Kura mfumo wa Muungano isipigwe bungeni

Kura mfumo wa Muungano isipigwe bungeni

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,768
Reaction score
29,214
Kwa kuwa kuna mvutano mkali kati ya wabunge wa CCM wanaopigania katiba ya CCM (uka-CCM) na wale wa upinzani, wanaopigania katiba ya wananchi (UKAWA), ni vema kura ya kuamua aina ya muungano (wa serikali 3 za wananchi au serikali 2 za CCM) ikapigwa na wananchi wa Tanganyika na Zanzibar ili kuamua aina ya muungano wanaoutaka kuliko huu muungano feki ambao CCM wanalazimisha kuulinda hata kwa kutumia mtutu wa bunduki

Nasema hivi kwa kuwa CCM tayari wameishaanza mbinu chafu ndani ya bunge kutaka kuchakachua na kutengua kanuni ya bunge inayotaka vifungu vipitishwe kwa kuzingatia 2/3 ya kura kutoka kila upande wa muungano. Hii ni baada ya CCM kung'amua kwamba sio rahisi kupata kura hizo kutoka pande 2 za muungano.

Naomba busara itumike kusitisha shughuli za bunge na kurudisha suala hilo kwa wananchi, vinginevyo litazidi kuwagombanisha wananchi na kubomoa mshikamano na utengamano wa taifa la Tanganyila na Zanzibar. Ili kuepusha nchi kupasuka, Rais Kikwete avunje bunge tuanze mchakato upya.

Tanganyika kwanza!
 
Mh Samwel 6 naye ameamua kutoka nje ya bunge na kwenda kuwarubuni viongozi wa dini (Kardinali Pengo wa katoliki na Mufti Simba wa BAKWATA) ili wawashawishi waumini wao waiunge mkono CCM ktk harakati zake za serikali 2. This's insanity and is totally unacceptable on every ground.
 
kanun hiyo hauwezi kutenguli pia wapo wana ccm wengi hawataki serikali mbili usiwe na shaka,bunge linamaliza kazi. ndio maana sitta kaenda kuomba huruma kwa akina mufti na kadinali ili wayasahau mawazo ya serikali 2.
 
Naliona bunge la katiba likivunjika misa ya kwanza. Endapo magamba watashikilia msimamo wao wa kusigina katiba ya wananchi, bunge lazima livunjike. Na hali hii hasa ilikolezwa na Kikwete pale aliposupport Zanzibar kuvunja katiba na kuwa nchi yenye mamlaka kamili. Ni kwanini anakataa kundwa kwa Zanzibar wakati amebariki Zanzibar kujitenga? Kikwete ana lake jambo!
 
Kwa kuwa kuna mvutano mkali kati ya wabunge wa CCM wanaopigania katiba ya CCM (uka-CCM) na wale wa upinzani, wanaopigania katiba ya wananchi (UKAWA), ni vema kura ya kuamua aina ya muungano (wa serikali 3 za wananchi au serikali 2 za CCM) ikapigwa na wananchi wa Tanganyika na Zanzibar ili kuamua aina ya muungano wanaoutaka kuliko huu muungano feki ambao CCM wanalazimisha kuulinda hata kwa kutumia mtutu wa bunduki

Nasema hivi kwa kuwa CCM tayari wameishaanza mbinu chafu ndani ya bunge kutaka kuchakachua na kutengua kanuni ya bunge inayotaka vifungu vipitishwe kwa kuzingatia 2/3 ya kura kutoka kila upande wa muungano. Hii ni baada ya CCM kung'amua kwamba sio rahisi kupata kura hizo kutoka pande 2 za muungano.

Naomba busara itumike kusitisha shughuli za bunge na kurudisha suala hilo kwa wananchi, vinginevyo litazidi kuwagombanisha wananchi na kubomoa mshikamano na utengamano wa taifa la Tanganyila na Zanzibar. Ili kuepusha nchi kupasuka, Rais Kikwete avunje bunge tuanze mchakato upya.

Tanganyika kwanza!

"Tuanze upya" kivipi? Sikuelewi hata kidogo! Halafu hao wananchi elfu 37 wana nini mbona wanatetewa kiasi hicho? Ingekuwa vema kura za maoni zikaamua!
 
Mh Samwel 6 naye ameamua kutoka nje ya bunge na kwenda kuwarubuni viongozi wa dini (Kardinali Pengo wa katoliki na Mufti Simba wa BAKWATA) ili wawashawishi waumini wao waiunge mkono CCM ktk harakati zake za serikali 2. This's insanity and is totally unacceptable on every ground.

Mbona UKAWA nao wanazurura huku na huko kuwashawishi wananchi Nje ya Bunge waunge mkono Serikali 3? Kunya anakunya kuku tu akinya bata...!
 
Naliona bunge la katiba likivunjika misa ya kwanza. Endapo magamba watashikilia msimamo wao wa kusigina katiba ya wananchi, bunge lazima livunjike. Na hali hii hasa ilikolezwa na Kikwete pale aliposupport Zanzibar kuvunja katiba na kuwa nchi yenye mamlaka kamili. Ni kwanini anakataa kundwa kwa Zanzibar wakati amebariki Zanzibar kujitenga? Kikwete ana lake jambo!

Hili Bunge halivunjiki ng'o hata UKAWA watoe machozi! Kama unabisha subiri uone mijadala ikiendelea bila wasiwasi wowote! Halafu unaposema Zanzibar ni nchi "kamili" unamaanisha nini? Huo "ukamili" wake uko kwenye nini?
 
Du!!! nakumbuka maneno ya Yesu aliposema na wanafunzi wake kuwa " wataona na kusikia lakini hawataelewa chochote ndo sawa na wewe.
Zanzibar wana bendera na wimbo wa taifa sasa nakuuliza swali Zanzibar sio taifa huru? utambulisho wa utaifa ni Bendera na wimbo wa taifa.
acha ubishi wa majukwaani uliza uelimishwe.
 
Hili Bunge halivunjiki ng'o hata UKAWA watoe machozi! Kama unabisha subiri uone mijadala ikiendelea bila wasiwasi wowote! Halafu unaposema Zanzibar ni nchi "kamili" unamaanisha nini? Huo "ukamili" wake uko kwenye nini?

Ukamili wake unatokana na ukweli kwamba inaye Rais (mkuu wa nchi), wimbo wa taifa, bendera ya taifa, nembo ya taifa, mahakama, bunge, na baraza la mawaziri. Na on top of that, kama ulimsikiliza Kikwete wakati anazindua bunge la katiba, alisema Zanzibar ni nchi na akawananga wale wote wanaoibeza Zanzibar kwa kuiita 'mkoa'.
 
Naliona bunge la katiba likivunjika misa ya kwanza. Endapo magamba watashikilia msimamo wao wa kusigina katiba ya wananchi, bunge lazima livunjike. Na hali hii hasa ilikolezwa na Kikwete pale aliposupport Zanzibar kuvunja katiba na kuwa nchi yenye mamlaka kamili. Ni kwanini anakataa kundwa kwa Zanzibar wakati amebariki Zanzibar kujitenga? Kikwete ana lake jambo!

JK amesoma alama za nyakati na kuamua kulivunja bunge ili kupunguza tension na misuguano ya serikali 2 na 3. Naona ameamua kufunika kombe mwanakharam apite lakini atambue kwamba pindi bunge likianza, tensio zitarejea sawia! Hiasaidii lolote--hii ni sawa na kuahirisha maziko kwa kuamua kurefusha matanga--msiba uko pale pale!
 
Hili Bunge halivunjiki ng'o hata UKAWA watoe machozi! Kama unabisha subiri uone mijadala ikiendelea bila wasiwasi wowote! Halafu unaposema Zanzibar ni nchi "kamili" unamaanisha nini? Huo "ukamili" wake uko kwenye nini?
Kwenye suruali yako. Mburula we!
 
Mchakato wa katiba mpya ulianzishwa wakati usio wake na mtu asiyetakiwa na sababu zisizo na uzito na watu wasiohusika wameamua kuuteka mchakato na kulazimisha watakayo. hii ndio maana kuna mgongano mkubwa na kuhatarisha uwepo na hatima ya jambo zima.
 
Wakati JK anahutubia bunge, alikataa pendekezo la serikali 3 waziwazi akisema kwamba haitekelezeki. Serikali 3 ndio maoni ya wananchi, kama walivyohojiwa na tume ya Warioba, na kama walivyowahi kuhojiwa huko nyuma na tume za majaji Kisanga na Nyalali. Alichotakiwa kufanya JK sio kuponda muungano wa serikali 3 bali alipaswa atoe ufumbuzi wa hizo changamoto anazoziona kwenye serikali 3. Yeye kama mwanaCCM na kama Rais wa nchi hakupaswa kuonyesha msimamo wake wa kiCCM bali alipaswa kuwa neutral kama Rais na asingebeza maoni ya wananchi wala kuyasigina na kuyatupilia mbali.
 
Back
Top Bottom