Kuondoa kitambi kwa kutumia Konyagi therapy | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuondoa kitambi kwa kutumia Konyagi therapy

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Bujibuji, Jun 24, 2012.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,219
  Trophy Points: 280
  Jamani mwenzenu badala ya kitambi kupungua ndio kwanza ,inaongezeka, je ni wapi nilipokosea?
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Mmmmhhhhh hii therapy kali bhana
   
 3. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Bujibujiiiiiiiiiiiii za siku?
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  ushakata hicho kitambi?

   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kunywa pingu, ndani ya wiki kitambi chote kwishney
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  konyagi itamaliza maini yako bora uingie gym
   
 7. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Tukishazimaliza pingu, hao pongo wabaki na virungu au?
   
 8. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ongeza kipimo badala ya chupa moja kwa siku bas kunywa mbili
   
 9. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Always short-cut is long-cut. Fuata njia sahihi za kuboresha afya.
   
 10. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Punguzeni kupombeka!
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,219
  Trophy Points: 280
  saa hizi nimetoka kupiga kabinti, njaa kali kinoma
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  he he he, kabinti na kitambi ulimi si unadondoka nje.

   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,219
  Trophy Points: 280
  Ukidondoka, unadakwa kabla haujafika chini, kisha unaingizwa ndani
   
 14. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,462
  Trophy Points: 280
  tafuta nyama choma itapanda vibaya mno.
   
 15. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Coz unakula choma na misupu yenye mafuta!

  Ukitaka ikate kitambi na maini punguza kula.
  As long as utumiaji ni mdogo kuliko uingizaji kitambi is there for stay.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  utakufa bujibuji shauri yako mipombe mikali namna hiyo
  Muone MziziMkavu kwa ushauri nasaha
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Pombe ina magonjwa 60 kwa binadam

  MOJA ya vyanzo vinavyolipatia taifa mapato kupitia makusanyo ya kodi ni pombe.
  Lakini pamoja na faida zote tunazozipata, ukweli unabaki palepale kwamba pombe ina athari katika maisha ya binadamu.

  Mwanzoni mwa mwaka huu wataalamu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na madaktari wastaafu walikutana na wanahabari jijini Dar es Salaam na kuzungumzia juu ya mkutano utakaozungumzia athari za pombe katika jamii.
  Mkutano huo unaotarajia kufanyika Jan 13 hadi 14 mwaka huu mkoani Arusha, utashirikisha nchi za Afrika Mashariki.

  Watunga sheria na wataalamu wengine kutoka serikalini watahudhuria huku ujumbe wa mkutano huo ni: ‘Kilevi si bidhaa ya kawaida na ni kikwazo katika maendeleo.’
  Mkurugenzi Msaidizi na Katibu wa Magonjwa yasiyoambukiza, Dk. Joseph Mbatia, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa

  Jamii anasema serikali ipo mbioni kutengeneza sera itakayohusu utumiaji wa pombe ili kupunguza athari zake katika jamii.

  Dk. Mbatia anasema wamelazimika kutunga sera hizo baada ya kuona matatizo yanayotokana na pombe yanaongezeka kila kukicha.

  Anasema kabla ya sera hizo kupitishwa watafanya utafiti katika maeneo mbalimbali ili kujua ni jinsi gani jamii inavyolichukulia suala la pombe na madhara yake.
  “Mfano, katika vijiji vichache tulivyofanya utafiti, wananchi walikuwa wakijitetea kwamba pombe imewasaidia kuendesha maisha yao…lakini ukweli ni kwamba pamoja na faida ambazo zimekuwa zikiorodheshwa, hasara ni nyingi kuliko faida.

  “Kwa mfano, bima zimekuwa zikilipwa kutokana na ajali zinazosababishwa na kulewa kupita kiasi,” anasema Dk. Mbatia.
  Anabainisha kwamba sera zitakazowekwa si katika kupiga vita biashara ya pombe na badala yake zitakuwa zikiangalia njia bora za matumizi yake na kwa wale wataoonekana wameshaathirika watawekewa utaratibu wa kupatiwa tiba.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Kanda ya Afrika Mashariki ya ‘IOGT-NTO Movement’, ambao ni waandaaji wa mkutano huo, Gunnar Lundstrom, anasema bado kuna changamoto zinazolikabili taifa katika kupunguza athari za pombe.
  Anasema changamoto hizo ni pamoja na pombe kupatikana kwa gharama nafuu na hivyo kusababisha watu kunywa kupindukia.

  Tatizo lingine anasema ni pombe kuwa moja ya chanzo cha mapato nchini, jambo linalofanya serikali kushindwa kupiga marufuku.

  Naye Daktari mstaafu, Maletnlema Tumsifu, anasema kuna jumla ya magonjwa 60 yanayosababishwa na unywaji wa pombe.

  Anataja baadhi ya magonjwa hayo kuwa ni mfarakano katika familia, maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, unene kupita kiasi, utapiamlo hasi, mimba kuharibika na kisukari.

  Dk. Maletnlema anasema kuna madhara ya pombe ya aina mbili. Kwanza ni kuathirika kwaa mishipa ya fahamu mwilini kote kwa kupunguzwa uwezo na pili ni kuungua baadhi ya ogani za mwili hasa tumbo pindi mtu anapokunywa.

  Anaeleza kwamba katika kuathirika mishipa ya fahamu kumetizamwa kwa hatua nne za wanywaji, hatua ya kwanza ni ile ya kuchangamka.

  Hapa mtu hujisikia mzima zaidi ya kawaida, moyo unapiga haraka, tumbo linameng’enya chakula haraka na hamu ya chakula kuongezeka.

  Hatua ya pili, mtu akiendelea kunywa anachanganyikiwa na kuzungumza sana, kukosa aibu, utu kubadilika, kutawala tabia za kimwili, hamu ya chakula kuongezeka na hapa ndipo watu wanaagiza nyama choma kwa wingi.

  Mnywaji akiendelea kunywa pombe hucharuka kutokana na neva zake za ubongo kushindwa kumiliki mwili.
  Mambo yote anayoyafanya hayana utaratibu kwani mnywaji huwa mkorofi.

  Dk. huyo anasema mnywaji huwa mkorofi na anaongea maneno yasiyo na maana, baadhi ya wanywaji huchukulia hatua hii kama raha yao. Hapa kitu kinachojitokeza ni kupoteza hamu ya kula.

  Hatua ya nne mtu akilewa kupita kiasi huwa hajijui na analala fofofo kutokana na kupoteza fahamu. Huenda akajikojolea au kutapika, inategemea na kiasi cha pombe alichokunywa.
  Wakati kwa upande wa ogani, pombe huathiri zaidi viungo vinavyopata pombe nyingi kila wakati mtu akiwa anakunywa.

  Mfano wa viungo hivyo ni mdomo, koo na tumbo, ambavyo vyenyewe hufikiwa na pombe nyingi mara mtu anapomeza.
  Tumbo likiumia inaonekana kama maumivu ya tumbo, pengine kutapika na kuharisha. Lakini kutokana na utaratibu wa tumboni, lazima chakula chote pamoja na sumu au madawa vinavyonyonywa tumboni vipitie katika ini kuondoa sumu na vyakula visivyohitajika.

  Na kwa sababu hii, pombe yote mtu anayokunywa hupita katika seli za ini na zinajaribu kuiondoa lakini nazo zinalewa chakari na baadhi zina kufa.

  Ieleweke kwamba tukinywa kidogo seli chache zinakufa na tukinywa sana zinakufa seli nyingi na nafasi yake inajazwa nyuzi nyuzi za kovu. Ini huwa na mabilioni ya seli ambazo ni imara, hata mtu akinywa pombe nusu, seli zake bado zitaendelea na maisha kama inafikia kikomo ini linashindwa kufanya kazi na kujikuta njia za nyongo na mishipa ya damu inaziba. Kila ogani ya mwili inaumia kivyake, lakini tumbo na ini ni mifano wazi. Bujibuji.. FirstLady1
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  hebu nishaurini,mi sina kitambi ila nafanya mazoezi ya kutengeneza six park,mbona sioni mabadiliko kabisa
   
Loading...