Kupatwa kwa satellite (satellite eclipse) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupatwa kwa satellite (satellite eclipse)

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by GM7, Sep 18, 2009.

 1. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wana JF wote,

  Mara chache sana tumekuwa tukishuhudia tukio la kupatwa kwa jua (Solar eclipse) na vile vile kupatwa kwa mwezi (Lunnar eclipse).

  Je unafahamu kuwa kuna kupatwa kwa Satellite?

  Napenda kuwajulisha kuwa tukio la kupatwa kwa satellite huwa linatokea wakati jua la utosi linakuwa katika mstari wa Equator (During Equinox). Kwa wale tuliosoma Geography tunakumbuka kuwa jua la utosi hupita katika mstari wa Equator kila tarehe 21 March na 23 September kila mwaka.

  Tukumbuke kuwa Satellite zilizo nyingi zinaelea juu ya mstari wa Equator. Kwa mfano Satellite inayoitwa IntelSat ambayo iko degree 64.5"E inatumiwa na mawasiliano ya Radio na Tv karibu zote hapa Tanzania kama vile ITV, EATV, Star Tv, TBC1, Channel ten, Capital TV. na Radio kama vile RFA, TBC taifa n.k.

  Wakati wa tukio hili la kupatwa kwa satellite Vituo vyote hivi vya Radio na TV hukata kabisa matatangazo yake kwa muda wa dakika kadhaa au saa nzima hasa tunaopata matangazo kwa njia ya satellite dishes hasa hasa mikoani hususan Mbeya.

  Tukio hili naendelea kulishuhudia hivi sasa na mara nyingi hutokea kati ya saa 3:45 asubuhi na saa 5:00 asubuhi. Tukio hili huanza takriban wiki moja kabla ya Equinox. Kwa sasa toka juzi hadi tarehe 28 September kuanzia saa 3:45 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi hvi waweza kushuhudia tukio kwa kuangalia TV na Radio nilizotaja hapo juu.

  Pia ningependa vyombo vya habari hasa TV na Radio kuelimisha wananchi kuhusu tukio hili maana wenyewe huendelea kurusha matangazo wakati wa tukio hili maana hatuwapati kabisaaaa. Je wanafahamu kuhusu tukio hili?

  Sasa tusiandikie mate wakati wino upo. Kesho saa 3:30 asubuhi hebu tushuhudie tukio hili kwa pamoja.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,439
  Likes Received: 22,355
  Trophy Points: 280
  Good advice
   
 3. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tukio hili ndio muda huu liko live, Naona Tv zote za Tanzania tunazoangalia kupitia kwenye madishi muda hazionyeshi kabisa hii pia ni kwa baadhi ya Radio hasa huku mikoani ambazo hupokea matangazo yake kupitia kwenye satellite ya nyuzi 64 mashariki.

  Tutaendelea kushuhudia tukio hili kwa takribani siku tano hivi. Tukio hili hutokea wakati ambapo jua la utosi linakuwa kwenye mstari wa Ikweta yaani MARCH 21 NA SEPTEMBA 23. kwa hiyo siku tatu au nne kabla na baada ya tarehe hizo ndipo utaweza kushuhudia tukio hili kila mwaka. Hutokea kati ya saa 4:00 ashubuhi na saa a 4:30 au saa 5:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.

  Naomba vyombo vyote vya habari viliweke wazi suala hili ambalo naona bado ni geni kwa baadhi ya watu.
   
 4. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Asante kwa habari hiyo.
   
 5. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana mkuu. That why I love JF. Mkuu vipi Canivor pmestaarabika cku hizi?
   
 6. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna pia swali hapa mkuu if dont you mind you may answer as well. Je kuhusu international phone calls vipi? I am trying to call from oversea siwapatai kabisa watu. Je na hili pia lahusika/
   
 7. D

  Dedii Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  ebwanaaee. .. nikweli hadi baadhi ya satelite nyingine zinaathirika, sasa cjui kwa mawacliano ya cmu inakuaje .
   
Loading...