******
Inaendelea.....
Kama ni mechi basi ile ilikuwa mechi haswaa. Wawili sisi tulikuwa katika ziwa Tamu la mapenzi.
Sio Mimi si Arafa wote tulikuwa hoi baada ya kutupiana makonde yenye uzani mkubwa. Mechi iliisha baada ya masaa manne tokea saa tisa mpaka saa moja usiku ambapo Mimi nilipiga magoli mann. Moja likiwa na kichwa, jingine la Skocha, la tatu la tiki taka na la mwisho ni shuti kali nje ya kumi na nane ambapo Arafa alilirukia na kujikuta amekumbatia upepo badala ya mpira. Goli la msimu ambalo Arafa alikuwa analisimulia ni lile la tiki taka. Akanambia; yaani Mahabuba wangu goli la tatu lilokuwa lamoto lilovyokuwa likiingia nilihisi moto wake. Basi lilikuwa tamu kweli.
Arafa kwa upande wake alipiga Magoli matatu huku akishindwa kutoa suluhu baada ya kunyosha mikono juu kwa kuchoka.
Tulienda kuoga huku tukiimba Kama watoto wadogo. Kiukweli Arafa alikuwa na sauti nzuri nadhani ni kutokana na ulaini wa shingo yake na mpangilio mzuri wa ala sauti Kama vile meno na ulimi mlaini.
Sikujua Kama Arafa pia alikuwa ana dimpo la shavu moja. Huku macho yake yakinakshiwa na nyusi nyeusi za wastani.
Mapenzi ndio kwanza yalikuwa yanachanganya. Mtoto simu zilikuwa hazikauki, text kila Mara. Basi kuna wakati alikuwa ananipigia alafu utasikia akisema nimemiss goli la msimu yaani lile la tiki taka.
Na Mimi namjibu naipenda ile style ya IS(Alkaida). Tunacheka siku inaisha.
Zawaidi zilikuwa hazikauki, kila akija Lazima aje na hiki Mara kile. Basi nilikuwa katika wakati mgumu Kama mwanaume kwa sababu Mimi zaidi ya hela ya bumu sikuwa vizuri kiuchumi. Hivyo sikuweza kumpa zawadi kila Mara kutokana na hali yangu kiuchumi.
"Nakupenda sana Michaelray kiukweli umeweza kuniteka nikatekeka, naomba usije kuniacha"
Arafa aliongea huku macho yake yakionyesha usiriazi wa kile anachokiongea.
"Arafa mpenzi wangu, hata Mimi nakupenda Sana. Ni furaha yangu kukupenda mpenzi, napenda niitimize furaha yako. Nitailinda na wala sitokaa nikuumize"
Tulikimbatiana kisha nikamsindikiza kwao. Tukiwa njiani macho ya watu yalikuwa kwetu. Hii ni kutokana na jinsi tulivyopendeza.
Nilijiona mwenye bahati kubwa kuwa na mrembo Kama Arafa katika jiji la Dar es salaam
Kuna siku Arafa alikuja kunitembelea chuoni. Basi rafiki zangu wa kike hawakuamini Kama kweli Michaelray naweza Miliki mtoto mkali kiasi kile.
Kila mmoja alikiri kuwa nimeotea dodo kwenye mpera.
Japo kwa swaga walikuwa wananielewa lakini Pesa ndio ilikuwa tatizo Kama mnavyojua mjini mtu pesa.
Tuliweza badili sehemu mbalimbali za kukutana kulingana na umbali na gharama.
Nilijitahidi Sana kuonyesha kuwa na Mimi naweza kuwa na mwanamke Kama Arafa.
Ama kweli mapenzi sio pesa Kama mwanamke anakupenda.