Kuoa au kuolewa kuna faida gani!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuoa au kuolewa kuna faida gani!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Unazo!, Aug 3, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,793
  Likes Received: 2,459
  Trophy Points: 280
  Wakuu kukicha kuna matatizo yanayotokana na maamuzi ya kuolewa au kuoa.
  Hivi kunafaida gani ya kuoa au kuolewa?ni kwa ajili ya kutimiza agano maandiko ya mungu?
  Au twaowana kwa ajili ya kupata watoto?Ila hili si sahihi kwa kuwa kuna watoto wanaopatikana hata nje ya ndoa?

  Au ni kwa sababu ya kulinda imani na desturi za mababu na wazazi wetu?

  Ni hasa faida ya haya maamuzi?
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Hapo naona ni suala la kulinda status kwenye jamii zaidi, vinginevyo kwa dunia ya sasa jinsi ilivyooza watu wengi wasingekubali kufunga ndoa.

  Ya nini kufunga ndoa na mtu ilhali historia inaonesha alishawahi kuwa na mabwana zaidi ya 10? si ni mambo ya kula makombo hapo? Halafu mtu unatembea barabarani kifua mbele kwamba una mke kumbe wakati huo huo kuna mtu tayari keshakuzunguka.

  Mmmmm!
   
 3. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,793
  Likes Received: 2,459
  Trophy Points: 280
  na hapohapo inawezekana bado wananendelea na mahusianao yao.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Aug 3, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ndoa ni mpango wa Mungu na kama mtu hutaki kuoa/kuolewa usilazimishe kufanya mapenzi nje ya ndoa ambapo ni kutenda dhambi mbele za Mungu! Adhabu ya jehanamu inatisha! Ni jambo la kutisha mtu kuanguka kwenye mikono ya Mungu aliye hai!
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Aug 3, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  ...... mh watu wote wangekuwa wanafikiria kama wewe kweli kusingekuwa na kuoana!! Eti makombo yaani wewe basi tu.

  Ila kwa jinsi ulivyoiweka inaelekea yamekukuta!
   
 6. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  wewe umewazunguka wangapi???? hata wewe pia ni makombo unless uko bikra....
   
 7. I

  Ivilikinge Member

  #7
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani mbona mnanitenga sana sijui hata sehemu kama nataka ni mimi nitoe labda hoja yangu ili tuijadili na nipate mawazo mbadala nielekezeni basi ni wapi?
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wanawake wakiendekeza kuwa na wanaume wengi wanchoka mapema yaani akuwa fouth hand used. Tofauti na wanaume utaona babu ana wanawake 7 lakini anadunda tu bado nyumba ndogo hapo hapo.
   
 9. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  maoni yangu ya sababu zitakazonifanya niolewe.... kwanza for companionship.... pili nataka niwe na watoto ambao watalelewa kwenya familia yenye baba na mama... life is sweet if you share it with your friend!! sitaki kuzeeka mungu akinijaalia niwe mpweke....sina hata wa kunikuna mgongo jamani duh!!!
   
 10. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,793
  Likes Received: 2,459
  Trophy Points: 280
  Good!!

  Hayo yote huwezi kuyapata mpaka uolewe?Kwa ni mpenzi wako hawezi kuwa baba wa mtoto?au hawezi kuwa company yako?
  au mpenzi siyo friend?
  Bado nauliza nini faida ya kuoa au kuolewa? Make kwenye ndo ndo kuna kila aina ya anasa?utasikia siku hizi jamaa anachelewa kurudi nyumbani mara hanipi haki ynagu ya msingi mara anasaidia sana kwao mara hanipendi mara ni mlevi mara ananyumba ndogo mara anamafiga matatu? Yote ndani ya ndoa?
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,471
  Trophy Points: 280
  Ndo kama hivi ulivoweka hoja hapa.
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Faida za kuoa/kuolewa ni tamu tena nyingi kuliko (spinsters na bachelors) mnavyoweza kufikiria...

  Matatizo yanayotawala mazungumzo kwenye jamvi hili ni asilimia kiduuchu tu ya raha tele zilizomo kwenye maisha ya ndoa.

  nitarudi kujadili zaidi....
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mara ana kidumu!! mara wanamtumia, mara hakutaki tena, mara anakuita ATM
   
 14. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  huo wote ni utamu wa ndoa.... nani alikudanganya itakuwa a smooth ride through??? ATM tena kwenye ndoa??? hamna wale nyumba ndogo ndio wanapata ATMs.
   
 15. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Dadangu yangu Chaku, dhambi ndo imeufikisha ulimwengu katika hali mbaya iliyonayo. Mungu alipomuumba Adamu aliona yuko peke yake na mpweke ndo akasema na amfanyie msaidizi wa kusaidiana naye (Mwanzo 2:1. Kwahiyo ndoa ni mpango mtakatifu wa MUNGU kwa wanadamu. Zinaa ni mbaya na ni dhambi inayowatafuna wanadamu wengi duniani kote. Machungu yote yanayoonekana kwenye ndoa ambayo hupelekea hadi talaka ni matokeo ya dhambi na wanadamu kukosa hofu ya MUNGU na wahusika kutotimiza wajibu wao katika ndoa. MUNGU anasema anachukia kuachana (Malaki 2:16).

  Faida za kuoa na kuolewa.

  1. Ni mpango halisi wa MUNGU kwa wanadamu

  2. Kupata mwenza wa kushiriki naye tendo la ndoa kwa halali

  3. Kupata watoto ndani ya ndoa takatifu (kumbuka watoto ni zawadi toka kwa MUNGU unaweza usiwapate, na mshukuru MUNGU kwa hilo pia maana hujui kwanini MUNGU imempendeza iwe hivyo)

  4. Kupata rafiki wa halali kutoka kwa MUNGU wa kushirikiana naye katika mambo mbalimbali ya kimaisha (Mhubiri 4:9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; maana wapata ijara njema kwa kazi yao)

  5. Kukupa status na heshima katika jamii (mfano ubalozi nyingi e.g ubalozi wa Marekani ni rahisi kupata visa ukiwa kwenye ndoa kuliko asiye kwenye ndoa)
  n.k

  NOTE: Wanandoa wakiwa na hofu ya MUNGU na kila mmoja kutimiza wajibu wake, utaiona hii dunia kama paradiso ndogo. Pia ndoa ni sanaa (it is an art) inahitaji vikorombwezo kadhaa kuiboresha na kuifanya mpya kila iitwapo leo. Kusoma Biblia na vitabu mbalimbali husaidia kujua wajibu wa kila mmoja katika ndoa. Zaidi ya yote uwepo wa MUNGU katika ndoa ni muhimu kupita yote.

  Namshukuru MUNGU niko kwenye ndoa miaka 5 sasa na tumejaa furaha tele na mke wangu mpenzi, ua la moyo wangu. I love my queen and she loves me too.
   
  Last edited: Aug 4, 2009
 16. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  a. Ndoa inakupa kampani ya kudumu. ndo mana ndoa inaitwa "pingu". Inakupa haki fulani ambazo lazima upewe na mwenzako, mf. haki ya tendo la ndoa, kutunzwa, nk . Nje ya ndoa hata kama utapewa mambo haya huwezi kuyavalisha sifa ya "haki". Kumbe kwenye ndoa unakuwa na uhakika wa kupata haki zako kutoka kwa mwenzako. Na asipokupa ana hatia, unaweza kumshitaki mahakamani, nk

  b. Faida nyingine ya ndoa ni matunzo/malezi ya watoto. Malezi haya yanakuwa kamili yanapofanywa na wazazi wote wawili wakiwa pamoja kama mume na mke. Mtoto anafaidi katika malezi umama na ubaba wa wazazi wake. Anakuwa balanced. Akilelewa na mzazi mmoja anakuwa na tendency zinazoegemea zaidi jinsi iliyomlea. Anakosa attitude/feelings za mzazi wa pili ambaye yuko mbali na kazi yake yeye ni kutuma matumizi tu. Matumizi tu haitoshi. Mtoto anataka uwepo wako. Afaidi kutoka kwako kwa maneno yako, appearance, feelings, na concrete care.

  c. Ndoa ina-extend mahusiano. Ni kwa njia ya ndoa tu tunapata kiuhalali mashemeji, wakwe, nk. Bila ndoa hawa huwapati japo watu wanakuwa wanavilazimisha hata katika mahusiano ya GF na BF. Lakini kiuhalali ni kwenye ndoa.

  d. Faida nyingine ni urithi: ndoa inakupa haki ya kurithi mali ya mwenzako wa ndoa pale anapokuwa amefariki dunia.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,827
  Trophy Points: 280
  Pamoja na matatizo yaliyomo katika ndoa, bado kwa maoni yangu ndoa ina umuhimu mkubwa katika jamii zetu ukilinganisha na maisha ya ubachelor. Wengi wanautaka ubachelor ili kuendelea kufurahia uhuru wao wa kutoka na kuingia saa wanazotaka na kuwa na mwanamke au mwanaume yoyote yule wanayemtaka bila ya kuulizwa na yeyote yule.

  Maisha haya ya kubadilisha mwanaume au mwanamke kila kukicha nayo yana matatizo yake hasa ukitilia maanani magonjwa mbali mbali ya zinaa yaliyopo.

  Pia kuna swala la kuzeeka, research nyingi zinaonyesha watu ambao wamo kwenye ndoa wanaishi maisha marefu ukilinganisha na wale ambao hawamo katika ndoa.

  Pia kuna swala hili la kuwa na watoto. Haipendezi kwa mwanaume au mwanamke kuwa na watoto na wanawake/wanaume tofauti hata namna ya kuwalea na kuwapa matunzo mazuri inakuwa ngumu sana ukilinganisha na hao watoto kuzaliwa na Baba na Mama mmoja.

  Life is so sweet if you share with your friend!! that is always true Shishi especially if that friend treats you with respect and loves you truthfully.
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Chaku,

  Ningependa kukupatia ushuri na labda ushuhuda wa nini kiko kwenye ndoa. Lakini mada yako inaonesha mtazamo hasi kuhusiana na suala la ndoa. Kwa sababu hiyo naweza kukuambia kuwa hata uishi miaka 200 hutaweza kupata majibu ya maswali yako isipokuwa ukifanya uamuzi wa kuingia kwenye ndoa ili uone mwenyewe. Majibu yote utakayopata hayatakusaidia. Kila ndoa ni unique kwa hiyo kila mtu analo lake. Ila kwangu mimi, kila kitu ninachopata kwenye ndoa ni raha tupu!
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa sana Ndugu hii sasa ni sexism,yaani makombo ale mwanaume na mwanaume je ambaye kabla ya ndoa anakuwa keshabanjuka na midemu lukuki mbona kina mama hawasemi?
   
 20. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Ndoa nyingi kwa kweli ni shughuli hasa hizi za dot com maana wote mke mume wajanja watupu na walifahamia kama sio Garden Bistro basi ni ukumbi wa Maisha au Billicanas.Undava undava tu wanavyoishi mme akiomba afuliwe anajibiwa 'kwani huoni washing machine?,mke naye akitaka lotion anaambiwa 'kwani hufanyi kazi?' kaaaaaaaaaaaaaaazi kweli kweli.
   
Loading...