AshaDii
Platinum Member
- Apr 16, 2011
- 16,189
- 18,099
Habari wana JF,
Kwanza nifurahi kwamba nipo miongoni mwenu na haswa katika kuwasilisha suala ambalo kila mmoja wetu linamgusa kwa namna moja au nyingine.
Mimi ni mdau wa MMU, napenda yale yote yanayohusisha mapenzi na mahusiano kwa namna moja ama nyingine. Leo hii ningependa tushirikiane katika kujadili mawasiliano kwa njia ya simu, pale inapohusisha mtu wa kati. (3rd party)
Kila mmoja ana maoni yake ya kupokea simu na yapo katika makundi haya:-
1. Kuna wanaokataa kwamba si sahihi
2. Kuna wanaokubali ni sahihi
3. Kuna wanaosema si sahihi hadi pale panapokuwa na sababu za msingi
Naomba kufahamu kutoka kwenu wana JF, mna msimamo upi na kwasababu zipi?
Tukumbuke, hii inaweza kutusaidia katika maamuzi na tafakuri kwa kila mmoja wetu inapokuja changamoto kama hii.
Msimamo wangu: Sina shida simu ikipokelewa na mtu ambaye sikutarajia wala sina shida shemeji yenu kupokea simu yangu.
Pamoja Saana!