Kuomba msamaha unapokosea kwenye mapenzi

AmbaB

Member
Joined
Sep 1, 2016
Posts
51
Reaction score
27
UNACHUKUA HATUA GANI UNAPOMKOSEA MPENZI WAKO?

Kwenye maisha hakuna binadamu mkamilifu, kila mtu anamadhaifu yake, madhaifu haya ndiyo husababisha watu kutofautiana, kukoseana.. Unafanya nini mara baada ya kuona mwenzio hajaridhika, umekosea na umemkosea?

Nadhani ni vema kuomba msamaha, hapa naongea na wanaume, kwa mwanamke ni rahisi kuomba msamaha lakini ni aghalabu sana kwa wanaume kufanya hivyo, nadhani panahaja ya kukumbushana, wala si dhambi, baba omba msamaha umkoseapo mwenza wako.

Kuomba msamaha ni ibada tosha, ni hekima na ni jambo la heshima kwa mkeo, ni kumpa heshima mwenza wako nafsini, hata Mungu anakubariki uombae msamaha. Ni rahisi sana, tamka "nisamehe".

Ukishaomba msamaha, mzigo unabaki kwa muombwa, unabaki kwa uliyemuomba, aruhusu wepesi moyoni mwake ama la, na hakika anapokusamehe yeye pia hupata Thawabu mbele ya Mungu, "Yatupasa kusamehe". Samehe bila kuhesabu ni mara ngapi umekosewa, utabarikiwa sana.

Nakusihi kijana, Baba, usiruhusu mwenza wako achukie bila kumtaka radhi, haijalishi ni namna gani ulihusika kwenye tukio, omba msamaha, tafuta amani, ni upendo huu.

Sawa umetengana na mkeo, ulichukua hatua gani kabla ya mwenza wako hajakuzira na kughadhabika moja kwa moja? Ulifanya jitihada gani kunusuru uhusiano wenu? Hukutaka hata kuomba radhi? Heshima yake iko wapi!!?

Akiondoka na ihali ulijishusha ,ukampandisha yeye kwa kumuomba msamaha, kila kitu utakiacha mikononi mwake, akusamehe ama akache, ni juu yake, wajibika kwa kuomba msamaha, nusuru penzi lako kwa kuomba msamaha kwa mwenza wako.

Utaoa mara ngapi, utabadirisha mara ngapi? Jifunze kuendeleza uhusiano wako, jifunze kuwa mwanaume kamili bila kuendekeza kiburi ama dharau kwa mwenza wako, ndoa ni Baraka !

Umeombwa msamaha, bado unajawa na kiburi, chuki, wala hutaki kumpa nafasi mwenza wako! Unataka afanye nini kunusuru uhusiano wenu? Haipaswi kuhesabu idadi ya misamaha, hata wazaz wetu walipitia njia hizi ndefu, na ndiyo maana wapo pamoja mpaka sasa! Ukiombwa msamaha ruhusu nafsi yako ipumue, samehe.

Unakataa kutoa msamaha na kukatisha uhusiano ! Kwa kosa la namna gani!? Utampata wapi huyo unayemwita ni mkamilifu ? Zaidi utaishia kubadirisha vitanda na nyumba ! Nakukumbusha kutoa msamaha....

Unajua maana ya mwenzio kukuomba msamaha? Akikuomba, ukakengeuka, naye atageuka, atateseka na mwisho wa siku atazoea na huwezi kuja kupata nafasi tena moyoni mwake, tusamehane.

Tuombane msamaha, tutoe msamaha, tusamehane saba mara sabini.

Na;
Ambangile, B
Instagram, ambangile_b
 
Maelezo yote haya unatusihi namna kuomba msamaha wanawake. Sawa bwana. Ni ngumu saana kusema nisamehe....!

komesha korona
 
Binafsi nilikua mwepesi sana wa kumuomba msamaha mpenzi wangu hasa pale nilipokua na uhakika kwamba mimi ndie niliesababisha tafrani na wakati mwingine hataka kama kosa sio langu nilijishusha ili tu maisha yaendelee kama kawaida....kuna wakati nilikua siwezi pitisha wiki bila ya kumsemesha mwenzi wangu pindi tunapikua tumekosana.....nadhani mwenzangu alikariri vibaya na aakachukulia kama mimi dhaifu sana...baada ya kuona hivyo nikasema sasa ngoja nimuoneshe huyu mwanamke kwamba mimi ni mwanaume kamili na nina misimamo yangu....ilifika wakati nikawa naweza kukaa hata mwezi mzima bila kumcheki na maisha yakawa yanaenda kama kawaida....yeye ndio akawa anahangaika kunitafuta baada ya kuona kimya kingi kila tunapokosana

Nihitimishe tu kwa kusema kwamba, tunapokua kwenye mahusiano tuache mambo ya kutingishiana kiberiti mana hujui ni siku gani mwenzi wako atakua amechoka kabisa vituko vyako hata kama anakupenda kiasi gani.
 
Ntakusamehe....lakini usiichukulie hiyo kama weakness yangu na kuanza kunipiga kwenye huo mshono...I won't accept.
 
Nikikosewa nakubali kigumu msamaha, nikikosea napambana kulifanya kosa liwe dogo kabla sijaomba msamaha inanisaidia.
 
Binafsi nilikua mwepesi sana wa kumuomba msamaha mpenzi wangu hasa pale nilipokua na uhakika kwamba mimi ndie niliesababisha tafrani na wakati mwingine hataka kama kosa sio langu nilijishusha ili tu maisha yaendelee kama kawaida....kuna wakati nilikua siwezi pitisha wiki bila ya kumsemesha mwenzi wangu pindi tunapikua tumekosana.....nadhani mwenzangu alikariri vibaya na aakachukulia kama mimi dhaifu sana...baada ya kuona hivyo nikasema sasa ngoja nimuoneshe huyu mwanamke kwamba mimi ni mwanaume kamili na nina misimamo yangu....ilifika wakati nikawa naweza kukaa hata mwezi mzima bila kumcheki na maisha yakawa yanaenda kama kawaida....yeye ndio akawa anahangaika kunitafuta baada ya kuona kimya kingi kila tunapokosana

Nihitimishe tu kwa kusema kwamba, tunapokua kwenye mahusiano tuache mambo ya kutingishiana kiberiti mana hujui ni siku gani mwenzi wako atakua amechoka kabisa vituko vyako hata kama anakupenda kiasi gani.
Ahsante sana mkuu, bonge moja la ushuhuda na ushauri kwa vijana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaa Mafundi ninyi, wazee wa kuandaa script

Sent using Jamii Forums mobile app
Eeeh kabla ya kumeza unatakiwa kwanza utafune, yani ni full movie Naanda conversation mwenyewe,
Akiniuliza hivi namjibu hivi tena kwa upole nimetulia macho makavu mpaka mwenyewe anakubali kwamba imetokea kwa bahati mbaya au kasingiziwa.
😂😂😂
 
UNACHUKUA HATUA GANI UNAPOMKOSEA MPENZI WAKO?

Kwenye maisha hakuna binadamu mkamilifu, kila mtu anamadhaifu yake, madhaifu haya ndiyo husababisha watu kutofautiana, kukoseana.. Unafanya nini mara baada ya kuona mwenzio hajaridhika, umekosea na umemkosea?

Nadhani ni vema kuomba msamaha, hapa naongea na wanaume, kwa mwanamke ni rahisi kuomba msamaha lakini ni aghalabu sana kwa wanaume kufanya hivyo, nadhani panahaja ya kukumbushana, wala si dhambi, baba omba msamaha umkoseapo mwenza wako.

Kuomba msamaha ni ibada tosha, ni hekima na ni jambo la heshima kwa mkeo, ni kumpa heshima mwenza wako nafsini, hata Mungu anakubariki uombae msamaha. Ni rahisi sana, tamka "nisamehe".

Ukishaomba msamaha, mzigo unabaki kwa muombwa, unabaki kwa uliyemuomba, aruhusu wepesi moyoni mwake ama la, na hakika anapokusamehe yeye pia hupata Thawabu mbele ya Mungu, "Yatupasa kusamehe". Samehe bila kuhesabu ni mara ngapi umekosewa, utabarikiwa sana.

Nakusihi kijana, Baba, usiruhusu mwenza wako achukie bila kumtaka radhi, haijalishi ni namna gani ulihusika kwenye tukio, omba msamaha, tafuta amani, ni upendo huu.

Sawa umetengana na mkeo, ulichukua hatua gani kabla ya mwenza wako hajakuzira na kughadhabika moja kwa moja? Ulifanya jitihada gani kunusuru uhusiano wenu? Hukutaka hata kuomba radhi? Heshima yake iko wapi!!?

Akiondoka na ihali ulijishusha ,ukampandisha yeye kwa kumuomba msamaha, kila kitu utakiacha mikononi mwake, akusamehe ama akache, ni juu yake, wajibika kwa kuomba msamaha, nusuru penzi lako kwa kuomba msamaha kwa mwenza wako.

Utaoa mara ngapi, utabadirisha mara ngapi? Jifunze kuendeleza uhusiano wako, jifunze kuwa mwanaume kamili bila kuendekeza kiburi ama dharau kwa mwenza wako, ndoa ni Baraka !

Umeombwa msamaha, bado unajawa na kiburi, chuki, wala hutaki kumpa nafasi mwenza wako! Unataka afanye nini kunusuru uhusiano wenu? Haipaswi kuhesabu idadi ya misamaha, hata wazaz wetu walipitia njia hizi ndefu, na ndiyo maana wapo pamoja mpaka sasa! Ukiombwa msamaha ruhusu nafsi yako ipumue, samehe.

Unakataa kutoa msamaha na kukatisha uhusiano ! Kwa kosa la namna gani!? Utampata wapi huyo unayemwita ni mkamilifu ? Zaidi utaishia kubadirisha vitanda na nyumba ! Nakukumbusha kutoa msamaha....

Unajua maana ya mwenzio kukuomba msamaha? Akikuomba, ukakengeuka, naye atageuka, atateseka na mwisho wa siku atazoea na huwezi kuja kupata nafasi tena moyoni mwake, tusamehane.

Tuombane msamaha, tutoe msamaha, tusamehane saba mara sabini.

Na;
Ambangile, B
Instagram, ambangile_b
Unachozungumza kiko sahihi sana ila kuna wakati msamaha huleta jeuri na kibuli .

Mimi kuna manzi flani niliwahi kudate nae kila ninapokesea huwa namwomba msamaha tunayamaliza sasa kuna kipindi kipindi manzi alifikia hatua alinipanda kichwani jambo dogo alikuwa anaongea sana visa vikawa vingi vituko vya kila aina

Sasa kuna siku tulipishana kauli akanifokea sana kuepusha mengi nikamwomba msamaha ila baada ya hapo alinijua Mimi ni nani visa nilivyomfanyia ndani ya nyumba alikaaa mwenyewe chini na kuniomba msamaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nilikua mwepesi sana wa kumuomba msamaha mpenzi wangu hasa pale nilipokua na uhakika kwamba mimi ndie niliesababisha tafrani na wakati mwingine hataka kama kosa sio langu nilijishusha ili tu maisha yaendelee kama kawaida....kuna wakati nilikua siwezi pitisha wiki bila ya kumsemesha mwenzi wangu pindi tunapikua tumekosana.....nadhani mwenzangu alikariri vibaya na aakachukulia kama mimi dhaifu sana...baada ya kuona hivyo nikasema sasa ngoja nimuoneshe huyu mwanamke kwamba mimi ni mwanaume kamili na nina misimamo yangu....ilifika wakati nikawa naweza kukaa hata mwezi mzima bila kumcheki na maisha yakawa yanaenda kama kawaida....yeye ndio akawa anahangaika kunitafuta baada ya kuona kimya kingi kila tunapokosana

Nihitimishe tu kwa kusema kwamba, tunapokua kwenye mahusiano tuache mambo ya kutingishiana kiberiti mana hujui ni siku gani mwenzi wako atakua amechoka kabisa vituko vyako hata kama anakupenda kiasi gani.
sure !
 
Huwa natumia maneno mengine lakini sio samahani directly
 
Mwanaume huwa hakosei....anapitiwa tu na wanawake hili wanalijua.
Yah for sure uwa tuna teleza tuu bro atuombi msamaha mana atukosei tuna teleza tuu mm nyumbani kwangu ninmkoloni haswa kwa mke wangu......nikimkosea simuombi msamaha....Mimi kwetu Tarime Mura mkurya wa tarime utaniambia nini Mura......

121.
 
Back
Top Bottom