Ushauri mzuri...lakini kuna jambo tu nafikiria kivivu hapa, bila shaka kondomu zilitengenezwa kwa matumizi yafuatayo:
1. Kuzuia ujauzito kwa wanawake
2. Kujikinga na maambukizi dhidi ya HIV na STD's
Sasa hiyo nambari 2 ndiyo inayonifanya nifikirie kivivu kwa kutumia nadharia hii...
Kama mipira hii ilitengenezwa kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi,
Je walengwa ni kwa wale watu wenye mpenzi mmoja tu au wale wenye utitiri wa wapenzi?
Kama mtu ana mpenzi mmoja tu, kwa nini umtengeneze kinga, ajikinge kwa lipi?
NB:
Binafsi naona jambo la muhimu kusisitiza hapa ni UAMINIFU tu, huwezi kuvaa mpira katika muda wote wa mahusiano/ndoa.