Kupimwa damu kwa kutumia vifaa vya adui kunampa fursa adui yako kukupandikiza madawa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Imeandikwa na Claudius Haule Claudius

Kwanza nauomba radhi umma kwa kuchelewa kutoa tahadhali hii. Kushindwa kutoa tahadhali mapema kulitokana na kupotoshwa na imani niliyokuwa nayo kwa idara ya mkemia mkuu wa serikali ambayo sasa nina mashaka nayo makubwa kutokana na hoja za kisheria zilizovunjwa na serikali ambayo ni mwajiri wa mkemia mkuu wa serikali.

Kama serikali imevunja sheria za utaratibu wa upelelezi na ukamatajj wa mtuhumiwa wa makosa ya jinai basi nj wazi huo ni ushahidi kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuvunja taratibu za upimaji wa damu pamoja na kukiuka haki za upimajj wa damu katika idara ya mkemia mkuu wa serikali.

Inawezekanaje mlalamikaji, mpimaji, shahidi na mkamatajj awe huyo huyo mmoja dhidi ya mlalamikiwa? Hapa sheria inawezaje kutoa haki? Kama upo ushahidi wa ukiukwajj wa sheria, je, uvunjaji wa sheria hizo haukusudia kuwalazimisha watuhumiwa wahujumiwe usalama wao kwa visingizio vya upimaji wa damu zao? Je umma unafahamu kama kuna uwezekano wa kumpandikiza mtu virus vya magonjwa mbalimbali kupitia upimaji wa damu?

Je Tanzania imeweka mazingira gani ya kisheria ya upimaji damu ambayo yanahakikisha usalama wa mtuhumiwa dhidi ya mlalamikaji? Je kifaa cha kutolea damu ni cha mtuhumiwa au cha mkemia wa serikali? Kama kifaa ni cha mkemia mkuu wa serikali basi kifaa hicho kitawawezesha watuhumiwa wote kushinda mashtaka yao dhidi ya serikali. Lakini kama kifaa hicho cha kutolea damu ni cha mtuhumiwa hapo serikali inaweza kushinda mashtaka iwapo haisimami mahakamani kama mlalamikaji. Kwa sababu ni vigumu kisheria kuwa mlalamikaji, mkamataji na shahidi huyo huyo mmoja kwa wakati mmoja.

Mbaya zaidi na hatari zaidi kama mlalamikaji ambaye ni serikali alitumia kifaa chake cha kutolea damu dhidi ya mtuhumiwa, je, kutakuwa na usalama kwa kiasi gani kama zoezi hilo lilifanyika bila chuki dhidi ya mtuhumiwa? Ikiwa kulikuwa na chuki kati yao nini kiliweza kumzua mkemia mkuu wa serikali asipandikize virus au madawa ya kulevya kwa mtuhumiwa ili kutii amri ya mwajiri wake ambaye ni serikali?

Kama kwenye uchaguzi wa viongozi tuna weka mawakala ambayo ni mashahidi, je serikali kwa nini haikuandaa mazingira ya kisheria ya uwepo wa mashahidi wa pande zote mbili za mlalamikaji na mtuhumiwa? Kwa nini kesi hizo za kuhakiki wa watumiaji wa madawa ya kulevya hazikuanzia mahakamani ili kutengeneza utaratibu wa kisheria wa kupanga ushahidi wa pande hizo mbili hasimu za mlalamikaji na mtuhumiwa? Serikali ilikuwa na malengo gani kuvunja taratibu hizo za sheria? Hapa ni lazima kuna kitu nyuma ya pazia ambacho serikali anakifanya.

Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia kuna uwezekano mkubwa wa kumpandikiza mtu kemikali za nyuklia ambazo zitasababisha kuzaliwa kwa virus waliokusudiwa kwenye damu ya mtu husika. Au akapandikizwa moja kwa moja virus au vijidudu vya homa ya kuuwa.

Je tutamwaminije mkemia mkuu wa serikali kama Yusuph Manji alitoka nyumbani kwake mzima na baada ya kupimwa tu na mkemia mkuu wa serikali alipata homa ghafla na kulazimika kulazwa? Kwa nini apate homa baada ya kupimwa?

Kama vifaa vya kutolea damu vilikuwa vya mkemia wa serikali basi watuhumiwa wote waliogunduliwa madawa ya kulevya na mkemia mkuu wa serikali watashinda kesi dhidi ya serikali kwa hoja kuwa ndiye aliyewapandikiza madawa hayo ya kulevya. Watuhumiwa wa madawa ya kulevya muwe makini na hoja ya vifaa vya kutolea damu kwa sababu kuna utaratibu wa kisheria umekiukwa katika upimaji wa kuhakiki damu kama ina madawa ya kulevya au haina.

Pia mna haki ya kudai fidia ya ukiukwaji huo wenye mashaka ya kuhatarisha uhai wenu kwa hofu ya uwezekano wa mlalamikaji kupandikiza madawa ya kulevya na virus vya homa mbalimbali kwenye damu yenu.

Huu unaonekana ni ugomvi kati ya nyoka na nguchiro. Ni utata mtupu!!!!

Ni Mimi Claudius Haule Claudius.
 
Attachments

  • nguchiro.jpg
    nguchiro.jpg
    55.1 KB · Views: 65

Mwanahabari , you are very right, niliandika humu kuwa hapa inaweza ikaja defence ya implanted evidence! Procedure for taking samples, chain of custody etc in a criminal investigation were not complied with, this very much I am sure!
 
Sasa mseme hapa mnataka kumtetea NANI?????.....kama wangekuwa wanafanya huo UJINGA manosema nadhani hata GWAJIMA leo hii tungekuwa tumeishaambiwa ni mtumiaji.....Tatzo kubwa la nyie vijana wa kitanzania mnnakosa muda wa kufikiria mambo ya msingi kwa faida yenu ila mnapata muda wa kugeuza X kuwa Y.........
 
wewe ukiwa hujui nini kinaendelea katika jambo uliza kuliko kutuhumu wewe ndiyo mjanja kuliko Manji? Kilichompata Manji ni "withdraw effect" acha kuuza ubuyu kama watanzania wote ni watu wasio na ufahamu wa mambo. Huyo mwenyekiti wako anaogopa nini ? Poleni sana na pole zaidi kwa familia yake he he hata Mjinga anajua sasa uoga wenu nini. Mnaongozwa na wala unga? he akapime London kama mkemia amuamini kuliko kuzuia mahakamani because itafika siku watampima tuu. So a shamed by that.
 
Ni kama vile sijakuelewa ama wewe ndiye usiyeelewa. Mwanasheria wa serikali, polisi, mkemia Mkuu, mkaguzi wa mahesabu, nk vyote ni vyombo vya serikali. Si mahakama hizo, wakimaliza kuutafuta ushaidi watakupandisha mahakamani tatizo liko wapi hapo?

Ulitaka awepo mkemia huru au? Nani kasema kuna uadui ktk siasa za upinzani? Eti tena uadui na serikali ilioko madarakani, huu ni ujuha wetu tu waafrika. Siasa za upinzani zinakinzana ktk Sera na mirengo tu, si vinginevyo.

Kwakuwa zetu hapa hazina Sera wala itikadi inayosomeka, wanajengeana uadui wa kinafiki. Wasioelewa, wazidi kupotoshwa. Naikumbuka Zanzibar ile, kuzikana kichama. Mungu ibariki Afrika, ibariki Tanzania, hizi mvua ziendelee kunyesha.
 
Hili nalo neno. Kupimwa damu na watu waliotumwa na Magufuli hii mbona ni hatari kubwa.
Nikijiweka kwenye nafasi ya hao waliopimwa, naogopa sana maana katika watu ambao sina imani nao hata chembe, ni Magufuli.
 
Ndugu mleta uzi, uko sahihi kabisa. technically serikali imekosea na imekurupuka bila kufuata procedure hasa zinazotakiwa kufuatwa. kuna msemo wa kilatin unaosema nemo iudex in causa sua...(Rules against biasness) na ndo maana tunashangaa serikali kuwa ndo mlalamikaji, ndo mpimaji wa watumiaji wa madawa, na ameshawahukumu tayari kabla hata hukumu ya mahakama haijatoka. kama wahanga wa makonda na seerikali kwa ujumla watapata uwakilishi mzuri mahakamani, watashinda kesi...
 
Ni kama vile sijakuelewa ama wewe ndiye usiyeelewa. Mwanasheria wa serikali, polisi, mkemia Mkuu, mkaguzi wa mahesabu, nk vyote ni vyombo vya serikali. Si mahakama hizo, wakimaliza kuutafuta ushaidi watakupandisha mahakamani tatizo liko wapi hapo?

Ulitaka awepo mkemia huru au? Nani kasema kuna uadui ktk siasa za upinzani? Eti tena uadui na serikali ilioko madarakani, huu ni ujuha wetu tu waafrika. Siasa za upinzani zinakinzana ktk Sera na mirengo tu, si vinginevyo.

Kwakuwa zetu hapa hazina Sera wala itikadi inayosomeka, wanajengeana uadui wa kinafiki. Wasioelewa, wazidi kupotoshwa. Naikumbuka Zanzibar ile, kuzikana kichama. Mungu ibariki Afrika, ibariki Tanzania, hizi mvua ziendelee kunyesha.
Mkuu nadhani haujauelewa uzi huu vizuri, mtuhumiwa hapaswi kupelekwa kwa mkemia kwa matakwa ya serikali (mshitaki) bali mahakama. Kwa sababu sheria inahitaji ushahidi wa kuthibitisha kuwa mtuhumiwa ataridhika na majibu ya vipimo. Polisi hawapaswi kupelekwa mtuhumiwa kwa mkemia bila kuptia mahakamani kwani kwakuwa walikuwa wanawatuhumu wangewapeleka mahakamani kwanza ndo sasa mahakama ipelekwe kwenye vipimo. Wanasheria tusaidie kwenye hili.
 
Na kitu kingine cha ajabu ni kuwa wote waliopelekwa kupimwa HAWA kuwa na wawakilishi kuthibitisha kilichokuwa kikifanyika.
Alipaswa ili haki itendeke, na ionekane imetendeka alipaswa ifanyike kama ilivyofanyika polisi.
Polisi manji alikwenda na mawakili wake basi pia alipaswa hata kwa mkemia aende na mkemia wake kuthibitisha kinachofanyika.
Sasa wewe unatolewa damu halafu mnaambiwa subilini hapo majibu hapo nje. Je mtajua nini kinachoendelea ndani?
Hii bwana hufanyika Tanzania tu
 
Ni kama vile sijakuelewa ama wewe ndiye usiyeelewa. Mwanasheria wa serikali, polisi, mkemia Mkuu, mkaguzi wa mahesabu, nk vyote ni vyombo vya serikali. Si mahakama hizo, wakimaliza kuutafuta ushaidi watakupandisha mahakamani tatizo liko wapi hapo?

Ulitaka awepo mkemia huru au? Nani kasema kuna uadui ktk siasa za upinzani? Eti tena uadui na serikali ilioko madarakani, huu ni ujuha wetu tu waafrika. Siasa za upinzani zinakinzana ktk Sera na mirengo tu, si vinginevyo.

Kwakuwa zetu hapa hazina Sera wala itikadi inayosomeka, wanajengeana uadui wa kinafiki. Wasioelewa, wazidi kupotoshwa. Naikumbuka Zanzibar ile, kuzikana kichama. Mungu ibariki Afrika, ibariki Tanzania, hizi mvua ziendelee kunyesha.
Nakuunga mkono katika para ya kwanza, lakini para ya pili umeonesha ushabiki usiosameheka bro. Africa, Tanzania hakuna uhasama wa kisiasa!!?? Unadanganya kitu kilicho wazi hata mtoto mdogo anaweza kukueleza hili kwa uwazi. Kuna watu wanasema hawawezi kuwapa mbwa (wapinzani) chakula cha watoto(chama tawala) halafu unasema hatuna uhasama wa kisiasa. Angalia wanaoshabikia kukamatwa wapinzani kama ni wapinzani wenzao, angalia wanaoshangilia ccm wanapopata matatizo kama ni ccm wenzao!! Tusilete utani kwenye mambo serious, katika hili tunahtaji muafaka wa kitaifa siyo blabla za kufunika moto chini ya carpet tutaumbuka.
 
wewe ukiwa hujui nini kinaendelea katika jambo uliza kuliko kutuhumu wewe ndiyo mjanja kuliko Manji? Kilichompata Manji ni "withdraw effect" acha kuuza ubuyu kama watanzania wote ni watu wasio na ufahamu wa mambo. Huyo mwenyekiti wako anaogopa nini ? Poleni sana na pole zaidi kwa familia yake he he hata Mjinga anajua sasa uoga wenu nini. Mnaongozwa na wala unga? he akapime London kama mkemia amuamini kuliko kuzuia mahakamani because itafika siku watampima tuu. So a shamed by that.
Haaaaaah! Ni proved anakula unga!??! Unga kabsaaaah! Mungu tusamehe hatujui tutendalo!
 
UNadhani ofisi ya mkemia mkuu inafanya kazi kama makanjanja mnaonunuliwa na pesa ya madawa?unayajua maadili ys kazi za kisayansi?
Mgeni hapa Tanzania?dawa za kulevya zinageuka majivu kwa mkemia mkuu....
 
Mwanahabari , you are very right, niliandika humu kuwa hapa inaweza ikaja defence ya implanted evidence! Procedure for taking samples, chain of custody etc in a criminal investigation were not complied with, this very much I am sure!
Haswaaa, na sina hakika kama hao wakubwa walilifikiria hivyo kabla ya kufanya hivyo.
 
Mkuu nadhani haujauelewa uzi huu vizuri, mtuhumiwa hapaswi kupelekwa kwa mkemia kwa matakwa ya serikali (mshitaki) bali mahakama. Kwa sababu sheria inahitaji ushahidi wa kuthibitisha kuwa mtuhumiwa ataridhika na majibu ya vipimo. Polisi hawapaswi kupelekwa mtuhumiwa kwa mkemia bila kuptia mahakamani kwani kwakuwa walikuwa wanawatuhumu wangewapeleka mahakamani kwanza ndo sasa mahakama ipelekwe kwenye vipimo. Wanasheria tusaidie kwenye hili.
Hapa upo sahihi kabisa.
Na wasichojua ni kuwa ukikosea utaratibu wa kupata ushahidi, basi yawezekana ushahidi wako usiwe admissible mahakamani. Ila sasa hapo ni pale ambapo utawala wa sheria unaheshimika, siyo sasa ambapo neno moja toka kwa Sirro au Makonda au mwenye heri mwingine yeyote ni ushahidi usiopingwa na mtu yeyote duniani na mbinguni...
 
Back
Top Bottom