Kupanda kwa bei ya gesi ya kupikia

Msaranga

JF-Expert Member
Feb 10, 2009
956
227
Jamani mimi nashangaa kupanda kwa bei ya gesi ya kupikia kutoka 37000 mpaka 70000tsh
wakati tunaambiwa hii ni nishati mbadala ya kutunza mazingira badala ya kutumia mkaa au kuni.
Jamani mimi naomba tuchangie mwanzoni tuliambiwa serikali imepunguza kodi kwenye nishati hii ili tuache kukata miti
 
Nchi isha uzwa hii.
Mlala hoi hathaminiwi kabisa.
Wewe ni kijimshahara chako cha kima cha chini ya chini ndio unapiga kelele, wenzako wanalipwa allowance ya gesi na kila mwezi kuna posho kwa ajili ya kununulia vyombo vipya
 
Kwa hili!!!! Kuna umuhimu wa kushuka majiani kwa ajili ya kuonesha hisia zetu. Lazima tuandamane maana wamepandisha gesi kinyemela au gizani.
 
EWURA wapo wapi? Huu upandaji wa bei ya gesi unatia mashaka sana.
 
Jamani mimi nashangaa kupanda kwa bei ya gesi ya kupikia kutoka 37000 mpaka 70000tsh
wakati tunaambiwa hii ni nishati mbadala ya kutunza mazingira badala ya kutumia mkaa au kuni.
Jamani mimi naomba tuchangie mwanzoni tuliambiwa serikali imepunguza kodi kwenye nishati hii ili tuache kukata miti

Sasa hivi kila fursa iliyopo kufanya ufisadi inatumiwa ipasavyo. Watanzania lazima tujifunze kusema hapana this is too much. Kwa nini wananchi wasiandamane kupinga upandaji wa bei ya gas kwa kiwango hicho. Tutakufa jamani.
 
kila kitu kinapanda bei sasa hivi, ningefurahi kama kuna mtu angefanya comparative ya prices wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi na sasa. lakini kipato kinazidi kushuka thamani! watawala wanatumia pesa nyingi kutangazia wananchi uongo kuhusu mauaji ya arusha
 
Sijui JK anasubiri nini maana kama ni hivyo kweli nchi imekwisha mshinda!, Kila kitu bei juu umeme,mafuta,gesi, chakula................... wananchi tuamkeni kupinga udhalimu kama huu maana tunakua kama hatuna serikali! wakati serikali ipo ila inatusahau sisi tulio iweka hapo!
 
Na wale walioyabadilisha magari yao ili yatumie gesi kukwepa gharama za mafuta inakuwaje.
 
na ndio haishuki tena hiyo
si JK alishawapa increament ya kima cha chini?
 
Hilo ni joka la kibisa mkuu!!
EWURA wataonekana kwa kasi ya ajabu ikifika 2014, Vitu vyote bei juu wananchi kaa kimya maana kima cha chini cha mshahara si kimepanda


Inabidi wananchi wakaombe kozi huko Tunisia ndiyo hali itaeleweka lakini kwa hivi ni ndoto
 
The government knows everything behind te whole drama, and it keeps silent coz the deal belongs to one of them dons. All in all the fact is gas is exported silently to Congo. Rwanda and Burundi and fetches a good price kuliko hata hiyo 70,000 unayoiongelea.

Things gonna happen big coz the Donz are closing out their last 5 years and want to make sure they do big. One of them things is fuel, the donz want to control the whole fuel inportation through a certain firm. You will hear soon ar maybe u have heard.

Thats it!
 
Hakuna sababu za msingi za kupanda kwa bei ya gas. Kinachojitokeza hapa na makampuni kufidia gharama zilizotumkia kuchangia kampeni za CCM 2010. Inabidi tuchukue hatua kama za Tunisia!
 
imeonekana mmeachana na matumizi ya Umeme majiko ya Umeme, so wameamua kuwabana kwenye GAS ili mrudi kuwachangia Tanesco ambao wanahaha kupata pesa za kuwalipa Dowans.
 
ndio mnalipia gharama za yale mabango ya kampeni sasa!! nyie mlizani yamekuja bure yale?

kuna watu walitoa hela zao ndio wanazirudisha sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom