KIGWANYA
Member
- Apr 14, 2016
- 81
- 103
Habari wa jamii,
Leo hii Uingereza imepiga kura ya kujitoa kwenye Jumuia ya Umoja wa Ulaya. Hii iwe funzo kwa nchi yetu tanzania kwenye hili linaloitwa Jumuiya ya Africa Mashariki. Nakumbuka kulipokuwepo na matatizo kati ya Tanzania na Rwanda nchi za Kenya, Uganda na Rwanda waliamua kufanya ushirikiano haramu "coalision of the willing" bila kuihusisha Tanzania.
Tanzania tuliamua kukaa kimya lakini ule umoja wa coalision of the willings haukudumu. Sababu ya kutokudum coalision of the will ilikua ni wazi kabisa bila Tanzania huna Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tanzania ndo nchi kubwa kieneo katika Afrika Mashariki, ndo nchi pekee yenye amani ya kutegemewa na kujivunia, ndo nchi pekee yenye opportunity za kazi, ndo nchi pekee yenye watu wenye busara na wanaopendana bila kujali itikadi zao mbalimbali.
Nchi nyingine za Afrika Mashariki haziwezi kuwa na ushirika bila Tanzania ndo maana raia wengi wa nchi hizo hupenda kukaa Tanzania na wanapopata fursa tu, basi huwa hawarudi kwao, utasikia wanajiita makabila fulani yaliyo mipakani mwa Tanzania ili tu wajulikane watanzania hivyo basi Tanzania tuwe makini sana hasa kuingia kwenye shirikisho na kuwa na rais mmoja tusikubali kabisa maana raia wote wa nchi jirani wanatamani kukaa na kuishi Tanzania kuliko watanzania kwenda huko makwao.