Sijui kuhusu yeye kama kuna shida mahala ama lah!!
Binafsi mimi ni mvivu kinoooma kupiga simu, huu ni udhaifu wangu, kuongea muda mrefu kwenye simu naona tabu,
Mke wangu yupo km 500 kutoka nilipo mimi, anajua kuwa hilo ni tatizo langu, imebidi siku hizi awe ananikumbusha fulani umewasiliana nae, umemjulia hali, haya wasiliana nae sasa hivi unipe mrejesho.
Kwake imekuwa si tatizo katika mara 20 tutakazo ongea kwenye simu basi mara 19 kapiga yeye, akiwa likizo kwa siku anaweza piga simu hata mara 5.
Nikimpigia anafurahi kuwa naanza badilika kwa ajili yake, ila nisipopiga sio kesi anajua ndio udhaifu wangu
Kwanza ngoja nimpigie mara ya mwisho kupiga mimi ni majuzi aliponitxt nimpigie salio limeisha [emoji23]