Ngoja nijibu kama alivyouliza mtoa mada (kwa upande wangu lakini):-
1. Uoaji wa aina hiyo bado unaendelea, ila kwa baadhi ya watu na makabila..mimi binafsi nimeshuhudia Kilimanjaro na Tanga
2. Mtazamo wangu juu ya uoaji/uolewaji wa namna hiyo ni kwamba Una faida zake. Wanandoa huishi kwa amani, furaha na mshikamano..Huwa wamefunzwa vya kutosha na hujua majukumu yao katika ndoa. Mara nyingi ndoa hizi hudumu ukilinganisha na hizi ndoa za 'kukutana pasi na kuchunguzana kwa kina'.
3. Kwa upande wangu nikitaka kuoa kwa haraka lazima niwe na network na yule kijana wa kike awe na network yake ili linapokuja suala la kuchunguzana kuwe na uwazi..Japokuwa inashauriwa 'Usioe haraka' au 'Oa kwa sababu fulani ameoa'. Ndoa siyo jambo la kukurupuka, yahitaji kujipanga kwa kiasi chake.
4. Ni kweli kabisa kuna mabadiliko makubwa katika jamii ya leo, sasa linapokuja suala la kuoa..network anazotakiwa kuwa nazo kijana ni zile za Wazee wa makamo, wazazi wake, ndugu zake na wanajamii wanaomzunguka..Nasema hivi kwa sababu hao niliowataja ndio wanatoa taarifa zako kama una maadili mema au laa! Network za kuchunguza kwa ajili ya ndoa zina umuhimu wake pale tu malengo yaliyopangwa yakatimia na si kuparanganisha wawili wapendanao.
Pia, network hizi kwa kiasi fulani husaidia kusuluhisha pale migogoro ya ndoa inapotokea, hujaribu kushauri kadiri wawezavyo ili kuweka mambo sawa ili ndoa iwe ya amani