Kupata kitambulisho cha NIDA

Kupata kitambulisho cha NIDA

Kampuni ya kutengeneza vitambulisho walivunja mkataba kwani hawakulipwa fedha zao
 
Zoezi halitakiwi kukoma maana kila siku watu wanatimiza miaka 18
 
Heshma kwenu mabibi na mabwana na WENGINEO. Hivi kama Mtanzania hujawai kujisajiri kupata kitambulisho cha NIDA popote kwa sabab zilizoko juu ya uwezo wako, na zoez lilishakoma mikoan ni nini ufanye kusajiriwa ili kukipata? Je, viambatanisho ni nini ili kuepuka mlolongo?

Aende ofisi za NIDA kwenye wilaya/mkoa wake atapewa taratibu za kukipata
 
Hahahaha mmesha anza kuhaha..

Nenda nida na kopi ya barua ya mtendaji yenye mhuri na picha, na kitambulisho chochote kinachofahamika (leseni cheti cha la 7, cha kura nk) waambie unataka kujisajili..

Utasubiri kuanzia wiki mbili kupata.
Mkuu Wiki mbili tuuu?
Nimepoteza kitambulisho changu cha NIDA, na nimeshalipia kwaajili replacementni, lakini ni zaidi mwezi Sasa nasubiri kupigiwa simu kwenda kuchukua kitambulisho changu.
Kila nikienda wananiambia subiri utapigiwa Simu.
Tatizo nini?
 
Back
Top Bottom