Kunguni na Mende ndani ya basi la abiria!

Kunguni na Mende ndani ya basi la abiria!

Hivi majuzi nilibahatika kuzunguka baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara/Tanganyika kwa kutumia usafiri wa mabasi ya abiria.

Cha kusikitisha basi moja la kampuni fulani nililopanda lilikuwa na kungunguni wengi ajabu. Kunguni wale hawakuwa na aibu walikuwa wanatoka kwenye ma'cover'/foronya ya/za viti vya basi hilo na kung'ata mchana kweupe.

Wakati tunaanza safari hiyo basi lilikuwa halijajaa, Baada ya kuwastukia kunguni wale kwenye siti yangu nikaamia kwenye kiti/siti nyingine, kule ndo nikakumbana na kunguni watoto lakini 'barubaru' kwa kung'ata, Nikarudi kwenye siti yangu ya awali.

Sikuvumilia kung'atwa na kunguni wale bila kulalamika, nilimuita konda kumueleza kero ya kunguni kwenye basi lake. Kwa siri , konda, nikamuonyesha kikosi cha kwanza cha kunguni kilichokuwa kwenye egemo la mgongo wangu waliojibanza karibu na tobo la foronya la siti yangu. Akashtuka 'kiana', alichosema nikuwa basi lile alikabidhiwa jana yake.

Na jana hiyo kazi aliyoanza nayo ni kupambana na mende kwenye basi hilo waliokuwa wengi kiasi cha kutishia abiria kususia basi. Akanihakikishia kuwa na hao mende hakuwamaliza vizuri.

Mwisho wa mazungumzo yetu alimrudikia konda aliyekuwa anasimamia basi hilo hapo awali kwa usumbufu huo. Nilichokifanya, tulipofika sehemu ya kuchimba dawa, mimi nilishuka kwenye basi hilo na kwenda kuchimba namba za gari/basi hilo maana walikuwa hawajaandika namba za basi hilo kwenye tiketi/risiti ya nauli ya basi.

Nilisafiri kwenye basi hilo nikiwa roho juu, ingawa haikuwa mara yangu ya kwanza kuumwa/ng'atwa na kunguni! Niliwahi kungatwa nilipokuwa shule ya Bweni enzi hizo.

SWALI KWA WADAU:

1. Ni nani anahusika kuwawajibisha, wamiliki, makonda, hata madereva wa mabasi yenye kuhatarisha afya za wasafiri?

2. Mimi kama abira sikunyingine nikikumbania na kadhia ya namna hiyo nikashtaki wapi ili wawajibishwe wahusika kwa uzembe huo?

USHAURI:
Abira wote wa vyombo vya usafiri kuweni makini mnapopanda vyombo hivyo kwa kuhakikisha havina vihataraishi vya afya zenu kama, kunguni, mende, nakadhalika.

Update:
=======
Kama nilivyoahidi: ZUBE TRANS (Moshi-Mwanza), siti namba F1, T954 AHH: nauli 35,000/=


Hilo basi linatakiwa lifanyiwe fumigation, au ndiyo mpaka dengue ije tena? hahaha mwanza - moshi , tsh 35,000/- that's why
 
Nadhani uko sahihi...nitataja jina la kampuni, namba ya gari, na namba ya siti lakini sitataja ilikuwa tarehe ngapi nilisafiri na basi hilo ingawa ni mwaka huu. Nitafanya hivyo kesho baada yakusikia maoni ya wadau wengine juu ya hili.

Acha uoga nyie ndiyo wale wale baada ya basi kupata ajali na kunusurika wakati wa kuhojiwa na waandishi mnaanza kusema oooh dereva alikuwa anaendesha kwa speed ya juu
 
Nadhani uko sahihi...nitataja jina la kampuni, namba ya gari, na namba ya siti lakini sitataja ilikuwa tarehe ngapi nilisafiri na basi hilo ingawa ni mwaka huu. Nitafanya hivyo kesho baada yakusikia maoni ya wadau wengine juu ya hili.

Mkuu lengo sio kuharibu biashara ya mtu bali ni kurekebishana. Huenda hata tajiri hajui kwamba bus lake lina hayo matatizo, ila kwa kulitaja utakuwa umemshtua kwa namna moja. Lakini pia utakuwa umesadia pia wengine waweze kufanya fumigation kwenye bus zao.

Shukran!
 
Imewahi kunitokea, toka Singida to Mwanza lile basi nje safii ila ndani...
^^
 
kunguni na mende mnaleta abiria wenyewe,mana mnasafiri na makuku,mambuzi,maviporo,mavitanda,magodoro,mashuka,mabata,wengine manguo machafu,wengine hamuogagi,etc.
Itabidi ianze kufanyika inspection kwa abiria kabla ya kupanda basi,kama hujaoga hakuna kupanda!!
 
Back
Top Bottom