Kupanda kwa madaraja

Nas Mapesa

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
5,271
5,366
Salam kwenu wote,

Wadau hebu niwekeni sawa katika suala la upandaji wa madaraja, hivi mtu anapokuwa masomoni haruhusiwi kupanda daraja?

Na je unapokuwa umepanda unapaswa kurekebishiwa mshahara baada ya muda gani?
 
Aliyeko masomoni naye anaruhusiwa pia kupanda daraja.
Barua utakayopewa ya kupanda daraja ndio itakayoonyesha umepandishwa daraja tangu lini na mshahara utapokea kwa mujibu wa barua hiyo
 
vibali vya masomoni vinasema utaendelea kupata haki zako kama mfanyakazi,
sasa hivi watu wanapanda barua ikija salary ushaizoea, kama barua unayo salary bado ni halmaahauri wazembe fwatilia
 
Hapo ndo kuna maswali mengi maana wilaya ya Temeke nasikia waliopo masomoni hawapandi japo wana ruhusa,sasa naanza kujua huenda ni fitina za wenye ofisi.
 
Hapo ndo kuna maswali mengi maana wilaya ya Temeke nasikia waliopo masomoni hawapandi japo wana ruhusa,sasa naanza kujua huenda ni fitina za wenye ofisi.

nami pia nahisi kuna halmashauri zina fitna kwa maelezo ya ndugu hapo juu
 
Ukiwa masomoni kisheria huwezi kupanda daraja unless afisa elimu na wengineo watumie utu tu...
 
Hapa kuna mawili yanakinzana. Mtu akienda kusoma kwa ruhusa hapotez haki yoyote hivyo lazma apande. Ila sheria za tz upandishwaji madaraja sio ilimradi Una miaka mi3 kazini lazma upande wanaangalia nidhamu na kazi zako. Sasa ukiwa Masomoni watapimaje kaz zako wakat hujaz opras. Lkn ktk utaratibu huu mpya madaraja yanapanda automatic na hazina kwa kuangalia mwaka ulioajiriwa
 
Huwezi kupanda cheo/daraja ukiwa masomoni kwa kuwa utendaji wako hauwezi kupimwa
 
Ukiwa masomoni kisheria huwezi kupanda daraja unless afisa elimu na wengineo watumie utu tu...

sheria ya kazi inasema mfanyakazi akijiendeleza anapata haki zote kama mfanyakazi maana elimu anyoipata ni kwa manufaa ya umma, na barua za ruhusa zimeansikwa hivyo, pia atansing order zimebainisha vyema tu.
 
Msidanganye watu,kama mmeamua kutowapandisha watu kwa utashi wenu au uswahida na wakuu wa mashule imekula kwenu.
mwalimu anapokuwa masomoni yupo kisheria,nakupanda daraja ni haki yake maana karuhusiwa kisheria kama lah angekuwepo kituo cha kazi.
Kama mwalimu alishakanywa kwa maandishi kwa utendaji kazi mbovu bila mafanikio huyo ni haki kutopandishwa,vinginevyo ana haki ya kupanda.
TSD KUWENI MAKINI,MAANA MSIINGIZWE KWENYE FITNA.
 
sheria ya kazi inasema mfanyakazi akijiendeleza anapata haki zote kama mfanyakazi maana elimu anyoipata ni kwa manufaa ya umma, na barua za ruhusa zimeansikwa hivyo, pia atansing order zimebainisha vyema tu.
Habari, naweza kupata sehemu ya kusoma hizo haki. Nina shida nazo.
 
Back
Top Bottom