Kuogelea kusingekuponya ajali ya MV Nyerere

Dawa ni kuvaa ma life jacket tu aisee, poleni kwa majanga
Kwa jinsi wabongo tulivyo sidhani kama hizo life jacket zinatolewa kwa kila abiria.
Hebu angalia hapo ferry, siku moja itokee kivuko kimezima, au kubinuka katikati ya maji ndipo utasikia wanasisitiza life jacket.
 
Tatizo hawa wasimamizi wa vyombo vya baharini wana akili ya ajabu sana unakuta zile life jackets zimefungiwa sehemu kwa kufuli sasa hata kama ajali imetokea hapo mtu ataponaje? Serikali lazima ilaumiwe kwa ajali hii
 
Asante sana mkuu kwa mada nzuri. Kuna watu wanaongea kama vile sijui nini eti kwanini wameshindwa kuogelea yani I can feel jinsi walivyokuwa wanajitahidi kuokoa maisha yao lakini mtu anakuja kubeza hapa.
 
🇮 🇳 🇦 🇹 🇮 🇸 🇭 🇦 🇸 🇦 🇳 🇦 .
 
Mimi kinachonishangaza inakuwaje umbali wa mita zisizozidi mia wafe watu wengi kiasi hicho
Kwa stahili hii yakupinduka inawezekana kabisa mkuu ukiongezea na maandalizi ya serikali yetu dhidi ya maafa haya
 
Serikali ikiweka malife jacket kwenye vivuko yataibiwa yooote.... WaTanzania akili zetu tunazijua wenyewe
 
Miaka miwili ilopita kivuko cha MV Kigamboni kiliacha njia na kuanza kuelekea sehemu ingine.



Kichotokea ni mtafaruku na abiria wengi kupatwa na woga na kuanza kutoka kwenye kivuko.

Kivuko hicho kilizidisha mizigo na idadi ya abiria.

Bahati nzuri kivuko hakikuwa mbali sana na nchi kavu na kama unavyomwona Richard nilikuwa wa kwanza kutoka na begi langu nimeliweka panapohuska.

Usiombe kabisa hii hali ikutokee.
 
Hapa umeongea point ila so yule jamaa alie kazana kusema wasukuma wazembe wamekufa hawajui kuogelea
 
Yote uliyoongea yapo tatizo ni utekelezaji wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…