Katika muendelezo wa kuwabeba mafisadi au kuwa watumwa wa wawekezaji uchwara, Serikali kupitia budget ya 2009/10 wanataka kutoa msamaha wa kodi kwa semi-refined oil hususana ya mawese kutoka nje kama malighafi wakati tunayo alizeti ambayo nyingine huishia mashambani au kuozea kwenye ghala.
Kama huyo mwekezaji anaona mafuta ya mawese ni mali kwanini asilimishe hayo mawese Kigoma na kutoa ajira hapa hapa nyumbani? au ndio hivyo uchaguzi unakaribia hivyo hela ya kukwepa kodi kwenye hiyo raw material ndio mafisadi watakapopitia na kupata mitaji ya kuwekeza kwenye mabenki yao na biashara nyinginezo wakati wananchi wanahitaji hiyo kodi kwa ajili ya zahanati, shule na barabara?