Kupelekwa Madini ya Tanzanite kwenye maonesho Marekani

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
7,563
13,276
Habari zenu Wadau

Leo katika Habari za Biashara ITV nimesikia kuna kampuni moja inataka kuandika barua kuomba madini ya Tanzanite tuliyoyanunua kwa bei ghali zaidi na makubwa zaidi dunia nzima yaende USA kwenye maonesho. Yafutayo ndio niliyojiuliza

Mosi, Ingawa wazo ni zuri ila tunauhakika gani na madini hayo yaende huko kwa mabeberu na yaangaliwe yarudi bila ya wao kutuchezea rafu na hila zao?

Mbili, hakuna mtu asiejua kuwa madini yale yanathamani kubwa, sasa kwa baadhi ya viongozi wetu wanaonunulika kirahisi tuna uhakika gani kuwa hatutaangukia pua kwa kuletewa vioo vya rangi ile ya Tanzanite badala ya dini lenyewe?

Hivi ukirejea tu kwenye janga la Corona, wanashindwa vipi kuyatanzanite-Corona hayo madini?

Hili wazo siliafiki hata kidogo, kama hoja ni kuliangalia tu hilo dini la tanzanite tulilouziwa na 'leizer- mmasai' ni Bora wapelekewe video clip waangalie atakaelipenda aje hapa Tanzania alione alipie utalii ukue.

Nawakaribisha waungwana tuijenge nchi yetu

Nawasililisha!
 
Hiyo kampuni yenyewe itakuwa ni mbongo yupo kati.

BTW: Hata huko yalikohifadhiwa sasa kuna walakini mwingi tu juu ya usalama wa hiyo tanzanite.

Cocaine iliyopelekwa kwa Mkemia mkuu imewahi kugeuka unga wa mhongo kipindi fulani.

Walimu ndo wanaongoza kwa kuingizwa mkenge according to taarifa za TAKUKURU na ikulu kuna Mwalimu.😁
 
Walimu ni wazuri sana kwenye kusimamia
Ukileta ujinga unakula mboko
 
Ninavyo jua na dunia nzima inavyojua ni kwamba, Tanzanite kubwa zaidi iliyowahi kupatikana ipo Thailand. Inachungwa kuliko ulinzi. Hao hao wamarekani huenda huko kujipigisha picha na hiyo Tanzanite. Inasemekana, weshajipatia mapato kama mara 7 ya bei waliyoinunulia na bado walikuwa wanaendelea kulipwa kiingilio. Sisi tutakuwa majuha kuipeleka huko Marekani kwenye maonyesho. Kama hawaamini waendelee kutokuamini hadu Yesu arudi. lakini hilo Jiwe la Taifa likae liliko wakitaka waje kulionea hapa hapa lilipo. Hii nayo ni njia ya kuwaleta kwetu na mifedha yao hiyo
 
Nilikuwa natazama channel ten leo kuna prof mmoja aliitaja iyo tanzanite ya thailand yenye kilo 3 ni wazi ss hii ya bwana laizer imevunja ngebe ya thailand .. hao wa merekani tuwaunganishe na zoom waitazame au waifuate huku waione
 
Kabla ya kuruhusiwa kuyachukua, watatakiwa kudeposit amount inayolingana na mawe hayo.. Wacha yaende.. Huenda yaka fetch buyers nchi ikapata hela zaidi.
 
Back
Top Bottom