KWELI Kupigwa vibao tumboni wakati wa Mazoezi husaidia kubana Misuli ya tumbo

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Ushiriki wa mazoezi ni jambo muhimu kwa afya. Husaidia kuongeza utimamu wa mwili pamoja na kuupa kinga ya kutosha dhidi ya magonjwa, hasa yale yasiyoambukizwa kama kisukari, shinikizo kubwa la damu na viribatumbo.

F43F5179-FB74-4F37-A668-705242050799.jpeg

Pamoja na faida hizi, watu wengine hushiriki mazoezi mbalimbali ya Gym kwa lengo la kuboresha muonekano wa miili yao, tunaweza kusema kwa sababu za urembo au utanashati.

Miongoni mwa mazoezi yanayofanyika sana siku hizi hasa kwa wanawake ni kupiga vibao sehemu ya chini ya tumbo ili kubana misuli.

Je, ni kweli kuwa mazoezi haya husaidia kubana misuli ya tumbo?
 
Tunachokijua
Sehemu ya chini ya tumbo kitaalam huitwa Abdomen. Huudwa kwa aina 5 tofauti za misuli ambayo pamoja na kazi zingine, huusaidia mwili kufanya mambo yafuatayo-
  • Kujisaidia haja kubwa na ndogo, kupiga chafya, kukohoa na kutapika.
  • Kuongeza mijongeo ya misuli ya tumbo wakati wa kujifungua mtoto.
  • Kulinda pamoja na kuziweka mahali sahihi ogani muhimu zinazopatikana tumboni kama vile mfuko wa chakula (tumbo lenyewe), utumbo, kongosho, wengu, figo, ini na mfuko wa nyongo.
  • Kusaidia uti wa mgongo wakati wa kukaa, kusimama na kujikunja.
Misuli hii ambayo kwa lugha maarufu hufahamika kama Abs, hupangwa kwenye safu mbili ambapo aina 2 kati yake huwa imesimama na aina 3 zinazobaki huwa zimekaa kwa kulazwa.

Kubana misuli ya tumbo
Kimuundo, kama tulivyoelezea awali, misuli hii huunda sehemu ya chini ya tumbo ambayo kitaalam huitwa Abdomen. Kujikaza au kulegea kwake huwa na athari za moja kwa moja kwenye sehemu hiyo inayounda kipande cha chini ya tumbo.

Tendo lolote linalolegeza misuli hii hulegeza tumbo, na tendo lingine la namna hii linalobana misuli hii hubana tumbo pia.

Hivyo, upigaji wa vibao sehemu ya chini ya tumbo kwa kutumia vifaa maalum husaidia kubana misuli kwa mhusika pamoja na kuongeza ustahimilivu wa maumivu kwa watu wanaoshiriki michezo ya mieleka na ngumi.

Tahadhari
Matumizi ya nguvu kubwa yanaweza kusababisha mkazo wa misuli (Muscle Strain) ambao humfanya mhusika apatwe na maumivu makali wakati wa kucheka, kupiga chafya, kukohoa na kunyanyuka. Hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi kwa kusababisha maumivu ya kudumu ya tumbo pamoja na kuathiri mijongeo ya misuli ya mwili.

Zoezi hili linaweza pia kuleta ulemavu wa kudumu au hata kifo ikiwa ogani muhimu za mwili hasa Ini, kongosho, figo, tumbo na utumbo vitapatwa na majeraha makubwa. Kumbuka, eneo hilo hutumiwa na mwili kuhifadhi na kulinda viungo hivyo.

Aidha, visa kadhaa vya kuvujia damu ndani ya mwili na kuvunjika kwa mbavu vimeripotiwa. Ni hali ya dharura inayoweza kusababisha kifo ikiwa haitashughulikiwa kwa uzito unaostahili.

Ushauri
Mazoezi haya yanapaswa kufanyika chini ya usaidizi wa mtu aliye na ujuzi wa kutosha ili kuepusha hatari zinazoweza kujitokeza ambazo huathiri moja kwa moja ubora wa maisha (Quality of life) ya mhusika.
Shukrani kwa mada nzuri, naomba kujua aina zingine za mazoezi ambayo husaidia kubana misuli ya tumbo?

Swali lingine eti ni kweli kuwa mtu aliyekaza misuli ya tumbo husaidia kuimarisha ushiriki wa tendo la ndoa?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom