Kuolewa/kuoa kwa network

yugoslav

Member
Joined
Mar 17, 2017
Posts
93
Reaction score
72
Habarini wa JF!
Kwa vijana wa zamani, nadhani mtakuwa mnakumbuka jinsi mila zetu za Kiafrika zilivyokuwa, kwa kijana hasa wakiume akitaka kuoa enzi hizo. Kwa ninavyokumbuka kwa makabila yaliyo mengi (Wajita, Wanyamwezi, Wasukuma) kuoa kwa kijana ilikuwa mpaka familia ya muoaji imejiridhisha vya kutosha juu ya mwenendo wa msichana na familia yake, tabia za ukoo ule ikiwemo na maradhi ya kuridhishana n.k. Hii ilikuwa na faida kubwa sana ktk ndoa hizo. Kiukweli ndoa za namna ile zilidumu sana.

Mara nyingi uchunguzi wa muoaji ulifanywa na ndugu/mtu wa karibu na kijana husika paspo familia/ukoo pamoja na msichana kujua kuwa anachunguzwa juu ya mienendo yake. Uoaji wa namna hii uoaji wa network (chunguza kwanza, jiridhishe na oa/olewa).

Kwa mkitadha huo, mimi napenda kufahamu kwa uzoefu
1. Je uoaji wa network bado unaendelea na kama ndiyo, ni wapi?
2. Je upi mtazamo wako juu ya uoaji / uolewaji wa namna hii?
3. Je ukitaka kuoa/kuolewa haraka lazima kijana wa kiume/kike awe na network?
4. Kwa mabadiko ya kijamii tuliyonayo leo, ndugu walio wengi hatujuani. Je kijana akitaka kuwa na network juu ya jambo hili, zipi ni network wanazoweza kuzitumia vijana kujipatia wenza wao?

Karibuni kwa michango yenu.
 
Ata sielewi! [emoji53][emoji53][emoji53]
 
Ngoja nijibu kama alivyouliza mtoa mada (kwa upande wangu lakini):-

1. Uoaji wa aina hiyo bado unaendelea, ila kwa baadhi ya watu na makabila..mimi binafsi nimeshuhudia Kilimanjaro na Tanga

2. Mtazamo wangu juu ya uoaji/uolewaji wa namna hiyo ni kwamba Una faida zake. Wanandoa huishi kwa amani, furaha na mshikamano..Huwa wamefunzwa vya kutosha na hujua majukumu yao katika ndoa. Mara nyingi ndoa hizi hudumu ukilinganisha na hizi ndoa za 'kukutana pasi na kuchunguzana kwa kina'.

3. Kwa upande wangu nikitaka kuoa kwa haraka lazima niwe na network na yule kijana wa kike awe na network yake ili linapokuja suala la kuchunguzana kuwe na uwazi..Japokuwa inashauriwa 'Usioe haraka' au 'Oa kwa sababu fulani ameoa'. Ndoa siyo jambo la kukurupuka, yahitaji kujipanga kwa kiasi chake.

4. Ni kweli kabisa kuna mabadiliko makubwa katika jamii ya leo, sasa linapokuja suala la kuoa..network anazotakiwa kuwa nazo kijana ni zile za Wazee wa makamo, wazazi wake, ndugu zake na wanajamii wanaomzunguka..Nasema hivi kwa sababu hao niliowataja ndio wanatoa taarifa zako kama una maadili mema au laa! Network za kuchunguza kwa ajili ya ndoa zina umuhimu wake pale tu malengo yaliyopangwa yakatimia na si kuparanganisha wawili wapendanao.

Pia, network hizi kwa kiasi fulani husaidia kusuluhisha pale migogoro ya ndoa inapotokea, hujaribu kushauri kadiri wawezavyo ili kuweka mambo sawa ili ndoa iwe ya amani na furaha.



Mtoa mada/uzi sijui nimekujibu ipasavyo???

[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
 
Sasa hivi tunaoa kwa network ya badoo,facebook,whatsapp na Jamii forum!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…