Kuoa au kuolewa kuna faida gani!!!

Chaku,

Ningependa kukupatia ushuri na labda ushuhuda wa nini kiko kwenye ndoa. Lakini mada yako inaonesha mtazamo hasi kuhusiana na suala la ndoa. Kwa sababu hiyo naweza kukuambia kuwa hata uishi miaka 200 hutaweza kupata majibu ya maswali yako isipokuwa ukifanya uamuzi wa kuingia kwenye ndoa ili uone mwenyewe. Majibu yote utakayopata hayatakusaidia. Kila ndoa ni unique kwa hiyo kila mtu analo lake. Ila kwangu mimi, kila kitu ninachopata kwenye ndoa ni raha tupu!


Kwa kweli ndugu yangu nashukuru kwa ushauri wako mzuri sana nami napenda sana maisha ya ndoa kama yakiwa nitakavyo lakini ni haya mambo ambayo watu wanapokuwa ndani ya ndoa yanakuwa hayaishi?

Kweli maana ya ndoa ni mikwaruzo ambayo haina msingi?Muingiliano wa familia wakati hao ndo wliokuwa wanashangilia siku ya harusi yenu?
Kweli ndoa inakuwa kama adhabu au ni laana ambayo mtu anakuwa amepewa na mwenyezi mungu?

Mbona mafundisho yote mliyopata kipindi mnajiandaa kuanzia begparty,sendoff na kitchen party yanapotea au ni kuburi cha wanandoa pale inapotokea kuwa hakuna jinsi hata akiniacha au nikimuacha tutagawana kila kitu.

Sasa hayo yote ndo nayoyataka kuyajua siyo kwamba kuuliza kitu nikumbia kuingia la hasha ila nikutaka kujua ili uelimike.

Mimi mfano hai ni kaka yangu ameoa lakini kipindi nasoma Olevel na A leve ni lipata shida kutoka kwa mkewe mpaka leo hii wanazaidi ya miaka kama kumi na lakini huyu mwanamke bado nimshrikina maana yake nini?
 
a. Ndoa inakupa kampani ya kudumu. ndo mana ndoa inaitwa "pingu". Inakupa haki fulani ambazo lazima upewe na mwenzako, mf. haki ya tendo la ndoa, kutunzwa, nk . Nje ya ndoa hata kama utapewa mambo haya huwezi kuyavalisha sifa ya "haki". Kumbe kwenye ndoa unakuwa na uhakika wa kupata haki zako kutoka kwa mwenzako. Na asipokupa ana hatia, unaweza kumshitaki mahakamani, nk

b. Faida nyingine ya ndoa ni matunzo/malezi ya watoto. Malezi haya yanakuwa kamili yanapofanywa na wazazi wote wawili wakiwa pamoja kama mume na mke. Mtoto anafaidi katika malezi umama na ubaba wa wazazi wake. Anakuwa balanced. Akilelewa na mzazi mmoja anakuwa na tendency zinazoegemea zaidi jinsi iliyomlea. Anakosa attitude/feelings za mzazi wa pili ambaye yuko mbali na kazi yake yeye ni kutuma matumizi tu. Matumizi tu haitoshi. Mtoto anataka uwepo wako. Afaidi kutoka kwako kwa maneno yako, appearance, feelings, na concrete care.

c. Ndoa ina-extend mahusiano. Ni kwa njia ya ndoa tu tunapata kiuhalali mashemeji, wakwe, nk. Bila ndoa hawa huwapati japo watu wanakuwa wanavilazimisha hata katika mahusiano ya GF na BF. Lakini kiuhalali ni kwenye ndoa.

d. Faida nyingine ni urithi: ndoa inakupa haki ya kurithi mali ya mwenzako wa ndoa pale anapokuwa amefariki dunia.


Kwakweli babuyao umeongea ukweli kabisa.

Ila ni kweli haya uliyoyasema yanafahamika kwa wanandoa au ni viburi tu vinavyojitokeza baada ya ndoa?

Mbona haya uliyoyasema ndo ndoto kubwa kabla ya ndoa na mtu anapojicommit inakuwa tofauti?
Au ni akili zetu zinakuwa hazilengi huko ila zinakuwa na malengo mengine ambayo ni vigumu kuyajua kipindi cha uchumba?

Nini kifanyike ili mtu kujua umuhimu wa ndoa kama ujuavyo wewe Babuyao na faida zake?
 
mie hata ckujuaga faida/hasara za ndoa, nilijishtukia nipo ndani ya ndoa, lakini ndoa ina changamoto kibao,kwa upande wangu imenifanya nijione mwanamke kamili, ninae weza kupambana na maisha, imenifundisha mengi na kila kukicha najifunza mengi.
 
mie hata ckujuaga faida/hasara za ndoa, nilijishtukia nipo ndani ya ndoa, lakini ndoa ina changamoto kibao,kwa upande wangu imenifanya nijione mwanamke kamili, ninae weza kupambana na maisha, imenifundisha mengi na kila kukicha najifunza mengi.
aah wapi bana.....sasa mbona kila siku mwalalamika hapa? inaonekana ndoa michosho tu.....
 
aah wapi bana.....sasa mbona kila siku mwalalamika hapa? inaonekana ndoa michosho tu.....


malalamiko/mikwaruzano/malumbano/raha/shida na mataatizo ktk ndoa ndio changamoto/mafunzo yenyewe sasa...na ndio yananifanya nakuwa jacri zaidi zaid....
 
Hakika mimi ngependa kuzungumzia kisheria zaidi suala hili la ndoa. Kwani kuna kasi nyingi sana zinazotokana na product zanazopatikana za watu kufanya mahusiano bila kuoana.

Kuna haki za kimsingi za MTOTO ambazo hata sheria za Tanzania zinazitambua (Sura ya 13 katiba ya Tanzania) na vile vile nikipembua Haki za Mtoto za kiislamu zinaanzia pale penye 1.nasaba ( Yaani mtoto kuwa na haki kisharia kutumia jina la Ubini wa baba Yake , 2.kuadhiniwa na kukimiwa 3. kufaniwa hakika, kupewa jina zuri etc.

sasa all in all, suala la kuoana ni muhimu sana katika mustakabali ya product ambazo Muumba atakazo wajaalia.

Nasriyah Saleh Al-Nahdi.
Doha
 
Kuoa na kuolewa kunafaida kuu moja:

Sababu ya 1

Kujenga maisha ya familia bora kwa makuzi bora ya watoto yenye lengo la kujenga jamii bora yenye makuzi ya kimaadili kwa jamii.

Jamii zikikosa ndoa imara itakuwa na wimbi kubwa la watoto wa mitaani wasio na malezi bora na ni chanzo cha jamii iliyo potoka isiyo na amani, elimu na maisha bora.

Mpango wa Mungu ni kwa mwanadamu kuishi katika familia bora na imara. hapo ndipo mwanadamu atapata mafunzo halisia ya kuishi kwa upendo na atajifunza kupenda wengine.

Ndoa hazidumu kwasababu ya Mwovu Shetani:

Yeye anajua familia bora ni chimbuko la watu wenye misingi bora kiroho. Hivyo huzipiga familia nyingi pigo kuu la utengano ili jamii ipate watoto wasio na malezi bora na kuweka jamii yenye hatari na kila aina ya uovu maana ni jamii inayotoa watoto wasio na malezi bora ambao hawajui hata kutoa na kupokea upendo.
 
Katika jamii nyingi duniani wanasema ukiwa huja owa au kuolewa basi bado hujatimia provided u-mzima wa afya, Kwa wengine wanasema ndoa ni kua na "Legality of ownership" ama ya mume au mke.And then the legality of what you produced between you and your partner.
Kuna baadhi ya wazungu nilishawahi ku-argue (kubishana) nao na mwisho wakaniambia kua " The meaning of marriage is a Legal Prositution'' nikamuuliza why do you think so? akanijibu kua when I feel to have sex I just go and pay, have a short, now if I want her for a long time or for life then I just go and pay lump sum and have a legal papers and I owned her, so what the difference here ?. Obviously I told him this doesn't apply in our community.
Tukiangalia dunia ya sasa, hapo ndio utaona kua na mke/wake au mume you are more safe then hanging/changing around with anyone you find atrractive day by day. Hii niliotouch hapa ni just social talk na mambo yalivyo mitaani, lakini ukija kwa upande wa dini zetu hivi mbili (Islam & Christianity) zimemaliza mjadala bili ya wasiwasi.
 
Ndoa ni muhimu kwani ina raha nyingi na faida zake ni lukuki kama kupata mwenza ambaye utakuwa naye na kuja kutengana naye kwa talaka au kifo. Lakini, ndoa inadumisha familia yaani mahusiano ya baba na mama kwa watoto wao na kama walivyosema wachangiaji wengine hapo juu ..watu waliopo kwenye ndoa huishi umri mrefu kwa tafsiri ya kilugha au kisheria.!
 
Back
Top Bottom