Kuota kwa meno siyo chanzo cha tatizo la kuhara kwa watoto

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Ukuaji wa watoto hupitia hatua nyingi tangu kuzaliwa kwao. Mabadiliko haya huhusisha tabia na namna ambavyo mifumo ya mwili hufanya kazi.

Ukuaji wa watoto huwa haufanani, lakini wengi huanza kuota meno wakiwa na umri wa kati ya miezi 4 hadi 7. Tofauti na jinsi ambavyo wazazi wengi huamini, tendo hili la kiasili huwa siyo chanzo cha kuhara kwa mtoto.

Kwa Mujibu wa Taasisi ya National Library of Medicine ya Marekani, Kuhara ni matokeo ya uwepo wa ugonjwa mwingine au uwepo wa mazingira yasiyo salama yanayo mzunguka mtoto kwa wakati huo, hasa yale yenye uchafu.

Ifahamike kuwa wakati huu watoto huwa na hamu ya kula kila kitu pamoja na kusugua fizi zao maana huwasha, hivyo wanaweza kula uchafu wa aina mbalimbali ambao kwa mantiki nyepesi ndiyo huwafanya waanze kuhara.

Dalili za kawaida za kuota kwa meno ni
  • Kuvimba na kulainika kwa fizi
  • Hasira na kulia
  • Kuongezeka kidogo kwa joto la mwili (homa ya kawaida)
  • Kulazimisha kula kila kitu
  • Kikohozi
  • Kusugua fizi
  • Kuweweseka
  • Kung’ata na kuvuta chuchu wakati wa kunyonya
Kuota kwa meno kunaweza pia kusababisha maumivu makali kwa mtoto, lakini hakupaswi kuwa chanzo cha kuhara au kupata homa kali.

Hizi siyo dalili za kawaida, apelekwe hospitalini haraka kwa uchunguzi na matibabu.

Meno mtoto.jpg

Chanzo: National Library of Medicine (NLM)
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri

Nahisi point ilikua hapo kwenye kusugua fizi anaweza kula chochote kikasababisha kuharisha sema wazazi wa kileo hawakujua hilo wao walilibeba lilivyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom