Hata ukibeti mkeka wa kula hela nyingi. Ukawa unaisubiria timu moja unaiangalia kabisa na labda ulibeti AWAY WIN,
dakika ya 3 tu ikawa 0:1
Mechi ikaenda hivyo hivyo mpaka dakika 90. Refa akaongeza dakika 4 za nyongeza. Kichwa hapo kinachakata mahesabu makali ya hela yako utakayopata labda ni 24,000,000.
Dakika ya 93 HOME anapata corner, inapigwa ndefu inaokolewa na kichwa lakini anatokea mchezaji mshenzi alibaki nyuma anapiga ndefu kipa anaigusa lakini inakuwa ya moto moja kwa moja ndani na unaona wachezaji wanashangilia hao tayari 1:1.
Hapo tayari dakika ya 93 sec46.
Unamwona kama refa kastopisha mpira anasikiliza radio labda kuna mchezaji wa home alimshika mchezaji wa timu yako na akamwangusha.
Hapo mwili unakufa kama ganzi hivi unamwangalia refa kwa huruma maamuzi yake yatakuwaje.
Mara refa anachora mstatiri kuashiria amesha-review tukio kupitia VAR, no offense. Ananyosha kidole mpira uwekwe kati, ni goli halali.
Hapo ndio utasikia wazungu hao hao hao.
Ilinitokea 2020 mkeka wa 8,000,000+