Kunguru kunidonyoa kichwani

Kuna kugurua alikuwa na vitoto vyake kwenye mti karibu na kwangu,ilikuwa kama kituo yao ,nikaamua kuu vitoto vyake aisee waliitana ili nisimalize hiyo shughuli,wanakupiga na mbawa hasimami mwingine naye anakuja walinichangia kwa zamu ila niliua vitoto ,mwisho wa siku wamehama wote hamna hata moja.
 
Utakuwa umewahi kuharibu kiota chao au kuua kunguru, kunguru wakikujua wanafahamishana na wako makini sana kukutambua na huitana wakikuona hata ukijaribu kujibadilisha kimavazi, ukitaka wakuogope beba manati.
Kachome sindano ya pepopunda (tetenasi) vinginevyo unaweza ukafa kimzahamzaha.
Aisee hawa kunguru walimlia houseboy wangu vifaranga wa kuku sasa naona kuna Kiota Chao hapa home na ninasikia vifaranga vyao wakilia. Nawalia timing wakijua kidogo niwaonyeshe KAZI. Kunguru kwangu asikanyage kabisa. Yaani wameweka makazi kwenye mwembe home siwataki kabisa. Nasikia ukiua mmoja ukitundika hawaji tena wanahama. Tofauti na hapo mnipe mbinu nyingine ya kuwahamisha kwa Amani.
 
Pole ndugu! Kwanza si kawaida kwa kunguru kufanya hayo lakini pia si kwa mara moja tu umefanyiwa hilo. Maana ya kujirudia ni kuwa unahakikishiwa au unapewa msisitizo kuhusu hilo jambo kuwa hakuna utani.
Lakini kwenye neno la Mungu yapo majibu.
1. Kwanza kinachoshambuliwa ni fikra au fahamu zako. (Kwa sababu kilichoshambuliwa ni kichwa)
2. Pili ni adhabu kutoka na kosa ambalo mtu anakuwa amefanya. Ukitazama Kitabu cha Mithali 30:17 "Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila."

Kwenye neno "jicho" hapo juu weka neno "kichwa"

Kuna mama mmoja mwaka jana namaanisha 2020 alikuwa anasumbuliwa sana na ugonjwa fulani alipopelekwa hospitali ya kwanza Kunguru wakawa wanajazana juu ya lile jengo alimolazwa. Baadaye wakaona wamuhamishe wampeleke hospitali fulani ya Rufaa nako kunguru wakahamia juu ya jengo alikolazwa yule mama. Ndugu yake akawa anamsimulia hiyo habari muinjilisti mmoja ambaye ni mtumishi mwenzangu katika kituo ambacho nilikuwa nikifanyia kazi na ikawa ndiyo msaada kwao maana ndiye aliyewaongoza cha kufanya hata yule mgonjwa akapona.

HATUA ZA KUCHUKUA
Jitafakari ni wapi umemkosea Mungu kwa namna yoyote ile mfano
1. Umedhulumu mtu
2. Umemwibia mtu
3. Kama upo kwenye ndoa angalia mkeo au mumeo umemfanyia nini?
4. Watoto umewafanyia nini?
5. Nenda mbele zaidi kujitafakari mwenyewe ukimuomba Roho mtakatifu akukumbushe
6. Ukushajua makosa yako tubu na ugeuke(uache huo uovu)
7. Achilia damu ya Yesu Kristo kwenye mlango uliofunguka hata ukaletewa mashambulizi hayo ili ufungwe na usishambuliwe tena.
8. Omba Mungu kwa jina la Yesu Kristo akuondolee madhara ya mashambulizi uliyoyapata.
9. Omba Mungu akuongezee ulinzi wa kimbingu.
10. Acha kabisa uovu na umgeukie Mungu.
Mimi siku Moja kunguru alininyea. Hahaha. Nilikuwa nimekaa ghafla kimba ya kunguru kwenye bega. Yaani houseboy wangu ana vikuku vyake hivyo kunguru wanapenda kutembelea Sana maeneo ya home na kuna mwembe ndiyo burudani Yao. Hata ufukuze vipi wanakimbia na kurudi.
 
Kuna kugurua alikuwa na vitoto vyake kwenye mti karibu na kwangu,ilikuwa kama kituo yao ,nikaamua kuu vitoto vyake aisee waliitana ili nisimalize hiyo shughuli,wanakupiga na mbawa hasimami mwingine naye anakuja walinichangia kwa zamu ila niliua vitoto ,mwisho wa siku wamehama wote hamna hata moja.
Masikini, sa kwanini uliwaua?
 
Niliwahi kupita pembeni ya kinda la kunguru ambae alikua kaanguka baada ya kujaribu kuluka,baas mama yake akanifukuza flani hivi,mm nikajua yameisha kumbe vita ndio inaanza,mwez mzima yule kunguru ana niwinda, aaah nikahama njia dadeki
 
Habarini! hivi hili swala la kunguru kukudonyoa kichwani Lina maana gani? Mara ya kwanza kunitokea nikafikiri kwa vile nilivaa shati jeusi, lakini Leo pia imenitokea Cha kushangaza ni Mimi tu wengine hawadonyolewi
Pengine uliwahi kuuwa kunguru mwenzao au uliwatupia mawe hivyo wamekukariri.
 
Niliwahi kupita pembeni ya kinda la kunguru ambae alikua kaanguka baada ya kujaribu kuluka,baas mama yake akanifukuza flani hivi,mm nikajua yameisha kumbe vita ndio inaanza,mwez mzima yule kunguru ana niwinda, aaah nikahama njia dadeki
Ha ha ha.

Kwa hiyo kunguru kakuhamisha njia
 
Utotoni niliwahi kukamata kitoto cha Kunguru, aisee wale Jamaa pamoja na kukaachia katoto kao ila waliniwekea Bifu karibia wiki nzima, kila nikikatiza maeneo yao walikuwa wananivagaa na kunipa ambush hasa maeneo ya kichwani.. Ikabidi nibadilishe njia Kwa muda..
Ha ha ha
 
Habarini! hivi hili swala la kunguru kukudonyoa kichwani Lina maana gani? Mara ya kwanza kunitokea nikafikiri kwa vile nilivaa shati jeusi, lakini Leo pia imenitokea Cha kushangaza ni Mimi tu wengine hawadonyolewi
Angalia mwenendo wa maisha/tabia yako mkuu! Penda kutenda matendo mema epuka matendo mabaya!

Na kama kuna mahali ulidhurumu au kuiba nenda ukarudishe...au nenda kanisani ukatubu na kumrudia Mungu.

USICHUKULIE POA!
 
Beef lao si la kitoto
Alafu wakikuandama
Wanakuchoresha tu machoni
Mwa watu

Ova
 
Back
Top Bottom