Kunuka miguu: Chanzo na tiba

Achukue unga wa muhogo apake kwenye miguu pamoja na mafuta yoyote yanazi ama vasseline akishapaka anavaa soksi na Viatu hadi jioni anarudi kuoga anasafisha na kukausha vizuri anaweza paka pia Uck anapolala
 
Kama hakuna ulazima wa kuvaa viatu vilivyo funika aache awe anavaa viatu wazi( open shoes) nadhani vyaweza kusaidia
 
sallute wakuu...naomben msaada wenu nina kijana wa age 21yrs ana tatizo la kunuka miguu..yaan akivua viatu hapo ndan hakukaliki, miguu anaosha vizur na kabla ya kuvaa viatu hua anaikausha vizuri tu. je tatizo labda ni nini na dawa yake ni nini,,,msaada mwenye kujua
Pole sana sio lazima useme kijana ata kama tatizo ni lako.tumia majani ya chai,nunua au pata majani kidogo ya chai safisha miguu paka mafuta vizuri chukua majan kidogo weka katikati ya kidole na kidole kwa miguu yote na vidole.vaa soksi.fanya hivyo siku mbili mfurulizo.utapona
 
Hiyo dawa ni kiboko akiendelea kunuka baada ya matumiza basi tatizo lake halina tiba kokote duniani
 
Mkuu huyo kijana huwenda haoshi vizuri hiyo miguu ananawa juu juu tu ndio maana hiyo hari haiishi,jambo la kufanya ni
*kunawa miguu vizuri hasa katikati ya vidole na unyayo
*kukausha miguu vizuri hasa katikati ya vidole na kupaka mafuta
*ajitahidi kuvaa soksi safi na viatu visafi au apendelee kuvaa viati vya wazi.
Akifata hivyo mambo yatakaa sawa.
Correct kwa kuongezea atumie Mycota Powder... Maduka ya Dawa ni 28,000/- tu
 
Wadau naombeni ushauri nina ttzo la kunuka miguu wapendwa hata kama sijavaa viatu yaaan nakosa amani pale ninapofanyiaa kazi
Nina socks sio chini ya pea kumi viatu kama pea sita hv nabadilisha frequently lakin haisaidiaaa nimejarbu matumizi ya powda na madawa mengine lakini sijaona matokea chanyaa
Ukweli nimekuaa wa kukosa amani kuanziaa siku inapoaza hadi kuishaaa naombeni msaada wa mawazo jamani niondokane na hii hali

Sikua na hili ttzo mwanzo ilaa nina muda kama week mbili sasa tangu linianze.
 
Mkuu pole sana
Labda unisaidie haya machache ili tuweze jua tatizo ni nini

Una tatizo la fungus miguuni?

Unavaa soksi za mpira au cotton?

Kama hukuwa Na hili tatizo mwanzo inawezekana hivo vitu viwili apo juu vimechangia, kama upo dar kwa Sasa joto limeongezeka sana hivo ni rahisi sana miguu yako kusweat Na kusababisha harufu especially kama Huwa unatembea sana kipindi kama hiki

Ushauri wangu nenda hosp iliyokaribu Na wewe muone daktari mueleze tatizo lako unaweza pata msaada

Pole sana mkuu harufu mbaya husababisha kuto jiamini kabisa maana kila wakati unahisi kama jirani zako wanasikia iyo harufu
 
Ahsantee mkuu siko dar ndugu yangu yeah niliuguaa fungus nikaponaa ila harufu tu miguuni ndo imegomaa kuondoka
Najarbu kilaa namnaa mkuu nakosa kujiamini kabisa mkuu ilaa naplan kwenda hospitali kwa matibabu zaidiii
Kwa sasa navaa soks cotton na ukweli sitembei sanaa mda mwingi nakua ofisini tu pale japoo kuna kuaa na jotoo na mm nasweat
Ilaa mkuu nashkuru kwa ushaur wako.
 
Ahsantee mkuu siko dar ndugu yangu yeah niliuguaa fungus nikaponaa ila harufu tu miguuni ndo imegomaa kuondoka
Najarbu kilaa namnaa mkuu nakosa kujiamini kabisa mkuu ilaa naplan kwenda hospitali kwa matibabu zaidiii
Kwa sasa navaa soks cotton na ukweli sitembei sanaa mda mwingi nakua ofisini tu pale japoo kuna kuaa na jotoo na mm nasweat
Ilaa mkuu nashkuru kwa ushaur wako.
Pole sana kama umewahi ugua fungus Basi yawezekana iyo ni moja wapo ya tatizo lako Na pia yawezekana hao fungus hawajapona vizuri hivo rudi tena Hosp wakati ukiendelea weka mazingira ya usafi wa miguu yako vizuri zaidi, mafuta ya mnyonyo ni mazuri kwa kutibu fungus waweza paka ayo muda wa usiku ukiwa walala mkuu inaweza saidia
 
Back
Top Bottom