Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,383
Wadau,
Kama tulivyomsikiliza Rais Kikwete Kuwa kura ya maoni itafanyika April mwakani na jinsi ninavyoona hilo lazima walitekeleze ukizingatia mizengwe iliyotawala wakati wa kupitisha hiyo rasimu.
CCM wanajua fika Kuwa Rais ajae anaweza asilipe kipaumbele hilo suala la kura ya maoni na pengine mchakato wote kuanza upya kwa hiyo watafanya lolote wawezalo ili kuipitisha katiba kabla JK hajaondoka madarakani.
Kwa maoni yangu Jambo hilo japo linapingwa na watu mbalimbali wakiwemo hata wana CCM wenyewe,lakini kundi la akina Sita hawataki kukubali Kuwa walivurunda hivyo katiba mpya lazima ipite kwa halali ama kwa haramu.
Mtazamo wangu ni kuwa endapo suala hilo litaendelea kulazimishwa ndo kitakuwa kitanzi Cha CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Sababu ya kuamini hivyo ni ukweli Kuwa katiba hii haiwezi kupita bila kuchakachua kura kama ilivvyokuwa katika Bunge maalum la katiba.
Uchakachuaji huo utaamsha hasira zaidi kwa wananchi na kuiadhibu CCM kupitia sanduku la kura kwani huko watakuwa na uhakika wa mawakala watakao linda kura zao.
Jambo la msingi kwa upinzani ni kuchunguza mianya yote ya wizi wa kura na kuiweka wazi mapema. Kwa maana nyingine kura ya maoni itawezesha wapinzani kujua mbinu mpya za kudhibiti wizi wa kura jambo litakalokuwa kitanzi shingoni mwa CCM.
Nawasilisha.