Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,140
- 14,678
Migogoro ya ardhi hapa nchini imekithiri na imefikia hatua ya umwagaji damu.
Migogoro hii imegawanyika katika makundi mawili; wakulima na wafugaji na wananchi na wawekezaji.
Migogoro hasa ya wananchi na wawekezaji ambayo imechukua sura mpya na inaleta tafsiri kuwa serikali yetu kuwa siyo ile ya 'mgeni njoo mwenyeji apone', bali mgeni njoo mwenyeji asulubike.
Katika maeneo mengi hapa nchini, tayari kumeshatokea uvunjifu wa amani uliosababisha damu kumwagika na hata kutokea vifo. Vurugu hizi zimetokea hata kwenye maeneo ambayo udugu na kuvumiliana vilitawala na hakuna mtu aliyedhani zingeweza kutokea. Hata hivyo, bado sizioni jitihada za haraka za kumaliza migogoro hii ambazo zimeshachukuliwa na serikali yetu.
Badala yake najionea hatua za kujaribu kuahirisha matatizo haya jambo linaloweza kutuletea maafa makubwa baadaye.