A-town
JF-Expert Member
- Oct 25, 2011
- 494
- 169
Sijui ni kwa sababu ya mapenzi yangu katika lugha ama nini. Lakini huwa nikikutana na daladala, bodaboda au lori lilioandikwa kitu basi ni lazima nisome. Siishii hapo, huwa najiuliza maana ya msemo au andiko hilo na kujiuliza huyo aliyetaka ƙiandikwe hivyo alikuwa anawaza nini? Yapi yalimkuta? Halafu miye huangalia maana yake kwa kuangalia experience ya maisha yangu.
Mara zote tunaamini kimtokacho mtu ndicho kilichomjaa moyoni na kichwani of course. Huwezi kuzungumza kitu usichokuwa nacho kichwani kwako. Ukiona mtu anaongea 'pumba' ujue ndizo zilizopo kichwani. Ukiona mtu 'anatema madini' ujue ndiyo yaliyomo kichwani kwake kutokana na uzoefu wa maisha kwa kuishi, kusimuliwa, kusoma au kuangalia kwa kideo. Hivyo haya maandishi hutokana pia na hali hiyo.
Juzi fulani nikakutana na hii "kunywa mtori, nyama zipo chini.." hahaha.. Nani asiyejua watu wapendavyo nyama? Wakumbuka siku za nyama shuleni kule boarding?? Yaani ilikuwa ni sherehe.
Sasa wanunua mtori umejaa bakuli na nyama huzioni, usiwe na shaka...nyama zipo chini. Kunywa mtori utazikuta.
Maisha ni kama mchanganyiko wa mtori na nyama. Utaanza kwa shida ila kwa juhudi zako za kumaliza mtori ndizo zitakukutanisha na nyama. Juhudi zako za kufanya kazi na kutimiza ndoto zako pasipo kukata au kukatishwa tamaa zitakukutanisha na maisha bora uyatakayo.
Kila mtu ana mtori wake.
� kazi yako ndio mtori wako
�masomo yako ndio mtori wako
�biashara yako ndio mtori wako
Komaa rafiki...piga kazi. Soma kwa usongo..boresha biashara yako kila kukicha. Usikate wala kukatishwa tamaa. Usiache kujifunza na kufanyia kazi ujifunzacho.
Maliza mtori huooo..nyama zipo chini.
#SimamaJipangeSongesha