Kuoa kunatisha ni kama unaingia vitani

Kuoa kunatisha ni kama unaingia vitani

Jaslaws

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
6,016
Reaction score
5,301
Nimekuwa nikifanya michakato ya kuoa kwa wiki kama mbili hivi, nimefanya utaratibu wa kwenda kujitambulisha kama mila za kwetu zinavyotuelekeza.

Kwakua mimi Niko Dar na mwanamke ninaetaka kumuoa tunatoka nae mkoa mmoja hivyo mzee wangu ambaye nae yuko mkoa huohuo ndo anachukua jukumu la kwenda kwao na binti kwenda kuwaeleza nia yetu ya kuoa kwao.

Leo ndo ikawa Siku ya kwenda kwao na binti kilichonikatisha tamaa ni Leo asubuhi mzee akiwa kesha jiandaa kwa safari na wazee wenzake alinipigia simu maneno yake ndo yamenikatisha tamaa kabisa japo aliongea kwa utani bila nimebaki natafakari alinambia hivi"interalia hello Jas sisi ndio tumeshajiandaa na safari hapa tunaenda kuuza uhuru wako"aliongea kwa utani.

Ila mpaka sasa bado natafakari nahisi hili zoezi huu ndo utakuwa mwisho wa huu mchakato siendelei tena, uhuru wangu bado nautaka.
 
Ahahaha!wenzio tumeshazoea!for yrs and counting!
uhuru gani unao uzungumzia?
 
Nimekuwa nikifanya michakato ya kuoa kwa wiki kama mbili hivi,nmefanya utaratibu wa kwenda kujitambulisha kama mila za kwetu zinavyotuelekeza...
Kwakua Mimi Niko dar na mwanamke nnae taka kumuoa tunatoka nae mkoa mmoja hivyo mzee wangu ambaye nae yuko mkoa huohuo ndo anachukua jukumu la kwenda kwao na binti kwenda kuwaeleza nia yetu ya kuoa kwao.
Leo ndo ikawa Siku ya kwenda kwao na binti kilichonikatisha tamaa ni Leo asubuhi mzee akiwa kesha jiandaa kwa safari na wazee wenzake alinipigia simu maneno yake ndo yamenikatisha tamaa kabisa japo aliongea kwa utani bila nimebaki natafakari alinambia hivi"interalia.... hello Jas sisi ndio tumeshajiandaa na safari hapa tunaenda kuuza Uhuru wako"aliongea kwa utani
Ila mpaka sasa bado natafakari nahisi hili zoezi huu ndo utakuwa mwisho wa huu mchakato siendelei tena,Uhuru wangu bado nautaka.
Hakumaanisha uhuru wa kuishi kwamba utakuwa jela(hapana).
Mantiki ya maneno hayo ni kwamba tabia za uhuni uhuni sasa inabidi uache na ukifanya maamuzi usijiamulie mwenyewe bali umshirikishe na mke wako
 
Usiogope kaka utani tu, hongera sana kwa hatua hiyo. Nadhani ukweli watakuta mashine ya EFD wakiwa wanatoa mahari, tulipe kodi kwa maendeleo.
 
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa dingi kamchana. safi. uhuru maana yake privacy ya mambo yako hakuna tena. mambo meeeengi sana mnafanya pamoja na mkeo ambaye ni mwili mmoja nawewe. usitishike. ktk kuoa tunaangalia mke mtarajiwa asiwe na tabia hizi mbili 1.mchawi na 2. mzinifu. mambo mengine yooote ni kawaida
 
Hahahhh we ni mwehu nenda kaoe uko uhuru wako atabaki nao mkeo [emoji28]
 
Ndo maana ndoa inaitwa pingu za maisha ni zaidi ya jela
Mkuu vipi wewe ushaingia uko unimegee ni Uhuru UPI hasa unaukosa ili kabisa niandae siraha za maangamizi!?
 
Bora ukosee kujenga nyumba.......
ukioa kimeo unaweza kwenda kukesha bar
nyumba yako inakua kama kituo cha polisi
 
Back
Top Bottom