Kupiga Kura Siku ya Jumapili imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupiga Kura Siku ya Jumapili imekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkombozi, Apr 1, 2012.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Wakuu,kwa nini kila chaguzi unafanyika siku ya Jumapili?Tume kwa kushirikiana na serikali wangepanga katikati ya wiki ila iwe siku ya mapumziko katika eneo husika.J2 watu waende kanisani,wapike,wafue na wengine wanapumzika.Ndio maana Arumeru wanalalamika watu wachache sana vituoni.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Mkuu unatafuta maneno. Watakuja wehu hapa watakuambia unaongozwa na mfumo Katoliki.
  Besides, wanaharakati wa ile dini wanajipanga kupigania IJUMAA iwe siku ya mapumziko. Hili litafanyika mchakato wa katiba mpya utakapoanza
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Amini nawwambia, hata ingekuwa kupiga kura ni siku ya Jumatatu bado watu mngelalamika tuu.
   
 4. k

  kicha JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 532
  Trophy Points: 180
  yani mkuu ndo mwisho wako wa kufikiri kweli umefikia apo? pole sana, bac tufanye j3 unaonaje?
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Bila shaka sherehe ya leo inakuhusu.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280

  Mkuu hili suala linazungumzika. Kwangu mimi si sahihi kufanya uchaguzi siku ya jumapili hasa uchaguzi mkuu. Siku ya jumapili ni siku ya mapumziko na pia ni siku ambayo wakristo wengi huenda kwenye ibada. kwa mfano leo imeangukia siku ya jumapili ya matawi ambapo hata wale ambao huwa hatuendi kanisani leo hujitutumua na kujihudhurisha pamoja na siku ya pasaka na krismas. Ni vyema ikawa siku ya kazi na isiwe ijumaa pia.
  Rev. hilo la Ijumaa kuwa siku ya mapumziko pia linaweza kuzungumzika. Tutajiuliza ni kwa nini tulizifanya jumamosi na jumapili kuwa siku za mapumziko ilhali wenzetu wa kule mashariki ya. ya kati Ijumaa huwa siku ya mapumziko. Kutokana na religion profile ya nchi yetu nadhani kuna siku kweli jamaa nao watadai na watakuwa na haki kufanya hivyo.
   
 7. bht

  bht JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ridiculous....
  Kuna wengine hapa hatuangukii ijumaa wala jumapili na sisi mtatupeleka wapi?
  Watu mnakuwa hypesensitive unnecessarily
   
 8. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  j2 poa tu. muda unatosha kuanzia saa moja hadi kumi
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Wataangalia uwingi mkuu.
   
 10. S

  SI unit JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  .
  Kama ni wingi basi wanaoabudu jumapili bado watashinda coz ndo wengi..!
   
 11. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Rev Mzitto ndio Jussa wa Chadema?
   
 12. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Iwe J2 au Ijumaa au J3 au siku nyingine yoyote, kupiga kura sioni taabu twaweza kupiga kura siku yoyote, lakini taabu ni wezi wa kura kama kubadili siku kutakuwa kumewakomesha wezi wa kura basi hiyo siku itakuwa pia siku yetu ya mapumziko maana uadilifu utakuwa umepatikana.
  Kwa suala la kupumzika j1 na j2 na badala yake au tufanye Alhamisi na Ijumaa au Ijumaa peke yake au siku nyingine yoyote, bado linazungumzika, lakini ukweli unabaki kuwa hatuwezi kupata siku itakayoridhisha wote maana wengine wana blue monday na wengine huenda mungu wao anawaambia wapumzike j5 au wengine siku nyingine. La muhimu ni kila mmoja kuheshimiwa ktk dini yake, lakini heshima haitokani na siku ya mapumziko bali waamini wa dini husika kujihusisha na dini yao kwa uhuru bila kuzuiliwa ambalo nadhni kama ni demokrasia katika hili TZ hatuna shida. Vinginevyo kudhania kuwa tukipumzika ndiyo dini yetu inapata heshima zaidi, tutakuwa waongo tu maana heshima ni sisi wenyewe wa dini fulani kuheshimu na kujitahidi kuenzi dini zetu bila kuathiri dini za wengine
   
 13. Clarity

  Clarity JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 810
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 80
  Ndio siku muafaka kabisa maana ndio siku ya mapumziko hivyo basi kula mmoja anapata nafasi ya kwenda kupiga kura kwani huko kusali ni kutwa nzima ?
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Inawezekana mkuu lakini ujue wenzetu wanakujaga na ile hoja ya kwamba wao wanaongezeka kwa.kaasi kwa kuwa baba mmoja anaweza kuoa aroba na hao aroba kil mmoja akizaa watatu basi baba mmoja atakuwa na 12! Sisi mtu mmoja mtu mmoja ukifuata wa mpango basi unaweza kuishia 4!
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Waislamu hawahitaji siku ya mapumziko ila MUDA WA KUSALI IJUMAA from 12-2pm period

  Hayo ya siku ya mapumziko umesema wewe mgalatia mwenye chuki na uislam
   
Loading...