa kuwa makamu wa rais wa JMT, Huyu ataapa Zanzibar kutii katiba ambayo inajitambua kuwa nchi kamili ndani ya JMT.

Baadae atakula kiapo cha utii kwa katiba ya JMT inayoitambua Zanzibar Kama sehemu ya JMT (sio Kama nchi). Kwa njia hii hapatokuwa na katiba, badala yake kutakuwa na uvunjaji wa katiba. Kwa kulazimisha katiba ya namna hii kupelekwa kwa wananchi, na kwa wananchi kupigia kura ya Ndio katiba hii, maana yake ni kubomoa muungano na taifa kwa ujumla.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mchambuzi na wewe sio makini kiasi hicho kura ya maoni inahitaji simple majority.50% + 1 ambayo inapatikana kirahisi... Na hii ni duniani kote.

You are right, a Valid outcome requires 50.01% (simple majority), lakini when it comes to Irreversible decisions, two thirds (super majority) approach hutumika;

Suala letu juu ya Mfumo wa muungano suala muhimu, ni suala ambalo wananchi wanashirikishwa kwa Mara ya kwanza tangia uhuru wa Tanganyika, tangia mapinduzi ya zanzibar, na tangia muungano, baada ya muundo wa kulazimishwa na watawala kwa miaka zaidi ya 50; hakuna Shaka Kwamba kura ya Ndio maana yake ni Kwamba CCM sasa itapata uhalali wa kuchakachua historia ya muungano na historia ya Tanganyika kwa Mujibu wa Sheria; kwa maana nyingine Rahisi and by implication, maamuzi haya yatakuwa "irreversible"; duniani kote, any irreversible decisions require super majority;

Suala la Mfumo wa muungano kwetu, hili ni suala ambalo maamuzi yake yataishi kwa muda mrefu sana, so hatuna haja ya kuamua muundo wa muungano kwa simple majority na kuishi kwa taifa lililo gawanyika kwa miaka mingine 50; kwa maana nyingine Rahisi, ipo siku the 49.99% will become the 50.01%, very easily;

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
RASIMU YA CHENGE ITABOMOA NCHI.

Samuel Sitta, Chenge, asha migiro na wenzao wametupilia Mbali rasimu ya tume ya jaji warioba ambayo iliweka misingi ya kutatua kero za muungano kwa pande zote Mbili za muungano, hasa kuzinduliwa kwa Tanganyika na mshirika Huyu kupewa hadhi na utambulisho wa kikatiba.

Rasimu ya mafichoni ya akina Sitta, Chenge, migiro na wenzao imeshindwa kutengua kitendawili cha Zanzibar kuwa ni nchi au ni sehemu ya jamhuri ya muungano. Dr shein Anasema Zanzibar ni sehemu ya muungano huku Katika aliyoapa kuilinda Ikisema Kwamba Zanzibar ni nchi. Shein anayasema haya akiwa kwenye ziara nje ya nchi ya Zanzibar, yani Tanganyika, lakini akirudi nchini kwake Zanzibar, Anasema Kwamba Zanzibar ni nchi.

Rasimu ya Chenge imeongeza mgogoro wa kikatiba Kati ya Zanzibar, Tanganyika na jamhuri ya muungano wa Tanzania; kwa mfano, rais wa Zanzibar kwa Mujibu wa katiba ya Chenge anafanywa kuwa makamu wa rais wa JMT, Huyu ataapa Zanzibar kutii katiba ambayo inajitambua kuwa nchi kamili ndani ya JMT.

Baadae atakula kiapo cha utii kwa katiba ya JMT inayoitambua Zanzibar Kama sehemu ya JMT (sio Kama nchi). Kwa njia hii hapatokuwa na katiba, badala yake kutakuwa na uvunjaji wa katiba. Kwa kulazimisha katiba ya namna hii kupelekwa kwa wananchi, na kwa wananchi kupigia kura ya Ndio katiba hii, maana yake ni kubomoa muungano na taifa kwa ujumla.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
RASIMU YA CHENGE ITABOMOA NCHI.

Samuel Sitta, Chenge, asha migiro na wenzao wametupilia Mbali rasimu ya tume ya jaji warioba ambayo iliweka misingi ya kutatua kero za muungano kwa pande zote Mbili za muungano, hasa kuzinduliwa kwa Tanganyika na mshirika Huyu kupewa hadhi na utambulisho wa kikatiba.

Rasimu ya mafichoni ya akina Sitta, Chenge, migiro na wenzao imeshindwa kutengua kitendawili cha Zanzibar kuwa ni nchi au ni sehemu ya jamhuri ya muungano. Dr shein Anasema Zanzibar ni sehemu ya muungano huku Katika aliyoapa kuilinda Ikisema Kwamba Zanzibar ni nchi. Shein anayasema haya akiwa kwenye ziara nje ya nchi ya Zanzibar, yani Tanganyika, lakini akirudi nchini kwake Zanzibar, Anasema Kwamba Zanzibar ni nchi.

Rasimu ya Chenge imeongeza mgogoro wa kikatiba Kati ya Zanzibar, Tanganyika na jamhuri ya muungano wa Tanzania; kwa mfano, rais wa Zanzibar kwa Mujibu wa katiba ya Chenge anafanywa kuwa makamu wa rais wa JMT, Huyu ataapa Zanzibar kutii katiba ambayo inajitambua kuwa nchi kamili ndani ya JMT.

Baadae atakula kiapo cha utii kwa katiba ya JMT inayoitambua Zanzibar Kama sehemu ya JMT (sio Kama nchi). Kwa njia hii hapatokuwa na katiba, badala yake kutakuwa na uvunjaji wa katiba. Kwa kulazimisha katiba ya namna hii kupelekwa kwa wananchi, na kwa wananchi kupigia kura ya Ndio katiba hii, maana yake ni kubomoa muungano na taifa kwa u
Hata wanaounga mkono katiba ya Chenge na Sitta wanajiuliza maswali mengi sana, ndio maana hatupati majibu
1. Je katiba ya change/sitta imetokana na maoni ya nani kwa ridhaa ipi na sheria gani iliyoipa mamlaka. Ya Warioba kwa mujibu wa kada wa CCM ambaye ni mjumbe wa vikao vizito vya CCM MwanaDiwani wamewaachia UKAWA

2. Katiba ya Chenge/Sitta imetatua tatizo la mfumo wa utawala, wau imekimbilia kuondoa vipengele vya maadilli ili kutowabana wahalifu ikiwemo waliyoiandika.

3. Katiba ya Chenge/Sitta imetatua tatizo la muundo wa muungano kwa miaka 50 au imeziba na kitambaa na donda linanuka?

Ukisoma zaidi utaona, marais 4 kutoka znz wana uwezo wa kuitawala Tanganyika bila kupigiwa kura na Mtanganyika yoyote. Hilo nalo sijui kama halitaleta mgogoro maana makamu wa Rais tu kwasasa ni mfungua makongamano, sijui mbeleni.

Hili ni bomu linalotegwa na JK na siku za karibuni litalipuka, muungano pwaa!
 
RASIMU YA CHENGE ITABOMOA NCHI.

Samuel Sitta, Chenge, asha migiro na wenzao wametupilia Mbali rasimu ya tume ya jaji warioba ambayo iliweka misingi ya kutatua kero za muungano kwa pande zote Mbili za muungano, hasa kuzinduliwa kwa Tanganyika na mshirika Huyu kupewa hadhi na utambulisho wa kikatiba.

Rasimu ya mafichoni ya akina Sitta, Chenge, migiro na wenzao imeshindwa kutengua kitendawili cha Zanzibar kuwa ni nchi au ni sehemu ya jamhuri ya muungano. Dr shein Anasema Zanzibar ni sehemu ya muungano huku Katika aliyoapa kuilinda Ikisema Kwamba Zanzibar ni nchi. Shein anayasema haya akiwa kwenye ziara nje ya nchi ya Zanzibar, yani Tanganyika, lakini akirudi nchini kwake Zanzibar, Anasema Kwamba Zanzibar ni nchi.

Rasimu ya Chenge imeongeza mgogoro wa kikatiba Kati ya Zanzibar, Tanganyika na jamhuri ya muungano wa Tanzania; kwa mfano, rais wa Zanzibar kwa Mujibu wa katiba ya Chenge anafanywa kuwa makamu wa rais wa JMT, Huyu ataapa Zanzibar kutii katiba ambayo inajitambua kuwa nchi kamili ndani ya JMT.

Baadae atakula kiapo cha utii kwa katiba ya JMT inayoitambua Zanzibar Kama sehemu ya JMT (sio Kama nchi). Kwa njia hii hapatokuwa na katiba, badala yake kutakuwa na uvunjaji wa katiba. Kwa kulazimisha katiba ya namna hii kupelekwa kwa wananchi, na kwa wananchi kupigia kura ya Ndio katiba hii, maana yake ni kubomoa muungano na taifa kwa ujumla.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mkuu Mchambuzi na Nguruvi,
hii ni moja ya katiba yenye mafumbo, mazingaombwe na sontofaham za kutosha sana ambazo hata majibu yake tunarashiwa rashiwa na kudanganywa na watetezi wa rasimu hii, kwa hakika ni kama visa vya Alfu lela ulela au kusadikika.

Kwa nini nasema hivyo? Watetezi sasa wa katiba hiyo penedekezwa ya CCM sasa badala ya hoja za kutetea legitimacy ya katiba hii wameanza vitisho sasa, viongozi wao mfano Wasira ambao Lukuvi alimnasibu kama jembe lao anasema wana CCM wanaopinga katiba yao basi warudishe kadi ya chama, hii inadhihirisha na kuthibitisha yale ambayo akina Nguruvi3 na Mchambuzi mnayapigia kelele kwamba hii ni katiba ya mafichoni ya CCM kama alivyothibitisha Wasira mwenyewe " katiba yao".

Tulichotarajia sasa sio mbwembwe za mafuriko ya ushindi kura ya maoni au udanganyifu mwingine wowote zaidi ya kuelimishwa ni kwa namna gani katiba hii pendekezwa imetatua kero za muungano na mambo mengine ya msingi. Sio kupiga propoganda za kusema rasimu hii imataja makundi yote, wnanawake, vijana na kadhalika, kana kwamba ni katiba ya makundi sio ya nchi.

Pls wapiga debe wa katiba hii pendekezw tunaomba ufafanuzi kwa mambo muhimu sio kuja na cheap propoganda and lies za makundi kwenye katiba, tunataka katiba ambayo leo mtu akiwa mkulima,mvuvi muwindaji katiba itamsaida sio bora katiba kwa wachache au. Kundi fulani
 
Back
Top Bottom