Kupendwa na wengi,,chanzo cha upofu wa kuchagua mtu sahihi

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,534
4,185
^^
Kila mmoja analo hitaji la kupendwa.Kuna wanaotumia nguvu nyingi ikiwemo rasilimali ili wapendwe.Na wengine hawatumii nguvu yoyote ili wapendwe.Na wapo ambao hawajui wako wapi.
....
Lakini katika sayari ya mapenzi,ufikapo wakati wa kuoa au kuolewa ipo hali hujitokeza kwa wengi.Hali yenyewe ni mtu kupendwa na wengi kiasi cha kuathiri uamuzi wake wa kumchagua mtu sahihi atakaemfaa katika ndoa.
....
Hutokea mwanamke akapata mchumba wa kumuoa na hapo hapo wakajitokeza wengine wengi na mwanaume akipata mchumba wa kuoa basi ndo wanawake hujifanya wanajua kuwa nae ni mwanaume.Naomba nitoe mfano kidogo niliowahi kuuona katika mapito ya kutimiliza kiu ya ndoa.
....
Miaka sita iliyopita nilimchumbia dada mmoja,ambae niliona ananifaa kwa ndoa.Binti akakubali na nikaanza hatua za awali za utambulisho.Basi bwana watu walipojua binti anataka kuolewa,,wanaume wa kila sifa wakajitokeza kwa nia ile ile ya kumuoa.Ndani ya wiki mbili binti huyu alikuwa na wanaume 8 wenye nia ya kumuoa.Kulikuwa na mabosi,mfanyakazi wa benki,wakulima,na choka mbaya kama mimi.Ni kana kwamba nilimfungulia nyota ya kupendwa.Binti akaniita kwa wema akaniambia haiwezekani mimi kumuoa akanisihi nimsamehe.Nikamwambia asijali,naelewa anachopitia..Basi nikaendelea na mengine huku ripoti zikisema amemchagua benki teller,,Kwa wakati ule niliondoka kule alipokuwa kwani sikuwa mkaaji na nilisitisha mawasiliano yote.Hata hivyo baada ya miaka sita nilitembelea mkoa ule na nikashangaa kumkuta dada wa watu akiwa kwao,hakutaka kuongea na mimi ila watu wa pembeni nilipowadadisi wakasema ile tangazo la ndoa yake ilipata vipingamizi vikali kwani yule bwana alikuwa ana mke na watoto.Na tayari wachumba wengine walikuwa wameyeyuka.Na sasa anazalia nyumbani kila baba na mtoto wake.
....
Ninachotaka kusema
hapa ni kuwa, kila mmoja hufika wakati hukumbwa na upofu wa kuchagua mwenza sahihi hususani unapopendwa na wengi.Mapenzi wakati mwingine yanatupa wakati mgumu sana wa kuamua.Wale wanaopitia nyakati hizi ni mtazamo wangu wazingatie yafuatayo
....
USIMSAHAU MLIETOKA NAE MBALI
Mpenzi mlievuka nae milima na mabonde anakujua vizuri na yuko tayari kusimama nawe nyakati za shida.
....
PUUZA MATAMANIO YA KIMWILI
Kumpata mtu kwa vigezo vya mali, umaarufu au mengine ni jambo jema japo si salama wakati wote.Sikiliza moyo wako.Mafanikio katika maisha mtapata tu hata na huyo ambae hana
....
HATA KAMA HUMUAMINI MUNGU hapa utajua umuhimu wake,maana ni wakati ambao utapata ushawishi wa kila aina toka kwa wazazi,marafiki,ndugu n.k Ila ujue ndoa yako itakuhusu wewe na si hao.Rafiki wa kuamini wakati huu ni Mungu ambae ukimshirikisha vema upofu utatoweka.

jazakallah kheir,as long nipo kwenye mchakato wa kusaka jiko,najitahidi sana kumuomba Allah kwenye sala zangu,anipe mke mwema
 
Somo zuri sana,tena wanawake ndo wako disadvantaged na hii falsafa
Cc Madame B
 
Hapo ndo atajulikana mpenda mtu na kitu,mchele na pumba zitajitenga!!
 
Duh ka unansema! Ila sijaolewa bado.. Somo ad line'nsisimua akyanani!
Yan af sjuw wanatokeaga wapi! Kama wameagizwa nenda pale!!
 
Swts wanapanga foleni utadhani benki
^^
 
Last edited by a moderator:
Hapo ndo atajulikana mpenda mtu na kitu,mchele na pumba zitajitenga!!

^^
Watu wanakuja na makoti ya kuazima,magari ya kukodi.. Kwa wadada atakuja na nidhamu ya kupiga magoti mpaka chini,,kuimba nyimbo za kusifu Mungu, lol
^^
 
pana mitihani migumu na mizito kwenye hii stage na kama usipokuwa makini vya kutosha utajikuta unakuwa mtu wa majuto tu
 
Himidini ahsante...najifunza mambo mengi ya busara kutoka kwako....namuomba sana mungu anipe mume mwema!inshallah kheri!
 
Last edited by a moderator:
ilmu murua kwa wanawake! sio kila saa ooh pesa oooh magari, hivi pesa ndio suluhisho la kuwa na ndoa tamu? just curious¡
 
hakuna jambo gumu jama kumchagua mwenza wa kuishi nae kwa miaka yote ilobaki hapa duniani, yan mtu utakae lala nae na kuamka nae, kwenye shida na raha, ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom