Kuongea uongo ndio uhuru tunao utaka?

MWAKATA KWETU

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
562
319
Imekuwa kawaida kwa raia au wanasiasa kuongea uongo mbele ya kadamnasi au vyombo vya habari.hivi unapozungumza uongo nini maana yake?uhuru wa kupata taarifa unapotumiwa vibaya he nyie WA watu haki za binadamu mbona mnakaa kimya?
 
Kama serikali itaendelea na mtindo huu wa kuficha habari na kufanya mambo gizani lazima na ni muhimu watu wakatafuta njia mbadala wa kupata habari hizo! Kwa kuwa habari hizo zitakuwa zimepatikana kwa mbinde uwezekano wa kuwa sahihi kwa 100% si rahisi lakini zitakuwa na ukweli angalau kwa asilimia kadhaa!

Endapo ukweli huo wa asilimia kadhaa utaikera serikali basi italazimika kutoa habari kamili kama itakavyoona inafaa ingawa kuna uwezekano mkubwa habari yenyewe ikaficha ficha mambo fulani nyeti!

Kwa hiyo mtindo huu ya kudodosa dodosa habari uendelee hadi serikali itakapokuwa inafanya kazi zake kwa haki na uwazi!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom