Kuogopa kula chakula hadharani kwa kuwa watu wengine wamefunga ni kukosa uhuru wa kuabudu

African Believer

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
436
425
Kumekuwa na kasumba ya baadhi ya watu waliofunga kuwakosoa wale wa imani nyingine pale wanapokula chakula mchana ilhali wao wakiwa kwenye funga.

Ijulikane kuwa, funga ni jambo la kiimani na si ugonjwa, hivyo aliyefunga apaswa kutambua kuwa hilo ni jukumu lake kulingana na maagizo ya dini yake.

Kwa sababu hiyo, kwenye nchi yenye uhuru wa kuabudu kwa watu wenye dini mbalimbali si vyema kumlazimisha mtu wa imani nyingine kufunga ama kutokula hadharani pindi wewe unapokua umefunga.

Naomba kuwasilisha.
 
Nimeona Zanzibar wamepiga marufuku kula mchana au kuuza chakula mchana.

Huu ni utumwa na ujinga wa kiwango cha juu sana.

Wewe kufunga na mimi kula wapi na wapi?

Mimi kula kwangu naingiliaje maombi yako kwa Mungu wako?

Yani nadhiri yako na Mungu wako unipe shida mimi nisile.
 
ndugu kuna mtu amekuzuia kula? mfano mdogo tu hapa nilipo ni mimi tu ndio nimefunga wenzangu wanapiga kuku mbele yangu na mimi nipo tu busy na kazi zangu wala sioni cha ajabu na wala sikereki, nasubiri alasir niingie zangu masjid....kawaida tu
Mimi nahisi hiyo ndiyo funga halisi, kwani suala la funga ni manuizi kati ya muumini na Mungu wake.
 
Kumekua na kasumba ya baadhi ya watu waliofunga kuwakosoa wale wa imani nyingine pale wanapokula chakula mchana ilhali wao wakiwa kwenye funga.

Ijulikane kuwa, funga ni jambo la kiimani na si ugonjwa, hivyo aliyefunga apaswa kutambua kuwa hilo ni jukumu lake kulingana na maagizo ya dini yake.

Kwa sababu hiyo, kwenye nchi yenye uhuru wa kuabudu kwa watu wenye dini mbalimbali si vyema kumlazimisha mtu wa imani nyingine kufunga ama kutokula hadharani pindi wewe unapokua umefunga.

Naomba kuwasilisha.
Kero ni pale wa imani hiyo wanapokuwa wengi eneo hilo.Maeneo walipo wachache msosi unaliwa mchana hadharani na mtu anayekula habughudhiwi.Migahawa iko wazi mchana kutwa
 
Kumekuwa na kasumba ya baadhi ya watu waliofunga kuwakosoa wale wa imani nyingine pale wanapokula chakula mchana ilhali wao wakiwa kwenye funga.

Ijulikane kuwa, funga ni jambo la kiimani na si ugonjwa, hivyo aliyefunga apaswa kutambua kuwa hilo ni jukumu lake kulingana na maagizo ya dini yake.

Kwa sababu hiyo, kwenye nchi yenye uhuru wa kuabudu kwa watu wenye dini mbalimbali si vyema kumlazimisha mtu wa imani nyingine kufunga ama kutokula hadharani pindi wewe unapokua umefunga.

Naomba kuwasilisha.
African Belever napenda tueleweshane kitu unahitaji elimu
1. Imani ya kufunga kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani imefaradhishwa kwa sisi waislamu ikiwa ni moja ya nguzo tano za Uislam. Kwa maneno mengine asiye muislam hii halimuhusu japo anatakiwa kuheshimu wanaofunga.
2.Kwa mafundisho yetu ya kiislam,ikiwa muislam ni mgonjwa,mama mjamzito,mwanamke aliye kwenye ada yake ya mwezi na mama anayenyonyesha wana ruksa ya kutokufunga,lakin masharti ni kwamba hawatakiwi kula hadharani.Kwa wale wasio waislam hili pia haliwahusu na pia hata wakila hadharani wasidhani kwamba wanawakwaza waislam.kwa sababu waislam hatufungi kwa sababu ya chakula hilo mkae mkilielewa
3.Waislam hatufungi kwa ajili ya chakula.Kwa wale wenye upeo mdogo wa mawazo wanadhani waislam huwa tunafunga kwa ajili ya chakula na hiyo inadhihirisha jinsi ambavyo hamjui maana na malengo ya mwezi huu mtukufu na ndio maana mnaona raha kupotosha.Kufunga ni suala la imani na kama ni suala la chakula wakati wa kufuturu kila mtu ana maamuzi ya kula kile anachokipenda ili mradi ni halali.

USHAURI KWAKO
Unapotaka kufahamu masuala ya Uislam uliza ujibiwe sio kupenda kupotosha wakati elimu yenyewe kuhusu jambo husika huna.
 
Zanzibar ni kisiwa chenye wakristo na waislam pia, sasa agizo la kukataza watu kuuza na kununua msosi naona kama wanataka kuleta chuki na matabaka (udini) kati ya waislam na wakristo, kwani haijawa nchi inayotawaliwa na utawala wa kidini kama mataifa mengine ya kiarabu...au ndio mwanzo wa alama ya mnyama(666)
 
Back
Top Bottom