Kupoteza Cheti cha NECTA

Kupoteza Cheti cha NECTA

krenea

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
405
Reaction score
160
Wasalaam.

Ndugu yangu kapoteza cheti cha kuhitimu form four kilichotolewa na Necta.Je anaweza kufata taratibu zipi kupata kingine?

Pia Necta wanaruhusu mtu baki third party kufatilia cheti cha muhusika au mpaka aje Dsm?

Katika tovuti maelezo haya hayapo.Tafadhali mwenye msaada wa taratibu kabla sijafika huko.
 
Inabidi awe na Loss report kutoka polisi........

kuna muda mwingine wanahitaji barua ya utambulisho kutoka
shule aliyokuwa anasoma, iwapo wanamtambua muhusika na kuwa
amepoteza cheti chake.........
 
Kama upo Dar fika Necta, nadhani utapata maelezo ya kutosha.
 
1.Barua ya polisi-loss report
2.Barua ya mkuu wa shule uliyosoma ikiwa na pasipoti yako
3.Ukifika baraza unapewa maelekezo kutangaza kwenye gazeti la serikali i.e. Habari Leo au Daily News
Kwa habari leo kile kijitangazo ni 20,000 na Daily News ni kama 40,000 usiniulize ni kwanini tofauti.
4.Baada ya hilo tangazo/gazeti kuwepo mtaani kwa siku saba 7 ndo unakata ile page yenye tangazo lako na
unapeleka pale NECTA then unapewa kibali cha kwenda kulipia bank kama 10,000 hivi hapo CRDB Kitijinyama afu matokeo yako yanapelekwa sehemu husika.

NB:HAKUNA CHETI KIPYA BAADA YA KUPOTEZA CHA AWALI-USIDANYAKE
HUPEWI MATOKEO YAKO DIRECT KAMA NI SEHEMU UMEFANYA APPLICATION NECTA WATATUMA MATOKEO YAKO DIRECT HUKO.

Mimi ni mhanga wa hii mambo ndo maana nimeliweka wazi kwa wengine ili wajue au usiibiwe.

Tycoon.
 
kama umemaliza after 2008,unapewa cheti kipya.
 
Baisha nashukuru for your updates nilikuwa silifahamu hilo mi form ni kitambo sana 2002
 
Last edited by a moderator:
Wahanga tupo wengi.Kama id yangu ilivyo,nami nimepoteza cha O-level na cha A-level.Nami nashukuru kwa maelezo wakuu.
 
Back
Top Bottom