askarikambi
JF-Expert Member
- Dec 22, 2013
- 246
- 264
Heshima kwenu,
Jana kwenye maongezi ya kirafiki na bi dada mmoja, alinieleza jambo lililonifanya nishangae kidogo na hata nilipobisha(japo sikuwa na data za kubishia) bado alisisitiza kuwa anachosema ni kweli.
Kama swali nilivyoliweka hapo juu, anadai kuwa, mwanamke anaponyonyesha mtoto wake vizuri kwa kuzingatia muda na wakati wa kunyonyesha, hawezi kushika mimba kwa kipindi cha miaka miwili ya unyonyeshaji hata akiingiliwa na mwanaume bila kinga, bila kuzingatia siku zake za hatari.
Najua humu wapo wengi waliowahi kunyonyesha, na wengine ni wataalamu wa mambo ya uzazi. Nimeona badala ya kuendelea kubisha (kukataa) ni bora niwaulize wajuzi wengine kwani hii sikuwahi kuisikia kabla.
Je, ni kweli kunyonyesha kwa kuzingatia utaratibu mzuri wa unyonyeshaji kunazuia uwezekano wa mama kupata mimba kwa kipindi hicho?