Kupata pasipoti ya kusafiria

Sipo

JF-Expert Member
Jul 25, 2008
2,139
91
Tafadhali naomba kujua gharama, mahitaji, mizunguko (sehemu za kupita) na mahitaji mengine kwenye kufuatilia hadi kupata pasipoti ya nchi yangu Tanzania.
Tafadhali
 
Tafadhali naomba kujua gharama, mahitaji, mizunguko (sehemu za kupita) na mahitaji mengine kwenye kufuatilia hadi kupata pasipoti ya nchi yangu Tanzania.
Tafadhali

Nakushauri nenda uhamiaji hapa hakuna wa kukujibu hilo swali kwani halina staha kwenye hili jamvi. tafadhali hapa paheshimu siyo pahali pake. Au wewe msomali nini? Unaogopa kutiwa mbaroni.Nedna wakusaidie uhamiaji.
 
Tafadhali naomba kujua gharama, mahitaji, mizunguko (sehemu za kupita) na mahitaji mengine kwenye kufuatilia hadi kupata pasipoti ya nchi yangu Tanzania.
Tafadhali

Taratibu za kupata passport zipo wazi kabisa, nenda ofisi ya uhamiaji iliyopo karibu nawe watakupa habari nzima. Inawezekana unajaribu kuulizia njia za panya, kwa nini? Hiyo ni haki yako, kama unakidhi vigezo. Tujaribu pia kufuata utaratibu.
 
Nakushauri nenda uhamiaji hapa hakuna wa kukujibu hilo swali kwani halina staha kwenye hili jamvi. tafadhali hapa paheshimu siyo pahali pake. Au wewe msomali nini? Unaogopa kutiwa mbaroni.Nedna wakusaidie uhamiaji.

Hahaha! msomali atapata siku hiyohiyo we utazungushwa wiki na hata zaidi.
 
Mkuu form ya kuombea pasipoti hii hapa chini,ina maelezo yote unayo yataka .
ADA: - TSh. 50,000/= Au USD 50 (Kwa Walio Nje ya Nchi)
TSh. 10,000/= Malipo Unapochukua Fomu
TSh. 40,000/= Malipo ya Mwisho

View attachment pass_form.pdf
 
nenda kwenye wilaya yako..ulizia hapo forms..ni tsh 10,000 kama malipo ya awali..na elfu 40 utalipa baadae ukishazijaza.
 
Nakushauri nenda uhamiaji hapa hakuna wa kukujibu hilo swali kwani halina staha kwenye hili jamvi. tafadhali hapa paheshimu siyo pahali pake. Au wewe msomali nini? Unaogopa kutiwa mbaroni.Nedna wakusaidie uhamiaji.

Kweli Jamiiforum imeingiliwa na wendawazimu
Hata hivyo nashukuru kwa mchango wako mkuu
 
Mkuu form ya kuombea pasipoti hii hapa chini,ina maelezo yote unayo yataka .
ADA: - TSh. 50,000/= Au USD 50 (Kwa Walio Nje ya Nchi)
TSh. 10,000/= Malipo Unapochukua Fomu
TSh. 40,000/= Malipo ya Mwisho

View attachment 5415

Mkuu Josm
Nakushukuru sana ndugu yangu kwa usaidizi wa hali ya juu ulionipa
Be blessed man
 
Taratibu za kupata passport zipo wazi kabisa, nenda ofisi ya uhamiaji iliyopo karibu nawe watakupa habari nzima. Inawezekana unajaribu kuulizia njia za panya, kwa nini? Hiyo ni haki yako, kama unakidhi vigezo. Tujaribu pia kufuata utaratibu.

Sio lengo langu
 
Kwanza niwashukuru wote ambao wamechangia michango chanya (positive) hapa na kipekee kabisa Josm ambaye ame-attach hadi fomu ambayo kila mtu ambaye bado alikuwa hajafanya hilo zoezi la kupata paspoti aweze kupata the early picture.

Pili niseme kwa mtazamo wangu kuwa mada au matangazo yanayoletwa hapa JF yanasaidia watu mbali mbali kwa wakati fulani na mahala fulani. Na kama mtu akiona yeye hawezi kuchangia hiyo mada asome then aondoke zake, hii tabia ya kuponda post za watu kama alivyofanya mhe. MalyaMungu siyo nzuri kwasababu hapa ni ukumbi wa watu wengi wenye nafasi mbalimbali, capacity mbaimbali na uelewa mbalimbali
Kwa mfano hii post ya kupata paspoti, mimi naamini sijakosea hata kidogo kuiweka hapa na kama nilikosea wapo moderators ambao ni jukumu lao kuiondoa ile ambayo inapingana na maadili ya Kitanzania
Lakini kuna watu wameona umuhimu wake wametoa na muda wao mpaka wameattach documents as reference. Na ukweli husiopingika kuwa sio watu waote wanaotembelea JF tayari wana paspoti, wengi tu watafaidika na michango kutoka hapa

Nashukuru sana
 
Sipo take easy man naona umeumia mno kaka. Ppo tumeumbwa tofauti sana just take easy man na Umsamehe. Thanx for your post maana majibu sahihi yamepatkana nami nimenufaika kwa kujua taratibu.
 
Last edited:
Sipo take easy man naona umeumia mno kaka. Ppo tumeumbwa tofauti sana just take easy man na Umsamehe. Thanx for your post maana majibu sahihi yamepatkana nami nimenufaika kwa kujua taratibu.

Mhe. dmaujanja1
Tumeumbwa kusamehe dunia hii ukikasirika na kuumia kwa sababu ya mtu ni dhambi hata kwa MUNGU aliyekuumba.
Kama umeelimika ndio lengo la JF mhe

tupo pamoja
 
Nakushauri nenda uhamiaji hapa hakuna wa kukujibu hilo swali kwani halina staha kwenye hili jamvi. tafadhali hapa paheshimu siyo pahali pake. Au wewe msomali nini? Unaogopa kutiwa mbaroni.Nedna wakusaidie uhamiaji.
bwa ha ha ha ha JF ina watu imebidi nicheke tu....
 
Na mimi nina shida moja. Natarajia kwenda Moroni Comoro nahitajika kuomba viza kabla au naweza kuchukulia Moroni Comoro niifika. Asanteni.
 
Passpoti ni haki ya mwananchi, lakini usishangae kupigwa maswali kama unataka kwenda wapi au mwaliko uko wapi? Mchezo wa kungojea mpaka mtu apate safari ndio afukuzie passpoti wakati mwingine umechangia kwa kiasi kikubwa njia za mkato kuwa kama ndio official procedure. All the best.
 
Unajua kuna jamaa aliambiwa atoe laki tatu cash achukue pasipoti yake baada ya siku mbili. Na hii sababu pamoja na nyingine ndio iliyonifanya niweke hii mada hapa. Watu wanaibiwa kwa kutojua taratibu na kuchoshwa na ukiritimba uliopo kwenye taratibu hizo lakini mtu akijua taratibu hizi na mahitaji anayotakiwa kuwa nayo atapata kwa haki yake tena kwa muda
Na kama ulivyosema Mndee hii ya kusubiri safari ndio utafute pasipoti ndio inafanya hawa jamaa wa uhamiaji kuneemeka kwa kupinga mapanga ya nguvu kutokana na mhitaji kuwa na haraka
 
Sasa tumeshajua procedure. No more kudanganywa wadau. Ni kiasi tu cha kwenda na elfu 10,unajaza form ukikamilisha vielelezo vyote unarudi na hiyo 40 waliyoandika hapo kwenye form kwishnei! Ila na sisi some times tunajitakia. Mtu anataka afanyiwe kila kitu: hata kujaza form mtu hataki,anataka afanyiwe eti na afisa pale counter. Ndio maana mnapigwa za kichwa kwa uvivu. Akikwambia kiapo cha mahakamani wewe nenda mahakamani kalete, TRA(stamp) nenda kanunue mwenyewe umpe, cheti cha kuzaliwa wahi home kalete(kama kweli unayo)..etc. Hapo rushwa itatoka wapi sasa? Tujitahidi kufuata taratibu tu, tusiwape jamaa vishawishi kwa kuonesha ubwana wa kutaka kufanyiwa kila kitu.
 
Taratibu za kupata passport zipo wazi kabisa, nenda ofisi ya uhamiaji iliyopo karibu nawe watakupa habari nzima. Inawezekana unajaribu kuulizia njia za panya, kwa nini? Hiyo ni haki yako, kama unakidhi vigezo. Tujaribu pia kufuata utaratibu.

What is a problem kama njia za paka zimefungwa?Wewe mjibu unavyoweza, wacha kumsukumia mambo ambayo hakuuliza,unazungumza kama Kingun.....bwana. Acha hizo.
 
Back
Top Bottom